Posti hii inahusu zaidi athari za kuweka vitu ukeni, tunajua kwa wakati huu kadri ya kukua kwa sayansi na teknolojia watu wanaendelea kugundua mbinu mbalimbali ili waweze kuwafurahisha wapenzi wao wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Zijue Athari za kuweka vitu ukeni .
1.wanawake walio wengi wanaweka vitu ukeni kama vile vipipi, mawe, vikokoto, sukari na madawa mengine mengi wakiwa na malengo tofauti wengine wanaweka vitu mbalimbali ili kuweza kuwafurahisha wapenzi wao wakati wa kufanya tendo la ndoa na wengine wanaweka ili kuweza kuongeza uchungu wakati wa kujifungua, pamoja na hayo kuna madhara makubwa kama ifuatavyo.
2.Vitu hivyo uharibu kabisa hali ya uke kwa kupunguza pH ambayo iko kwenye uke kwa sababu pH ya kwenye uke ina kiwango chake ambacho ni kati ya 3.8 hadi 4.5 ukiweka vitu kama hivyo unaweza kuipunguza au kuiongeza kwa hiyo na kusababisha kuingia kwa wadudu kwa sababu kazi ya pH ni kuweka uke kwenye hali maalum ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali kwa hiyo matumizi ya vitu hivyo uharibifu kabisa hali ya uke.
3. Matumizi ya vitu ukeni ni chanzo cha kuwepo kwa magonjwa mbalimbali, kwa sababu vitu vingine vinatolewa kwenye mazingira ya uchafu na maandalizi ya vitu hivyo pengine ni ya kimila mno hali ambayo Usababisha kuwepo kwa Magonjwa kwenye sehemu ya uke, magonjwa mengine ni kama fungusi za ukeni, Maambukizi kwenye mlango wa kizazi, Maambukizi kwenye mfuko wa kizazi na pengine mtu anaweza kupata ugumba kwa sababu ya vitu hivyo na hata kansa mbalimbali zinaweza kujitokeza.
4. Madhara wakati wa kujifungua.
Kwa wakati mwingine wanawake wanaweka vitu hivyo na wanafikia wakati wa kujifungua bado vipo na kwa wengine wanadhubutu kuwaamini wale waliowaweka vitu hivyo ndo wawasaidie wakati wa kujifungua hali ambayo mtoto anakuja vibaya na unakuta maarifa wanayo kidogo hali hii Usababisha vifo kwa akina Mama na watoto wao kwa sababu ya matumizi ya vitu visivyoeleweka na kuweza kujiamini.
5. Kuchanika na kupasuka wakati wa kujifungua.
Kwa sababu ya matumizi ya vitu hivyo ukeni kuna vingine kweli vinaongeza uchungu, kwa hiyo kuna kipindi akina Mama wanakuwa na uchungu kabla ya mda kwa sababu ya matumizi ya vitu hivyo na wakija hospitalini wanasukuna mtoto kabla njia haijafunguka vizuri kwa sababu ya kuongeza uchungu kwa hiyo wanaposukuma wanapasuka na kutokwa na damu nyingi na kama alijifungulia kwenye sehemu ambayo haina vifaa vya kutosha wanaweza kupata matatizo na hata kupoteza maisha wao na watoto wao.
6.Kwa hiyo akina Mama vitu hivyo havina maana yoyote kabisa kwa wale wanaovitumia kwa lengo la kufanya tendo la ndoa lipendeze jua kuwa kuna hatari ya kupata magonjwa na pia kabla ya tendo la ndoa mjiandae vizuri ili kuweza kufanya tendo la ndoa juwa tamu sio kutumia vitu hivi vya ajabu na kumbuka wewe Mama ukipata matatizo ni wewe kwa mwanaume ni kiasi kidogo kwa hiyo akina Mama jali afya zenu na maisha yenu ni ya muhimu sana.
7.Na kwa wale wanaotumia vitu hivi ili kuongeza uchungu na kujifungua mapema sio kweli kwa sababu uchungu ukija ukiwa hospitalini watakusaidia wakunga kwa sababu wenyewe wanajua mda gani utajifungua na kwa wakati kwa hiyo acha kuharakisha mambo acheni short cut kwa sababu kwa kutumia vitu hivi ni kuhatarisha maisha yako na mtoto wako.
8.Pia jamii inapaswa kutoa elimu kwa jamii kwa ajili ya kuepukana na mila na desturi ambazo zinahatarishwa maisha ya watu na wanawake wanapaswa kuhudhuria kliniki ili kuweza kupata maelekezo muhimu kwa sababu huko kila kitu kinafundishwa huko, asilimia kubwa ya wanawake wanaokwenda kliniki mda umeenda ndio wanafanya vitu vya hivyo kwa hiyo mama maisha ni ya kwako tunapaswa kuungana kwa pamoja ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Jifunze sababu kuu zinazosababisha kuhisi maumivu makali ya tumbo wakati wa kushiriki tendo la ndoa
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja, aina hiyo ya mimba kwa kitaalamu huitwa complete abortion.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo ni moja katika dalili za ujauzito. Maumivu wanawake wengi hushindwa kujuwa kuwa ni ujauzito ama laa. Na hii ni kwa sababu kwa wanawake wengi maumivu ya tumbo ama changu ni jalivya kawaida kwao.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali yanayodhoofisha afya za wanaume, kwa wakati mwingine wanaume ukosa kujiamini kwa sababu ya mambo ambayo yanaadhiri afya za wanaume.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia Faida za Uzazi wa mpango kwa watoto, mama, wanandoa, na jamii au JUMUIYA.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zilijitokeza zinaweza kusababisha ugumba hasa kwa wanawake, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa makini kwa Dalili hizi hasa kwa wadada, kama kuna uwezekano wa matibabu tibu mapema ili kuepuka tatizo la kuwa mgumba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza uke, tunajua wazi kuna magonjwa mbalimbali yanayoweza kutokea iwapo uke hautaweza kutunzwa vizuri na pia uke ukitunzwa vizuri kuna faida ya kuepuka maradhi ya wanawake kwa njia ya kutunza uke.
Soma Zaidi...Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...