WANAOSTAHILI KUPEWA ZAKA
“Sadaqat hupewa (watu hawa): Mafakiri, Maskini, wanaozitumikia (wanaozikusanya na kuzigaw anya) na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya
Uislamu),na katika kuwakom boa watumwa,na katika kuwasaidia wenye madeni, na katika njia ya Allah (s.w) na katika kuwapa wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima” (9:60).
Japo aya hii imeanza na neno Swadaqat, mgawanyo ulioelezwa hapo umekusudiwa mgawanyo wa Zakat kutokana na msisitizo uliopo mwishoni mwa aya hii: “Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu”. Tunafahamu kuwa Zakat ni faradh na Swadaqat ni wajibu au sunna iliyokokotezwa. Kama ilivyo katika aya hii Zakat inastahiki igawanywe katika mafungu manane yafuatayo:
(a)Fukara
Fukara ni kundi la wale wasiojiweza kabisa kumudu maisha yao bila ya msaada kutoka kwa wenziwao katika jamii. Hawa hupangiwa fungu la Zakat ili kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji ya maisha yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na chakula, mavazi, makazi na mahitajio mengine muhimu ya Mwanaadamu. Ni lazima Waislamu waunde utaratibu mzuri wa ugawaji wa Zakat ili pasiwe na yeyote katika hawa wasiojiweza kabisa anayekosa baadhi ya mahitajio muhimu ya maisha.
Ufukara unaotokana na maumbile au uzee ni wa kudumu au wa muda mrefu, lakini kuna fukara wengine wa muda mfupi ambao pia katika hali hiyo ya ufukara wanahitaji kusaidiwa kutokana na fungu la Zakat. Hawa ni pamoja na watu waliopatwa na ajali kama vile kuunguliwa nyumba na vyote vilivyokuwemo. Kwa ujumla Muislamu anapokabiliwa na matatizo ya wazi yaliyomtokea nje ya uwezo wake na akawa hana uwezo wa kupata kabisa mahitaji muhimu ya maisha yake na wale anaowaangalia, asaidiwe kwa fungu la Zakat mpaka hapo atakapopata tena uwezo wa kuyamudu maisha.
(b)Masikini
Kutokana na maelekezo ya Qur’an na Hadith, maskini ni wale ambao ukiwaangalia haraka haraka katika hali zao za nje bila ya kuwaangalia kwa undani, utawadhania kuwa wanao uwezo wa kujipatia mahitaji muhimu ya maisha kwa vile hawana kilema chochote kinachoonekana kwa nje na hawaombi (kama ni Waislamu kweli kweli). Lakini ukweli ni kwamba maskini hana uwezo wa kujitosheleza kwa mahitaji yake yote muhimu ya maisha bali ana uwezo wa kupata baadhi yake tu. Kwa mfano kama mahitaji yake muhimu ya maisha ni shilingi 1,000/= kwa siku,yeye ana uwezo wa kupata shilingi 400/= tu na inabidi aishi kwa dhiki bila ya shilingi 600/ = zilizobakia. Katika Qur’an tunafahamishwa:
(Wapewe hizo Sadaqat) Mafakiri waliozuiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, wasioweza kwenda huko na huko katika ardhi (kufanya kazi ya kutafuta riziki); asiyewajua ha li zao anawadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao (na kuomba). Utawafahamu (kuwa wahitaji)
kwa alama zao (zinazooyesha ufakiri, lakini) hawawaombi watu wakafanya ung’ang’anizi. Na mali yoyote mnayoyatoa, basi kwa yakini Mw enyezi Mungu anayajua (atakulipeni) (2:2 73).
Hivyo, kwa kuwa maskini si rahisi sana kumuona kwa kuwa hana alama ya nje kama fukara na wala hajitambulishi kwa kuomba, Waislamu wanatakiwa kujuana kwa hali zao na kila mmoja kuwa macho juu ya dhiki na huzuni za wengine ili kutoa msaada kila utakapohitajika. Kwani maskini hutambuliwa (hung’amuliwa) na wale wenye huruma na wanaojishughulisha na dhiki za Waislamu na wanaadamu wenziwao. Tumeamrishwa kuwasaidia wenzetu hawa ile asilimia sitini (60%) ya mahitajio yao muhimu ya maisha iliyobakia kwa kuwapa Zakat na Sadaqat.
