Vyakula hivi hapasi kuvila mwanamke mwenye ujauzito kwa kiasi kikubwa, hasa yule mwenye mimba chaga
VYAKULA HATARI KWA MJAMZITO HASA KWA MIMBA CHANGA
1.Mayai mabichi: Mayai ni chakula kizuri kila mtu anatambuwa hili. Hata hivyo si jambo jema kula mayai mabichi. Hii inaweza kuwa hatari kwa ujauzito hasa kwa mwenye ujauzito mchanga. Hivyo epuka kula mayai mabichi ama yasiyowiva vyema.
2.Maini ya wanyama kwa wingi: Maini ni katika vyakula ambavyo vina virutubisho vingi sana. Kama ijulikanavyo ini lina kazi nyingi mojawapo ni kuondoa sumu mwilini. Hivyo unahitajika kutokula maini kwa mjamzito.
3.Shubiri: shubiri hufahamika kwa uchungu wake. kwa mwenye ujauzito hasa mimba changa shubiri sio salama. Shubirilinaweza kutoa ujauzito kama litatumika kwa kulinywa. Onyo hili linaandamana na miti mingine michungu.
4.Viazi mbatata vilivyoanza kuota: onyo hili ni kwa nafaka zote zinazoanza kuota sio nzuri kula. Hasa hasa viazi mbatata ambavyo vimeanza kutoa miche sio salama kwa mwanamke mjamzito kutuia kama chakula.
5.Mapapai hasahasa mapapai yasiyowiva: Matunda nimuhmu sana kwa mjamzito kwa afya yake na ya mtoto wake. Hata hivyo kuna matunda sio mazuri kuyala kwa wingi kwa mwenye mimba changa. Mapapai ni mojawapo, hasa papai ambalo halikuwiva, yaani lile la kijani lililokomaa.
6.Mananasi: nanasi ni kama papai, kama mjamzito atatumia kwa wingi, inaweza kuwa hatari kwa mimba iliyochanga.
7.Vyakula ambavyo havijawiva vyema hususani samaki na nyama: sio samaki tu na nyama, chakula chochote ambacho hakikuwiva vyema ni hatari sana kwa mwenye uauzito. Hii ni sawa na nyama ya kuku na vyakula vingine.
8.Kutumia majani ya chai yenye caffein kwa wingi. Mjamzito hakatazwi kunywa chai ya majani ya chai. Kilichokibaya ni kuzidisha unywaji wa chai yenye majani ya chai kupitiliza. Majani ya chai yana kemikali inayoitwa caffein, hii ikiwa nyingi inakuwa hatari kwa ujauzito.
9.Chumvi kwa wingi
10.Energy drink
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowTofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma kwa mtoto mwenye shida ya kupumua, mtoto kama ana shida ya kupumua tunaangalia dalili kwanza na baadaye tunaweza kutoa huduma kulingana na Dalili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuangalia kama mtoto anapumua pindi anapozaliwa,tunajua kabisa ili kujua na kuelewa kama mtoto yuko hai ni lazima kuangalia upumuaji wa mtoto,ambapo tunaitambua pale anapolia tu.
Soma Zaidi...inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mama mjamzito, kwa sababu kuna baadhi ya Dalili zikitokea kwa mama mjamzito ni vizuri kabisa kuwahi hospitali mara moja.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea ugonjwa wa kisukari wakati mama akiwa mjamzito.na yafuatayo ni Mambo hatari yanayotokea wakati Mama akiwa na ujauzito.
Soma Zaidi...Ikiwa mtoto wako ana kasoro ya moyo wa kuzaliwa, ina maana kwamba mtoto wako alizaliwa na tatizo katika muundo wa moyo wake. Baadhi ya kasoro za moyo za kuzaliwa kwa watoto ni rahisi na hazihitaji matibabu, kama vile tundu dogo kati ya chemba za moyo amb
Soma Zaidi...