Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha

Watu wengi wamekuwa kijiuliza sana kuhusu hatma ya ujauzito kwa mwenye virusi vya ukimwi. Je ni kiasi gani mtoto aliye tumboni atakuwa salama?. ni tahadhari gani mjamzito mwenye virisi vya ukimwi achukuwe. Na atakapojifunguwa ni muda gani ataendelea kunyonyesha? Katika kipengele hiki tutaangalia kwa ufupi habari hii kama ifuatavyo:-
1.Je inawezekana kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kupata HIV/UKIMWI?
Yes inawezekana, na hili ni swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Itambulike kuwa kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika si lazima kuwa nawe utaathirika, ila kauli hii isieleweke vibaya. Kwani njia ambayo inaongoza leo katika kueneza maambukizi ya HIV ni kushiriki tendo la ndio. Mtu anaweza kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kuathirika endapo:-
A.Endapo hakutatokea michubuko wakati wa tendo
B.Endapo muathirika ametumia dawa za ART kwa muda mrefu kwa kufuata masharti hata viral load yake ikawa haionekani (undetected) na akadumu kwa hali hii walau miezi 6
C.Endapo walitumia kinga wakati wa kushiriki tendo.
2.Je HIV ma UKIMWI hupelekea mimba kutoka?
Inategemea, ila kwa ufupi HIV na UKIMWI huhatarisha ujauzito endapo muathirika hatakuwa mwangalifu ama hatafata maelekezo vyema. Wajawazito walioathirika inashauriwa wafike kituo cha afya mapema sananili kupatiwa maelekezo jinsi ya kulea mimba yake kwa usalama bila ya kuathiri afya ya ujauzito wake. Hata hivyo wanatakiwa wafuate maelekezo vyema.
3.Je maisha ya mtoto yapo hatarini endapo mama mjamzito ana HIV na UKIMWI?
Ni kweli kama mama mjamzito hatakuwa makini, anaweza kuweka maisha ya mtoto wake hatarini. Na si maisha ya mtoto tu bali hata maisha yake pia.
4.Je mtoto anapataje HIV na UKIMWI kutoka kwa mama?
A.Wakati wa kujifunguwa kama kuna kosa litafanyika.
B.Wakati wa kumnyonyosha kuanzia miezi sita toka kuzaliwa mtoto
C.Wakati wa kumlea kama mama hatakuwa makni
5.Kwa nyakati za sasa wajawazito wote wanatakiwa kuzalia kwenye kituo cha afya maalumu. Hii ni kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Hatahivyo wakunga wa jadi pia wamepatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya dharura. Ila inalazimika kwa mwenye HIV afanye juu chini azalie hospitali kwa usalama zaidi wa mtoto wake.
6.Je kunyonyesha mtoto kunawza kumuambukiza HIV?
Yes inawezekana, hata hivyo mama akiwa makini na maelezo aliyopewa, katu hatoweza kumuambukiza mwanaye. Inashauiwa mtoto kunyonya kwa muda wa miezi 6 tu ama chini ya hapo. Ni kuwa endapo mtoto atakuwa na michubukomdomoni ama tumboni.
7.Mama asimchanganyie mtoto ziwa lake, maziwa ya kopo na chakula. Kama ataamuwakumnyonyesha ndani iwe ni ndani ya miezi 6 tu na asimpe chakula chochote. Na kama ameamuwa kumpa chakula asimnyonyeshe tena. Na kama ameamuwa kumpa maziwa ya makopo ampe hayo tu na asimnyonyeshe. Anaweza kuchanganya chakula na maziwa ya kopo ama ya ng’ombe na si yake na kitu chingine chochote. Mama awe makini sana na jambo hili, asimchanganyie mtoto maziwa yeke na kitu kingine chochote. Hali hii inaweza kusababisha michubuko mdomoni ama tumboni na kusababisha kupata maambukizi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi Ute ambao umo kwenye uke, Ute huu utofautiana kulingana na hali ya mama aliyonayo, kama mama ana mimba uke utakuwa tofauti na yule ambaye hana mimba au kama Ute una una magonjwa na hivyo utakuwa tofauti.
Soma Zaidi...Inaweza kutokea ukapima mimbaikawa ipo, na baada ya wiki kadhaa unapima tena haipo. Hali hii unadhani inaweza kusababishwa na nini?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya mzunguko wa damu kwa wajawazito, tunajua wazi kuwa wajawazito pindi ujauzito ukiingia tu, kila kitu kwenye mwili ubadilika vile vile na mzunguko wa damu ubadilika.
Soma Zaidi...Kama na wewe unasumbuliwa na hali ya kupitiliza siku zako post hii itakusaidia.
Soma Zaidi...Nimesoma makala yenu, sasa nina swaliJe kitunguu saumu kina madhara kwa Mgonjwa wa figo?
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kulia
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa namaumivi wakati wa nlishiriki tendo la ndoa ama baada. Huwenda post hii ikakusaidia.
Soma Zaidi...