Maana ya shahada kama nguzo ya kwanza ya uislamu
4.
Maana ya shahada kama nguzo ya kwanza ya uislamu
4.1 Shahada.
Tafsiri na Maana ya Shahada.
- Shahada ya kwanza.
“Nashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah”
Sifa (tabia) za mtu aliyetoa Shahada ya Kwanza Kiutendaji:
-Hatamtii yeyote katika maisha yake ya kila siku ila Allah peke yake.
-Hatamuogopa, hatamtegemea na hatamuomba yeyote ila Allah.
-Hatafuata mwongozo wowote ila ule wa Allah pekee.
-Hatamshirikisha Allah (s.w) kwa chochote kile.
-Atajipamba na sifa na tabia njema zilizoainishwa katika Qur’an na Sunnah.
- Shahada ya Pili.
“Nashuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Allah”
Sifa (tabia) za mtu aliyetoa shahada ya Pili Kiutendaji:
- Kumtii Mtume (s.a.w) kwa kufuata aliyoagiza na kuacha aliyokataza.
- Kumuiga Mtume (s.a.w) katika mwenendo na tabia yake.
- Kumfanya Mtume (s.a.w) kuwa hakimu wa mambo yetu yote.
- Kuliendea lengo la kuletwa kwake la kuusimamisha Uislamu katika
jamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 ai web app 👉5 web hosting 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Swala ya Istikhara na jinsi ya kuiswali
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara
Soma Zaidi...Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah.
Soma Zaidi...Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa
Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.
Soma Zaidi...Milki ya raslimali katika uislamu
Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.
Soma Zaidi...