image

Utaijuwaje kama swala yako imekubalika

Hapa tunakwenda kuona jinsi ya kuzitathmini swala zetu.

Tathmini ya Swala Zetu

Tumeshafahamu lengo la swala na na nna linavyopatikana. Lakini ukiichunguza jamii ya Waislamu wanao swab leo, huoni lengo hill liki#lkiwa. Kwa maana nyingine Waislamu wengi tunaoswali swala tano kwa kila siku, mwenendo na tabia zetu katika maisha ya kila siku hazitofautiani na we wasioswali.

 


pamaja na kuswali kwetu tunapoteza wakati wetu katika mambo ya. upuuzl. tunasema uwongo, tunasengenya, tunafitinisha watu, tunawadharau wengine, tunavunja ahadi tulizoweka, tunahini amana za watu, tunadhulumu kaki za watu, tunachuma katika njia za haramu, tunawatii viangozi wetu kinyume na zmxi za Allah{s.w), tunafuata njia

 

nyingine za maisha kinyume na ile aliyoiridhia Allah (s.w), tunawatumikia wengine na kuwategemea kinyume na Allah (s.w) na tunatenda mengine mengi kinyume na ridhaa ya Allah (s.w).
Je, kama mwenendo wetu ndio huu katika kuendesha maisha yetu ya kila siku tunatofauti gani na wale wasio swali na tunajitofautishaje na makafiri na washirikina kiutendaji? Kama tabia na mwendo wetu katika kuendesha maisha yetu ya kila siku ni sawa na ule wa makafiri na washirikina tutasalimikaje na adhabu kali ya Allah (s.w) aliyowaandalia makafiri na washirikina? Je swala zetu hizi zisizotunufaisha kama ilivyo matarajio na zisizotufikisha kwenye lengo lililokusudiwa haiwi ni mzigo kwetu na usumbufu mtupu? Bila shaka, kwa kujiuliza maswali haya, wengi tunaoswali kwa nia njema kabisa, tutaona kuna haja kubwa ya kupata jibu sahihi la swali lifuatalo:
“Kwa nini swala zetu hazituzalii matunda yanayotarajiwa na kutufikisha katika lengo tarajiwa? Japo kila mmoja anaweza kujibu swali hili kwa jinsi anavyoona, mchango wetu katika kujibu swali hili ni kwamba wengi wanaoswali wana mapungufu yafuatayo:

 


1. Kutojua Lengo la Kusimamisha Swala

 


Kutojua lengo halisi la swala au kuipa swala lengo lingine lisilokuwa lile aliloliainisha Allah (s.w), ni sababu tosha ya kufanya mwenye kuswali asifikie lengo la swala na kukosa manufaa yanayoambatana nalo. Lengo la swala kama lilivyobainishwa katika Qur-an ni:

 

“... Hakika swala humzuia mtu na maovu na mambo machafu...” (29:45)

 

Kwa maana nyingine lengo la swala ni kumfanya Muislamu awe na mwenendo mzuri anaouridhia Allah (s.w) katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Utendaji wowote, shughuli yoyote au tabia yoyote mtu atakayokuwa nayo kinyume na ridhaa ya Allah (s.w) itakuwa ni miongoni mwa maovu na mambo machafu. Wengi wetu wameelewa kuwa lengo la swala ni kupata Thawabu (ujira mwema kutoka kwa Allah). Ni kweli kabisa kuwa Allah (s.w) ameahidi kuwazawadia wale wote watakaoishi hapa ulimwenguni kulingana na ridhaa yake, lakini zawadi hii sio lengo bali ni matunda yanayopatikana baada ya lengo kufikiwa. Hali kadhalika lengo la swala si kupata thawabu bali ni kumwepusha mwenye kuswali na yale yote yenye kumuudhi Allah (s.w) na kumpa msukumo wa kuyafanya yale yote yenye kumridhisha Allah (s.w) ili kupata radhi yake na kustahiki kupata ujira mwema (Thawabu) aliowaahidi waja wema.

 


Hatari ya kuchukulia kuwa kupata “Thawabu” ndio lengo la swala, ni kwamba mtu anaweza kuridhika na swala zake kuwa zimempatia “Thawabu” na akawa na tumaini la kupata “Pepo” na huku amezama katika maovu na mambo machafu katika kuendesha maisha yake ya kila siku.
2.Kutohifadhi Swala
Swala haitoi matunda yanayotarajiwa na kufikia lengo lililotarajiwa mpaka ihifadhiwe. “Wamefuzu Waislamu ambao swala zao huzihifadhi” (23:1, 8). Kuhifadhi swala ni kuzingatia na kuyatekeleza kwa ukamilifu masharti ya swala, na kutekeleza kwa ukamilifu nguzo zake.
Wengi tunaoswali hatutekelezi ipasavyo masharti na nguzo za swala ama kwa kutojua au kwa kupuuza. Ni makosa makubwa mno kufanya ibada bila ya kuwa na elimu yake. Miongoni mwa watu wanaochukiza mbele ya Allah (s.w) ni mtu kufanya ibada yoyote ile kwa ujinga.Swala yoyote iliyoswaliwa pasina kutimiza na kukamilisha masharti na nguzo zake haimfikishi mwenye kuswali katika lengo la swala bali humzidishia uovu na kumfanya astahiki kupata ghadhabu za Allah (s.w) na adhabu kali:

