Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke

Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke

Maambukizi kwenye Njia ya Uzazi kwa kifupi hujulikana Kama PID.ni Maambukizi ya mfumo wa Uzazi yanayoathiri wanawake, Maambukizi haya kwa Kawaida huhusisha sehemu Kama shingo ya uzazi,nyuma ya mfuko wa Uzazi na mirija ya uzazi.

Zifuatazo Ni Dalili za Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke PID.

Mwanamke atakundulika kuwa na PID Kama akiwa na Dalili zifuatazo;

1.maumivu makali ya tumbo hasa chini ya kitovu. Kutokana na Maambukizi yaliyoenda kuathiri via vya Uzazi .

 

2.kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu ya rangi ya maziwa mgando. Uchafu huu hutokana na bacteria ambao hushambulia sehemu za shingo ya uzazi, nyuma ya mfuko wa Uzazi, na mirija ya uzazi na ndio maana hupelekea kutoa uchafu.

 

3.kupata homa za Mara kwa Mara. Kwasababu ya Maambukizi hayo yaliyoenda kuathiri kwenye Uzazi wa mwanamke pamoja na maumivu hupelekea kupata homa za Mara kwa mara.

 

4.kupata Hali ya kichefuchefu au kutapika. Hii Ni kwasababu mwanamke anaweza kukosa hedhi au hedhi kujirudia kwa mwezi pamoja na uchafu unayotengenezwa na hao bacteria hupelekea kupata kichefuchefu au kutapika.

 

5.kupata maumivu wakati wa kukojoa. Maambukizi haya hufanya sehemu hizo kuwa na michubuko hivyo husababisha mtu akikojoa kupata maumivu.

 

6.kutokwa na Damu wakati wa kujamiina. Damu hizi hutoka pia kwa sababu ya michubuko iliyotokea Ndani na ndio maana akijamiina anaweza Kutokwa na Damu.

 

7.kupata maumivu ya mgongo. Ni kwasababu ya Maambukizi yanayoathiri via vya Uzazi Kama shingo ya uzazi, nyuma ya mfuko wa Uzazi, na mirija ya uzazi ndio hupelekea kupata maumivu ya mgongo.

 

8.kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa au kujamiina.hii pia Ni kwasababu ya michubuko iliyotokea Ndani na iliyosababisha na Mashambulizi ya bacteria hao.

 

9.wakati mwingine Kutokwa na usaha ukeni. Uchafu ukizid na Hali hii hupelekea kutoa usaha kwa sababu ya kukosa matibabu na kukaa na Ugonjwa huu kwa muda mrefu.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 2266

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Dalili za ujauzito: Nini kinatokea kwanza

Je, unafahamu dalili za mwanzo za ujauzito? Kutoka kwa kichefuchefu hadi uchovu, ujue nini cha kutarajia.

Soma Zaidi...
Huduma kwa wanaopata hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi

Posti hii inahusu zaidi huduma kwa wanaoingia kwenye siku zao zaidi ya mara moja kwa mwezi.

Soma Zaidi...
Mambo yanayopelekea ugumba.

Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi.

Soma Zaidi...
Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito

Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo kabla ya kupata hedhi

Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba.

Soma Zaidi...