image

Hawa ndio waaasi wakwanza wa Dola ya kiislamu wakati wa makhalifa

Hawa ndio waaasi wakwanza wa Dola ya kiislamu wakati wa makhalifa

Uasi wa Dola (Riddah)



Habari za kutawafu kwa Mtume(s.a.w) zilipelekea makabila mengi ya Kiarabu yaliyokuwa chini ya himaya ya Dola ya Kiislamu kuasi. Tukio hili katika vitabu vya tarekh huitwa Riddah kwa Kiarabu na apostasy kwa Kiingereza.


Kwa ujumla dola ya Kiislamu wakati wa ukhalifa iligawanyika katika makundi sita ya watu. kuna waliobakia na Uislamu wao bila kutetereka hasa watu wa Madina, Taif na Makka. Wanafiki ni kundi lililokuwepo na hila zao za mwisho ziligonga ukuta mwaka mmoja tu kabla ya kutawafu kwa Mtume(s.a.w). Hivyo walikuwa macho kuvizia fursa yoyote iliyopatikana waitumie. Kulizuka kundi la Waislamu waliobakia Waislamu lakini walikataa kupeleka Zaka Madina kwa hoja kuwa itumike kuwasaidia wasiojiweza katika eneo lao.


Wapo waliobaki Waislamu lakini walikataa kulipa Zaka kabisa. Kundi lingine ni lile lililoritadi na kurudia dini zao za asili. Kundi lingine ni wale mitume wa uwongo alioanza tangu wakati wa Mtume na sasa wakaongezeka kufikia wanne. Ikumbukwe pia wakati wa majilio ya wajumbe mbali mbali kwa Mtume(s.a.w) yapo makabila ambayo hayakusilimu ila yaliitambua Dola ya Kiislamu wakawa wanalipa Jizya. Mfano ni kabila la Hanifa la sehemu ya Arabia ya kati. Wayahudi nao ambao siku zote walikuwa maadui wa Mtume(s.a.w) si kuwa tu wametolewa Madina lakini hata huko Khaibar walikohamia walishindwa na kulazimishwa kuutambua utawala wa Kiislamu na kulipa Jizya.


Sio Wayahudi tu bali Wakristu wa Najran na Urumi waliazimia kuiangamiza dola ya Kiislamu kwa vile wote walikuwa wanalipa Jizya. Hivyo ni dhahiri uasi katika dola ya Kiislamu ulikuwa mkubwa. Dola yote ya Kiislamu ilisambaratika, maadui walikuwa wengi na waliobakia na utii kwa Dola ni miji baina ya Madina, Makka na Taif. Kabla ya kutazama hatua alizochukua Abubakr Siddiqi ni vyema kwanza tuchambue sababu zilizopelekea uasi huu.


Sababu zilizopelekea Uasi


Kwa wale waliosilimu kisha baada ya kutawafu Mtume walikataa kulipa Zaka na wale waliokubali kulipa Zaka lakini wakajenga hoja kuwa hawatapeleka Madina lakini itumike kwa watu wao; makundi yote haya Sababu yao kubwa ya kufanya hivi ni udhaifu wa Imani kama isemavyo Qur’an:


Walisema wanaokaa jangwani (kumwambia Mtume) “Tumeamini” Sema uwaambie Hamjaamini, Lakini semeni Tumesilimu maana imani haijaingia nyoyoni mwenu bado.......... (49:14).


Ama kwa wale waliorudia dini zao za awali walikuwa na sababu mbili, moja ya kiuchumi ya kulinda biashara zao na mali zao kwa kuondokana na kulipa Jizya na pili kulinda hadhi zao na nafasi zao katika koo na mila . Sababu hizi pia ndizo zilizopelekea uasi kwa wale waliokuwa hawakusilimu lakini walikuwa wanalipa Jizya. Na kwa wale waliodai utume na walioungana nao pamoja na sababu zilizotajwa walikuwa na husda na uroho wa mamlaka. Bado ipo hoja inayowahusu Waarabu wote, wengi wao walizoea maisha yasio na mpangilio maalum, yasiyo na nidhamu na hawakuzoea kutoa utii wao nje ya koo zao au makabila yao.


Mabadiliko yaliyoletwa na Mtume(s.a.w) yaliwaweka katika mfumo wa maisha wenye nidhamu wasioitaka. Waliukubali wakati wa Mtume(s.aw.) kwa kuwa walikuwa hawana jinsi. Kutawafu kwa Mtume(s.a.w) kulitoa nafasi siyo tu ya kujitenga na utawala wa Madina bali walikusudia kuuhilikisha kabisa. Kwa upande wa Wayahudi na Wakristu ni kweli waliasi kulinda tawala zao na utukufu wao lakini kulinda dini (itikadi) zao pia kulitoa msukumo mkubwa. Sababu hizi na nyinginezo ambazo huenda hatukuzitaja zaweza kuwa ndio chimbuko la “Riddah”.





                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 687


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HISTORIA NA VISA VYA MITUME, MANABII NA WATU WEMA WALIOTAJWA KWENYE QURAN
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KATIKA HARAKATI ZA KULINGANIA DINI
Soma Zaidi...

Mbinu walizotumia makafiri wa kiqureish katika kuupinga uislamu makkah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)
Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a. Soma Zaidi...

Uchaguzi wa Ali bin Abu Twalib kuwa Khalifa wa nne na chanzo cha Makundi katika Uislamu
Soma Zaidi...

Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Harun(a.s), Achaguliwa Kuwa Msaidizi Musa(a.s) na kumkabili (kumlingania) firauni
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

Kulingania Uislamu kwa Jamii Nzima
Baada ya miaka mitatu ya Utume, Muhammad(s. Soma Zaidi...

Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...

Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri
Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a. Soma Zaidi...

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa
Soma Zaidi...