Sababu za kutoka mimba yenye miezi Saba na nane

Posti hii inahusu zaidi sababu za mtoto kuzaliwa akiwa na miezi Saba na nane kwa kawaida mtoto wa hivi anakuwa hajafikisha mda wake kwa hiyo uzaliwa akiwa na miezi saba na nane, kwa hiyo kuna sababu mbalimbali kama tutakavyoona

Sababu za mtoto kuzaliwa akiwa na miezi saba na nane.

1.sababu ya kwanza ni kuwepo kwa presha.

Kuna kipindi akina mama wanakuwa na presha wakati wakiwa na mimba hali inayosababisha kuzaliwa kwa watoto ndebile kwa hiyo akina mama wanapaswa kupima presha wakati wakiwa na mimba tangia mwanzoni ili kuweza kuepuka tatizo la kuwepo kwa presha wakati wa ujauzito.

 

2. Mtoto kukosa maji akiwa tumboni.

Kwa kawaida mtoto akiwa tumboni huwa na maji yake ambayo kwa kawaida maji hayo huitwa amniotic fluid ambapo maji hayo umsaidia mtoto kufanya vitu mbalimbali akiwa tumboni kwa hiyo kuna kipindi maji hayo  upungua au kuisha  kwa sababu mbalimbali na kupelekea mtoto kuzaliwa ndebile.

 

3. Kuwepo kwa Maambukizi kwenye mji wa mimba.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na Maambukizi mbalimbali kwenye mji wa mimba ambayo Usababisha mimba kutoka.

 

4. Kuwepo kwa kisukari wakati wa ujauzito.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na kisukari wakati wa ujauzito ambacho usababisha matatizo mbalimbali kwa mtoto na kusababisha mimba kutoka au kuzaliwa kwa mtoto ndebile.

 

5. Kuwepo kwa kifafa cha mimba.

Hali hii uwapata sana akina mama wengi wenye presha wakati wa mimba na kufuatia degedege wakati wa mimba hali hii ikizidi usababisha mama kujifungua mtoto ndebile.

 

6. Mfuko wa uzazi kuwa dhaifu na kushindwa kubeba mtoto.

Kuna wakati mwingine mfuko wa uzazi unakuwa dhaifu na kusababisha kushindwa kubeba mtoto akiwa tumboni hali inayosababisha kuzaliwa kwa mtoto ndebile.

 

7. Kulegea kwa mlango wa kizazi kabla ya wakati.

Kuna kipindi mlango wa kizazi unalegea kabisa kabisa kabla ya wakati hali inayosababisha kuzaliwa kwa mtoto ndebile kwa sababu mlango wa kizazi ukifungukaa na umpatia  mtoto kupita kwa urahisi.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/21/Thursday - 10:25:42 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 5592


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-