Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam


Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam. Allah(s.w) akaikubali ile nadhiri na dua ya mama yake Maryam.Basi Mola wake akampokea (mtoto) kwa mapokezi mema na akamkuza kwa makuzi mema, na akamfanya Zakaria awe mlezi wake. Kila mara Zakaria alipoingia chumbani(kwa Maryam) alikuta vyakula pamoja naye. Akauliza: “Ewe Maryam! Unapatawapi hivi? Akajibu: “Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila kutarajia(3:37)Aya hizi zinatuonesha kuwa Maryam alikuwa katika malezi mema na uangalizi wa karibu toka kwa Nabii Zakaria(a.s) kiasi cha kuepusha mazingira ya ufuska yasimfikie.Allah(s.w) aliweka maandalizi haya mapema ili atakapoleta muujiza wake kwa Maryam kuzaa mtoto bila ya kuwa na mume isionekane kuwa alikuwa mzinifu, bali iwe ni dalili ya kuwepo Allah(s.w) mwenye nguvu na uwezo wa kila kitu.Kutokana na mazingira hayo na hifadhi ya Allah(s.w) Maryam akakua vyema na kupata hadhi ya kuwa mwanamke bora kuliko wanawake wote:

“Na (kumbuka) Malaika waliposema: “Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa ulimwengu (wote).(3:42)