(c)Wanaozitumikia (Al-A’miliina A’laiha):
Wale wote watakaoshughulika katika ukusanyaji na ugawanyaji wa Zakat, ujira wao hutokana na hiyo hiyo Zakat. Kuwekwa fungu hili la Zakat ni ushahidi kuwa Zakat si ibada ya mtu binafsi au ibada ya matajiri tu bali ni ibada inayotakiwa itekelezwe na jamii yote kwa ujumla. Ni lazima jamii ya Waislamu iunde utaratibu wa ukusanyaji na ugawaji wa Zakat kama ilivyokuwa wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w) na Makhalifa wake waongofu.
(d)Wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu
Wanaohitaji kutiwa nguvu nyoyo zao ni wale Waislamu walioingia katika Uislamu katika siku za karibuni na kwa kiasi ambacho nyoyo zao hazijawa madhubuti katika Uislamu na huweza kuyumba wakati wowote wa dhiki. Haki ya kuwapa hawa Zakat iko wazi. Wakati mwingine kwa kuchukua uamuzi wa kuacha dini ya zamani na kujiunga na Uislamu huweza kumletea mtu matatizo ya kukosana na ndugu zake, marafiki zake na hata kukosa mali yake, matukio ambayo yatamuathiri sana katika maisha yake mapya. Kwa sababu hii Waislamu wanalazimika kumkaribisha mwenzao kwa kumtengea fungu maalum la Zakat na Sadaqat ili kumuonyesha udugu wa kweli wa Kiislamu na kumthibitishia moyoni mwake kuwa Uislamu ndio dini pekee inayomstahiki mwanaadamu. Tunao mfano mzuri kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w). Katika vita vya Hunain Mtume (s.a.w) alitoa sehemu kubwa ya ngawira (vitu vilivyotekwa vitani) kuwapa maswahaba waliosilimu katika siku za karibuni. Ansar walipolalamika juu ya jambo hili, Mtume (s.a.w) alisema: “Watu hawa wameingia katika Uislamu sasa hivi baada ya kuacha kufru. Nataka nifariji mioyo yao”.
Pia fungu hili linaweza kutumika katika kuwanunua maadui wa Waislamu ili wafute wazo la kupigana na Waislamu au katika kuwapa watu wanaoweza kuwashawishi maadui wa Waislamu wasipigane na Waislamu. Kitu muhimu mbele ya Uislamu na Waislamu ni amani, hivyo amani haina budi kutafutwa hata ikibidi kuinunua kwa namna hii kwa fungu la Zakat. Makhalifa wa Mtume walifanya hivi.
(e) Kuwakomboa watumwa (Fir-riqaabu)
Wakati Mtume (s.a.w) anahuisha Uislamu Uarabuni na duniani kote palikuwa na mtindo wa kijahili na ukandamizaji wa matajiri, watawala na wengine wenye uwezo wa kuwachukua watumwa kwa kuwanunua au kwa nguvu na kuwafanya watumwa wa kuwatumikia katika maisha yao yote bila ya malipo yoyote na bila ya uhuru. Uislamu unatufundisha kuwa wanaadamu wote wamezaliwa huru na hawapaswi kujidhalilisha kwa yeyote au kuutoa uhuru wao kwa yeyote asiyekuwa Allah (s.w), Aliye Bwana wao pekee . Hivyo Uislamu unalaani utumwa wa aina zote. Kufuatana na Hadithi ya Mtume (s.a.w), anayemfanya mwenziwe mtumwa, hata kama akijiita Muislamu mahali pake pa marejeo ni motoni. Mtume (s.a.w) ametoa onyo kali katika Hadithi ifuatayo:
Kuna watu wa aina tatu ambao mimi mwenyewe nitasimama kuwashitaki katika siku ya Hukumu; miongoni mwa hao ni yule anayemchukua mtu huru na kumfanya mtumwa na kumuuza... (Bukhari, Ibn Majah).
Uislamu pamoja na kuukemea utumwa kiasi hicho, umewaamrisha Waislamu wawakomboe Waislamu wengine walio utumwani kwa kutoa kikomboleo kinachohitajika kutokana na Zakat na Sadaqat. Pia katika kundi hili ni pamoja na wafungwa wa kivita waliotekwa katika kupigania haki. Hawa nao watakombolewa kwa fungu hili la Zakat.
(f)Kuwasaidia wadaiwa kulipa madeni yao
Deni ni jambo linalochukuliwa kwa uzito mkubwa katika Uislamu. Inatakiwa Muislamu aingie katika deni inapokuwa hapana budi, na kamwe asithubutu kukopa wakati anao uwezo wa kuvumilia kuishi na hali ya upungufu wa mahitaji muhimu inayomkabili. Kukopa kwa ajili ya kutosheleza matamanio yasiyo ya muhimu katika maisha kumekatazwa. Dhambi kubwa inayofuatia madhambi makubwa ni kufa na deni kama tunavyofahamishwa katika hadithi ifuatayo:
Abu Musa ameeleza kutoka kwa Mtume (s.a.w) aliyesema: Hakika katika madhambi makubwa mtu atakayokwenda nayo mbele ya Allah baada ya madhambi makubwa Allah aliyoyakataza ni mtu kufa na deni na ikawa hakuacha kitu cha kulipia deni hilo. (Ahmad, Abu Daud).
