Fahamu mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa
Posti hii inahusu zaidi mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa, kwa kawaida tunajua kwamba mtoto wakati wa kuzaliwa ni lazima atangulize kichwa ila Kuna kipindi mtoto anatanguliza matako, kuna aina nne za mtoto kutanguliza matako.
Aina za mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa.
1. Tunaposema kwamba mtoto katanguliza matako kuna aina mbalimbali za kutanguliza matako , pengine ni matako yenyewe mtoto akiwa amejikunja aina hii kwa kitaalamu huitwa complete breech, kwa hiyo mikono ya mtoto huwa imejikunja Ila mtoto uzaliwa kawaida au hali kama sio nzuri mtoto anaweza kufanyiwa upasuaji na kutolewa kawaida tu.
2.Aina nyingine ni pale mtoto anapokuwa ametanguliza matako na mikono ikiwa imejikunja Ila ameamsha mguu mmoja juu na mguu wa pili unakuwa imejikunja chini ya mguu ulioamshwa juu,aina hii kwa kitaalamu huitwa in complete breech, kwa hiyo wauguzi na wataalamu wengine wa afya wanapaswa kufahamu Ili kuweza kuwasaidia wakina mama waweze kujifungua salama.
3. Kuna aina nyingine ni pale Mtoto anakuwa ametanguliza matako lakini miguu yake yote imeinuliwa juu na mikono alkiwa amejikumbatia kifuani aina hii kwa kitaalamu huitwa frank breech,kwa hiyo mtoto akijitokeza namna hii anapaswa kuangaliwa vizuri Ili kuepukana kuleta matatizo wakati wa kujifungua.
4. Kwa hiyo baada ya kuona na kujua aina za mtoto aliyetanguliza matako tunapaswa kuelewa kuwa na Hawa ni watoto wa kawaida, Kuna jamii ambazo uona kuwa ni watoto wa kipekee katika familia na kwa wakati mwingine upatiwa majina ya mapacha wakimanisha kuwa ni mapacha kuna jamii nyingine wanapona labda ni mkosi na kuanza kutambikia wakiwa na maana kwamba waondoe mkosi au tukio baya linaloashiliwa na mtoto kutanguliza matako.
5. Kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwenye jamii Ili kuweza kuondoa hizi Imani potofu na kufahamu kuwa huyu ni mtoto wa kawaida kama watoto wengine na pia kitenge cha mtoto kutanguliza matako ni kawaida utokea hasa kwa wanawake waliojofungua mara nyingi kwa hiyo uwanja huwa ni mkubwa na mtoto uweza kujigeuza jinsi anavyopenda akiwa tumboni, pia Mama akigunduliwa mapema kuwa mtoto katanguliza matako ni vizuri kujitahidi kujifungulia hospital Ili kupata huduma nzuri
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 ai web app 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki, kliniki nisehemu ambayo mtoto hupelekwa Ili kujua maendeleo ya mtoto akiwa chini ya umri wa miaka mitano
Soma Zaidi...Faida za kula yai lililopikwa kwa mama mjamzito
Yai lililopikwa ni chanzo kizuri cha protini, vitamini, na madini muhimu kwa mama mjamzito. Husaidia katika ukuaji wa mtoto tumboni, afya ya mama, na kuimarisha kinga ya mwili.
Soma Zaidi...Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa
Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Soma Zaidi...Dalili za mimba changa
Zijuwe dalili 17 za mimba na mimba changa, kuanzia siku ya kwanza mpaka mwezi mmoja
Soma Zaidi...Sababu za kupasuka kwa mfuko wa kizazi
Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.
Soma Zaidi...Zijuwe Dalili za minyoo na dalili kuu 9 za minyoo
Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini
Soma Zaidi...