Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula uyoga
Uyoga (mushroom)
Uyoga pia ni katika vyakula vya asili, ijapokuwa upatikanaji wake umekuwa mchache siku hizi. Shukrani ziwaendee wataalamu wa kilimo, kwa sasa tunaweza kuzipata mbegu za uyoga kutoka maabara na kulima uyoga popote pale. Wataalamu wa mimea wanaamini kuwa uyoga si katika mimiea kwani uyoga upo katika kundi la viumbe liitwalo fungi (kingdom fungi). ila tunapozungumzia vyakula uyoga tunauweka kwenye kundi la mbogamboga. Uyoga una virutubisho vingi na vizuri kwa afya.
Kulinda mwili zidi ya cancer, Kama ilivyokuwa kwenye matunda na mboga zingine kuwa kuna antioxidant ambayo hii ni chembechembe inayopambana na sumu na kemikali ambazo zinaweza kuathiri seli za mwili wako. Basi kwenye uyoga pia kuna antioxidant kama iliyo karoti na matunda mengine tuloona hapo juu. Hii husaidia kwa kiwango kikubwa kupambana na kuuwa seli za kansa au saratani ambazo zinatengenezwa mwilini.
Mna kwenye uyoga madini yanayoitwa selenium, madini haya huwezi kuyapata kwenye matunda mngi sana na mbogamboga nyingi lakini haya utayapata kwa urahisi kwenye uyoga. Madini haya husaidia katika kuuwa seli sa saratani, pia kuzuia kuota kwa uvimbe unaosababishwa na saratani na aina zingine za vimbe.
Uyoga una vitamin D, ambavyo hivi pia husaidia katika kupambana na kuthibiti kukuwa kwa seli za saratani mwilini. Vitamin D husaidia katika utendaji mwema wa kazi za DNA. Itambulike kuwa saratani huanza kuathiri DNA ndio baadae huendelea kukuwa ndani ya mwili na baadae kuathiri sehemu za mwili. Hivyo uyoga una chembechembe hizi ambazo husaidia katika kupamba na nsa saratani.
Uyoga husaidia katika kuthibiti na kupamabana na kisukari hususan type 2 diabetes. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa ulaji wa vyakula vyenye kambakamba (fiber) husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Hivyo husaidia katika kuimarisha afya ya itengenezwaji wa insulin.
Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo, uwepo wa lkambakamba, madini ya potassium pamoja na vitamin C husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha afya ya moyo (cardiovascular health). ulaji wa vyakula vyenye madini ya potassium kwa wingi pamoja na sodium kwa kiwango kidogo husaidia katika kupunguza shinikizo la damu hivyo husaidia kwa wale wenye presha ya kupanda ya damu.
Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (immune system). madini ya selenium yaliyomo kwenye uyoga kusaidia katika kushawishi na kustimulate mfumo wa afya mwilini katika kupambana na wadudu wavamizi. Madini haya husaidia katika kusahwishi T-cell au CD4 katika kupambana na wadudu wavamizi kama bakteria, virus na fangas. Beta-glucan inayopatikana kwenye ukuta wa seli za uyoga husaidia katika kuufanya mwili upambane vyema na wavamisi na kupamba nna na vijidudu vya maradhi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za upungufu wa iodini ambapo kitaalamu hujulikana Kama goiter. Goiter Ni Sababu ya kawaida ya goiter duniani kote ni ukosefu wa iodini katika chakula. Nchini Marekani, ambako utumiaji wa chumvi yenye iodini ni j
Soma Zaidi...Hii ni orodha ya vyakula salama na vizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha
Soma Zaidi...Je umesha wahi kujiuliza kuwa ni vinywaji vipi mwenye presha ya kupanda anafaha kutumia, Unadhani ni maji, mvinyo wa pombe, chai na kahawa. Bila shaka ungependa kujuwa zaidi kuhusu jambo hili. Makala hii ni kwa ajili yako
Soma Zaidi...Fida za matunda huanzia kwenye rangi zake, je unajuwa kama rangi ya matunda inaeleza jambo?
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha madhara ya kuwa na mafuta mengi mwilimi
Soma Zaidi...