 

“Basi adhabu kali itawathubutikia wanao swali, ambao wanapuuza swala zao”.
Hivyo, ili tupate matunda ya swala zetu na tufikie lengo lililotarajiwa hatuna budi kuyafahamu vyema masharti ya swala na kuyatekeleza kwa ukamilifu na hatuna budi vile vile kuzijua nguzo za swala na kuzitekeleza kwa ukamilifu.

 


3.Kutokuwa na khushui katika Swala

 


Unyenyekevu(khushui) ndio roho ya swala. Swala iliyoswaliwa pasina unyenyekevu huwa si swala bali maiti ya swala. Ni dhahiri kwamba kama swala ya mtu itakuwa maiti, haitakuwa na uwezo wowote wa kumfikisha mwenye kuswali kwenye lengo lililotarajiwa.

 


Unyenyekevu katika swala hupatikana kwa kuwa na utulivu wa mwili na mawazo na kuwa na mazingatio ya Allah (s.w). Mazingatio ya Allah katika swala ndio nguvu pekee inayompelekea mja kufikia lengo la swala:

 


“... Kw a yakini kumbuko la Mw enyezi Mungu (lililomo ndani ya sw ala) ni jambo kubwa kabisa (la kumzuia mja na maovu na mambo machafu)...”. (29:45)
Ni swala ile tu iliyoswaliwa kwa unyenyekevu ndio inayoweza kumfikisha mwenye kuswali kwenye lengo la swala na kumfanya afaulu na kustahiki ujira mkubwa na pepo ya Firdaus kutoka kwa Allah (s.w):

 

Hakika wamefuzu Waislamu ambao huwa wanyenyekevu katika swala zao... Hao ndio warithi ambao watarithi Pepo wakae humo milele”. (23:1-2, 10-11)
Wengi tunaoswali hatuswali kwa unyenyekevu. Mara nyingi tunaswali huku mawazo yetu yamehama kwenye swala na yanajishughulisha na mambo mengine kabisa nje ya swala. Mara nyingi ndani ya swala ndimo tunamokumbuka mambo yetu mengi tuliyoyasahau .Hii yote huonyesha udhaifu tulionao katika kumzingatia Allah (s.w) katika swala zetu. Miongoni mwa sababu kubwa zinazotufanya tukose mazingatio katika swala zetu ni kutojua maana na undani wa yale tuyasemayo katika swala. Wengi wetu hatujui maana ya aya za Qur-an tunazozisoma, dhikri na tasbihi mbali mbali tunazozileta, maamkizi na dua mbali mbali tunazoziomba katika swala. Hali hii ya kutojua maana ya yale tuyasemayo katika swala inachangia kwa kiwango kikubwa kutupunguzia uwezo wa kumuelekea na kumnyenyekea Allah (s.w). Wengine tunajua maana ya yale tuyasemayo katika swala lakini hatuyazingatii bali tunayatamka kikasuku tu sawa na wale wasiofahamu maana yake.

 


Bila shaka tukisimamisha swala kwa kujua vyema lengo lake na kwa nia ya kulifikia lengo hilo, tukajitahidi kuliendea lengo hilo kwa kutekeleza kwa ujuzi na kwa ukamilifu masharti yote na nguzo zote za swala, tukajitahidi kuyafahamu yale yote tuyasemayo katika kila hatua ya swala, na tukajitahidi kuyazingatia na kisha tukajitahidi kutuliza miili yetu na nyoyo zetu katika swala, tutalifikia lengo la swala na kupata matunda yatokanayo - Insha-a Allah(s.w)

 

Mola wangu! Nijaalie niwe msimamishaji swala na kizazi changu. Mola wetu na upokee maombi yangu mengine.

            

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/15/Monday - 10:42:25 am Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 735


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Utaratibu wa kutekeleza hija, matendo hatua kwa hatua, pamoja na kusherehekea sikuku baada ya hija
4. Soma Zaidi...

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu
Soma Zaidi...

Ni upibutaratibu wa kuingia eda na kutoka eda
Katika uislamu hakuna sheria ya mwanamke kuingizwa eda na kutolewa eda kama ilivyozoeleka. Endelea na post hii ujifunze zaidi Soma Zaidi...

Namna ya kuosha maiti hatua kwa hatua
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Zaka ni nini? Nini maana ya zaka katika uislamu
Zaka, kilugha ni kukua; kubariki na kuzidi kheri. Soma Zaidi...

Nguzo za kufunga ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuwapa wanaostahiki
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mambo yanayoweza kutoa udhu wako
Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu. Soma Zaidi...

darasa la funga
Soma Zaidi...

Sunnah za udhu
Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu sunah za udhu Soma Zaidi...