Makala hii inakwenda kukupa elimu juu ya vyakula na vinywaji vilivyo salama kwa mtu mwenye kisukari, na ni vyakula vipi ni hatari kwa mwenye kisukari. Pia utajifunza njia za kujilinda na kupata kisukari.
VYAKULA SALAMA NA HATARI KWA MWENYE KISUKARI
Kisuari ni hali ya mwili kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari hivyo kuachia sukari yote kuishia kwenye damu bila ya kuingia kwenye seli ili kutumika maeneo mbalimbali ya mwili. Na hutokea endapo uzalishwaji wa homoni ya insulini utakuwa katika shida. Eidha hutokea kwa sababu homoni ya insulini inayozalishwa si yenye kutosheleza ama mwili wenyewe unashindwa kuitumiahomoni ya insulini. Homoni ya insulin ndio ambayo hudhibiti kiwango cha sukari.
Vipi kisukari hutokea?
Mwili unahitaji sukari kwa ajili ya kuzalisha nishati yaani nguvu. Mwili pia unahifadhi sukari kwa matumizi ya baadaye. Endapo sukari mwilini itakuwa ni nyingi basi homoni ya insulini huzaliwa kwa wingi ili kupunguza sukari iliyozidi n akuihifadhi kwa matumizi yaa baadaye. Na endapo sukari itakuwa ni kidogo mwilili homoni ya insulini huzuiliwa hivyo mwili hutumua sukari iliyohifadhiwa. Kwa kufanya hivi kiwango cha sukari hudhibitiwa.
Sasa endapo kutatokea shida yeyote katika matumizi ya homoni ya insulini mwili utashindwa kuhifadhi sukari pia kuitumia sukari. Hivyo sukari itabakia kwenye damu bila ya kwenda kokote kwa matumizi. Hali hii ikitokea ndipo mtu huambiwa ana kisukari. Kisukari kinaweza kuwa ni kwa muda mfupi kama kwa baadhi ya wajawazito. Pia kinaweza kuwa ni cha kudumu, na hapa tunazungumzia type1 na type 2.
Mtu mwenye kisukari anatakiwa kuwa makini sana katika matumizi ya vyakula na vinywaji. Vinginevyo anaweza kuingia kwenye matatizo makubw aya kiafya. Je unavijuwa vyakula salama kwa nmwemye kisukari? Na je unavijuwa vyakula hatari kwa mwenye kisukari? Endelea na makala hii hadi mwisho:-
VYAKULA SALAMA KWA MWENYE KISUKARI
1.Samaki hasa wale wenye fati kwa wingi kama samlon na sardines
2.Mbogamboga za majani
3.Palachichi
4.Mayai
5.Mbegu za chia
6.Maharagwe
7.Kitunguu thaumu
8.Nyama yandege wafugwao kama kuku
9.Kahawa
10.Vinywaji visivyowekwa sukari
11.Jusi za mbogamboga
12.Usikoboe mahindi, mchele, na mtama
13.Matunda kwa uchache
VYAKULA HATARI KWA MWENYE KISUKARI
1.Nafaka zilizokobolewa
2.Nafaka zilizoongezwa sukari
3.Mikate yenye sukari
4.Nafaka zisizo na kini
5.Mboga zenye chumvi nyingi
6.Mboga zilizoongezwa maziwa
7.Vinywaji vyote vya sukari usitumie mpaka kiwango chako cha sukari kiwe kipo katika udhibiti hata asali epukana nayo kwanza
8.Juisi zilizowekwa sukari ama zenye utamu kama za matunda
9.Vinywaji vya energy (energy drink)
10.Nyama ya kuoka
11.Nyama zenye mafuta mengi
12.Nyama ya ngurue
13.Maziwa fresh
14.Samaki wa kuoka
15.Soda
Njia za kujikinga na kisukari
1.Dhibiti uzito wako. Hakikisha huna uzito w akupitiliza
2.Fanya mazoezi mara kwa mara
3.Kula mlo kamili
4.Punguza misongo ya mawazo
5.Kunywa maji kwa wingi
6.Wacha kuvuta sigara
7.Punguza ama wacha unywaji wa pombe
8.Punguza ulaji wa sukari kwa wingi
9.Pendelea kunywa kahawa
10.Tumia dawa za asili kiasi uwezavyo
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...Nazi ni katika matunda bora sana kiafya, Soma faida zake kwa afya yako
Soma Zaidi...Umeshawahi kuumwa na dawa yako ikawa maji? Huwenda bado basi hapa nitakujuza kidogo tu, juu ya jambo hili.
Soma Zaidi...Tufaha ni katika matunda adimu na matamu, je unazijuwa faida zake kkiafya?
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Ukosefu wa madini ya Shaba mwilini, ni Ukosefu wa madini ya Shaba mwilini ambao usababisha madhara kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kabichi
Soma Zaidi...