Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Kwa mujibu wa Qur’an (9:60) na (2:273), wanaostahiki kupewa Zakat ni waislamu tu katika makundi yafuatayo;
- Ni kundi la wale wasiojiweza kwa chochote cha kumudu maisha yao kabisa ya kila siku bila kusaidiwa.
- Ni wale wasio na uwezo wa kupata mahitaji yao ya msingi ya kimaisha ila wana uwezo wa kujikimu kwa kiasi fulani tu.
- Ni wale wote wanaozikusanya na kuzigawanya kwa wanaohusika bila kujali uwezo wao.
- Ni wale walioingia katika Uislamu karibuni na wanahitajika kuimarishwa imani zao juu ya Uislamu.
- Ni kuwakomboa au kuwanunua watumwa au watu wote wanaoishi chini ya miliki ya watu (mabwana) na kuwaachia huru.
- Ni kuwalipia waislamu madeni yao waliokopa ili kujikimu kimaisha lakini bila kukusudia wameshindwa kulipa deni zao.
- Ni kutumika katika shughuli zote zinazopelekea kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.
- Msafiri yeyote muislamu aliyeharibikiwa kwa kupoteza, kuibiwa au kuishiwa mali yake hata kama ni tajiri, ni wajibu kupewa zakat.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Yajuwe mambo ambayo yanapendeza kuyafanya wakati ukiwa umefunga Ramadhani.
Soma Zaidi...Talaka zimegawanyika katika makundi mengi. Katika somo hili utakwenda kukifunza aina kuu za talaka katika uislamu.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Wajibu wa KufanyakaziUislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada.
Soma Zaidi...