Miongoni mwa dua za Mtume (s.a.w) ilikuwa hii ya kumuomba Allah (s.w) amkinge na madeni. Alikuwa akiomba:
Ee Allah, Najikinga kwako kutokana na mtamanio (hamu na huzuni) kutokana na uzembe (ajizi na uvivu) kutokana na moyo mnyonge na ubakhili, kutokana na mzigo wa deni na kunyongeshwa na watu. (Bukhari na Muslim).
Deni ni lazima lilipwe, ama hapa duniani au mbele ya Allah katika siku ya Hukumu. Kama mtu alikopa kwa shida ya wazi iliyomkabili na akashindwa kulipa katika wakati waliokubaliana na mdai, basi Waislamu wamsaidie kulipa deni hilo kwa fungu la Zakat na Sadaqat. Iwapo Waislamu hawatamlipia na akafa na deni hilo, basi Allah (s.w) atamlipia mwenyewe siku ya malipo.
(g)Katika njia ya Allah (Fii-Sabilillah)
“Katika njia ya Allah” ni maneno yanayotumika kwa maana ya shughuli zote zinazofanywa kwa ajili ya kuhuisha Dini ya Allah na kusimamisha Ufalme wake hapa ulimwenguni. Kwa maana nyingine juhudi yoyote inayofanywa ili kuuwezesha Uislamu kusimama kama unavyostahiki inaingia katika uwanja huu wa “Fii Sabilillah ”. Kwa hiyo aina zote za jihadi katika Uislamu - jihadi ya ulimi, jihadi ya kalamu na jihadi ya kitali (vita) zimo katika huu uwanja wa “Fii Sabilillah ” na hasa fungu la Zakat limetengwa ili kuziendeleza kwa ufanisi jihadi hizi. Mtume (s.a.w) amesema kuwa hairuhusiwi kumpa Zakat mtu aliye tajiri lakini kama tajiri atataka msaada kwa ajili ya jihadi ni lazima apewe Zakat, kwani mtu mmoja hata akiwa tajiri inawezekana asiweze kutoa gharama zote zinazohitajika katika maandalizi ya jihadi. Tukumbuke kuwa kulingania na kupigania dini ya Allah si kazi ya watu maalum bali ni amri kwa kila Muislamu. Hivyo ikitokea Waislamu wako katika harakati za kusimamisha dini ya Allah au katika vita vya kuihami, wale wasioweza kujigharimia wenyewe katika harakati na mapambano hayo, wasaidiwe kwa mfuko wa Zakat.
(h)Kuwasaidia wasafiri walioharibikiwa njiani (Ibnis Sabiil)
Msafiri aliyeharibikiwa njiani kwa kuibiwa, kupoteza mali yake, kupata ajali, kuishiwa na masurufu, (matumizi) n.k. Akawa hana uwezo wowote wa kupata mahitaji muhimu ya maisha, hata kama ni tajiri huko alikotoka,inabidi apewe fungu la Zakat ili aweze kuyamudu maisha mpaka afike mwisho wa safari yake. Fungu hili pamoja na mafungu mengine yote ya Zakat au mgawanyo wa Zakat kwa ujumla unatupa picha kamili juu ya udugu wa Kiislamu.
Wanaostahiki kupewa Sadaqat
Pamoja na Waislamu matajiri kuamrishwa watoe Zakat ili iweze kuinawirisha jamii kwa kufuata utaratibu huu, pia Sadaqat imewajibishwa kwa matajiri ili pamoja na kuwasaidia Waislamu katika mahitajio haya na mengine yasiyotajwa hapa, wawasaidie pia wanaadamu wenzi wao wasiokuwa Waislamu. Kama tulivyoona hapo awali tofauti iliyopo kati ya Zakat na Sadaqat ni kwamba Zakat hugawanywa katika mafungu haya manane yaliyotajwa hapo juu kwa Waislamu tu, ambapo Sadaqat hugawanywa kwa hata wasiokuwa Waislamu maadam wako katika dhiki inayohitaji msaada. Hebu pia tuzingatie aya zifuatazo juu ya watu wengine wanaostahiki kupewa Sadaqat pamoja na hao waliotajwa katika aya ya (9:60):
Na umpe jamaa (yako) haki yake, na maskini na msafiri aliyeharibikiwa, wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu (17:26).
