Ni vyakula gani anapasa kula mjamzito, na utaratibu mzima wa lishe kwa wajawazito
Kwa ufupi ni kuwa mjamzito na anayenyonyesha wanatakiwa wapewe lishe kamili iliyokuwa na virutubisho vyote. Haata hivyo ni vyema kuzingatia nukuu za hapo chini. Wanaonyonyesha na wajawazito wanahitaji kupata vyakula vyenye viinilishe vya kutosha ili kuwezesha ukuaji wa mtoto tumboni , utengenezwaji wa maziwa na kwa ajili ya afya zao wenyewe.
Vyakula vya protini vinahitajika kwa mkiwango kikubwa ili kuwezesha mwili wa mama kujenga misuli vizuri , tishu katika mwili wake na mwili wa mtoto aliye tumboni. Utengenezwaji wa maziwa , usafirishwaji wa damu na ukuaji wa viungo vya mama na mtoto unahitaji protini. Hivyo wamama hawa wapewe protini kwa wingi.vyakula vya protini ni kama:-
A.Nyama
B.Mayai
C.Maharagwe
D.Samaki
E.Maziwa
F.Pia kwenye nafaka na baadhi ya mboga za majani na matunda.
Vyakila vya folic asid na vitamini B vinahitajika kwa ajili ya kuwezesha kupunguza tatizo la kushindwa kujifunguwa kwa njia ya kawaida. Vyakula vya madini ya kashiam(calcium) ni muhimu kwa ukuwji wa mifupa ya mtoto aliye tumboni na kuimarika mwili wa mama pia. Kwani mjamzito asipopewa madini haya mtoto atatumia madini yaliyomo kwa mama na kumfanya mama awe na mifupa dhaifu katika kipindi hiki.
Madini ya chuma ni muhimu katika utengenezwaji wa damu, halikadhalika mtoto anahitaji madini haya ili ayatumie katika wiki ya kwanza ya kuzaliwa. Madini ya zink ni muhimu katika kuwezesha kujifunguwa.(progression of labour) na ukuaji salama wa mtoto aliyoko tumboni.
Wamama wajawazito wapewe vyakula vyenye kambakamba (dietary fiber}. Hivi vitamuwezesha kutopata tatizo la kukosa choo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye ngozi wakati wa ujauzito, ni mabadiliko yanayotokea kwenye ngozi ya Mama wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa mama aliyejifungua kuanzia miezi sita mpaka mwaka mmoja.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...Makala hii itakujuza baadhi ya njia utakaoweza kuzifuata ili kukabiliana na fangasi sehemu za siri kwa wanaume
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma muhimu anazopaswa kupewa mama mjamzito wakati akiwa na mimba, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua yaani ndani ya masaa ishirini na manne, tunajua wazi kuwa Mama akiwa mjamzito anaweza kupata matatizo mbalimbali kwa h
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuhusu kwa mimba kutoka kabla ya mda wake,ni kitendo ambacho mimba utoka kabla ya wiki ishilini na na nane.
Soma Zaidi...