picha

Boga (pumpkin)

Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula maboga

 Boga (pumpkin)

Boga ni katika vyakula vya asili walivyotumia mababu zetu toka enzi za zamani sana. Boga ni katika chakula chenye vitamin A. pia boga husaidia katika kushusha presha kwani mna kwenye mbegu za maboga aina ya mafuta pytoestrogens ambayo ndio hupunguza shinikizo la damu (hypertension).

 

Maboga husaidia katika ku[ata usingizi mnono kwani mna kwenye mbegu za maboga typtophan aina ya amino asid ambayo husaidia katika kurelax. Pia mna beta-carotene na aina zingine za antioxidant ambazo husaidia katika kuzuia kupata cancer.

 

Maboga ni muhimu katika kuboresha na kuimarisha afya ya nguvu za kiume. Pia chakula hiki ni muhimu kwa afya ya moyo. Kwani kutokana na kambakamba zilizomo kwenye maboga mlaji anakuwa na nafasi ndogo sana ya kuweza kupata mabonjwa ya moyo (coronary heart diseases).

 

Chakula cha maboga pia husaidia katika kuzuia na mlaji kupata ugonjwa wa kisukari. Pia huimarisha vyema afya ya mwenye kisukari. Chakula hiki husaidia katika ufyonzwaji wa glucose kwenda kwenye tishu za mwili. Pia husaidia katika kubalans kiwango cha sukari ndani ya mwili.

 

Maboga husaidia katika kuboresha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (immune system). kwani vitamin C pamoja na beta-carotene husaidia mara dufu katika kuimarisha mfumo wa kinga ili kuweza kupambana na maradhi mbalimbali mwilini. Isitoshe beta-carotene kuweza kubadilishwa kuwa vitamin A, na hali hii huweza kusaidia katika kuzalishwa kwa seli hai nyeupe mwilini ambazo ndio hupambana na maradhi na vijidudu vishambulizi kama bakteria, fangas na virusi

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 3890

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 web hosting     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Faida za kiafya za kunywa chai

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa chai

Soma Zaidi...
Zijuwe kazi na faida za Vitamini C mwilini

Vitamini C ni moja kati ya vitamini muhimu sana katika kuboresha ufanyaji kazi wa mfumowa kinga mwilini yaani immune system. Katika post hii utakwenda kujifunza kazi za vitamini C mwilini

Soma Zaidi...
Faida za kunywa maji kabla ya kula chochote.

Posti hii inahusu faida za kunywa maji kabla hujula kitu chochote,tunajua kabisa kabla ujala au kunywa chochote sumu nyingi mwilini zinakuwa hazijachanganyikana na chochote kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa kuna faida kubwa nyingi za kunywa maji kama ifuatavy

Soma Zaidi...