Sio wema (tu huo peke yake) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi (katika kusali. Yako na mema mengine). Bali wema (hasa) ni (wa wale) wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na wanawapa mali juu ya kuwa wanayapenda - jamaa na mayatima na maskini na wasafiri (w alioharibikiwa) na waw aombao na katika (kuw akomboa) w atumw a (2:1 77).
Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsani wazazi wawili, na jamaa na mayatima na maskini na jirani walio karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa walio ubavuni (mwenu) na msafiri aliyeharibikiwa, na wale iliyomiliki mikono yenu ya kulia (kuume). Bila shaka Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wajivunao”. (4:36).
Na katika mali zao ilikuwako haki ya kupewa maskini aombaye na ajizuiaye kuomba. (51:19).
Tunajifunza kutokana na aya hizi kwamba mgawanyo wa Sadaqat ni kama ule ule za Zakat bali pamewekwa fungu la nyongeza la kuwapa jamaa haki yao. Linalosisitizwa na Uislamu ni kwamba kila mwenye uwezo lazima awaangalie jamaa zake kwanza wa karibu na mbali. Wala si Uislamu kuweka akiba kwa kipindi cha mwaka mzima huku jamaa zako wa karibu na hata wa mbali wamo katika dhiki na wanaishi bila ya kujitosheleza kwa mahitajio yao muhimu ya maisha.
Muislamu wa kweli kama ilivyoelezwa katika aya (2:177) ni yule anayetoa mali yake kwa moyo mkunjufu kuwapa jamaa zake wanaohitaji msaada, mayatima, maskini, wasafiri walioharibikiwa na wengineo wenye shida waombao na wasioomba. Baada ya kufanya hivyo kwa kipindi cha mwaka mzima, akiba ya mali iliyobaki ndiyo itakayohisabiwa na kutolewa Zakat na kugawanywa katika mafungu yaliyotajwa katika Qur’an (9:60). Kwa kufuata utaratibu huu wa kutoa Sadaqat kila inapohitajika na kuwapa wanaostahiki kupewa, utakuta kuwa kila mtu anao uwezo wa kutoa Sadaqat. Ni katika msingi huu Mtume (s.a.w) am e s em a: Kuna Sadaqat kwa kila Muislamu. Wakauliza: Kama hatapata cha kutoa je? Akajibu: Na afanye kazi kwa mikono yake miwili, kwa kufanya hivyo atakuwa amejinufaisha mwenyewe na pia kitendo hicho ni Sadaqat. Wakauliza: Kama hawezi kufanya hivyo je? Alijibu: Basi na amsaidie (kihali) mhitaji na aliyedhikika. Wakauliza: Kama hakuweza kufanya hivyo je? Alijibu: Basi hana budi kuamrisha mema. Wakauliza: Kama haw ezi kufanya hivyo je? Alijibu: Hana budi kujizuilia na maovu kwani hii hasa ni Sadaqat kw ake. (Bukhari na Muslim).
Hivyo kila Muislamu wa kweli anatakiwa apanie kutoa misaada ya hali na mali kwa jamaa na kila anayehitajia awe Muislamu au asiwe Muislamu. Kama Muislamu hana chochote cha kutoa basi aongee nao kwa wema na aonyeshe kuwa pamoja nao katika dhiki hiyo. Kufanya hivi huhesabiwa vile vile kuwa ni Sadaqat.
Katika aya hii tunafahamishwa kuwa kauli njema nayo ni Sadaqat na ni bora kuliko Sadaqat iliyotolewa kwa masimbulizi inayomdhalilisha mpokeaji na kumnyima uhuru wake. Pia si vyema kumpa mtu Sadaqat kisha umtake akurejeshee tena. Kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w) Sadaqat hairejeshwi. Si vyema mwenye kupewa akaikataa kama ni mwenye kustahiki kupewa na si vyema kwa mtoaji atake arejeshewe tena baada ya kutoa. Kwani katika Hadith tunafahamishwa:
Umar bin Khattab (r.a) ameeleza kuwa: Nilitoa farasi kwa ajili ya kupigania njia ya Allah, lakini yule aliyem chukua alimfanya akakondeana sana. Nilifikiria angeliuza kwa bei rahisi”. Kisha nilimuuliza Mtume ambaye alisema: Usimnunue na usiirejeshe Sadaqat yako (kwako baada ya kuitoa) hata kama atairudisha kwako kwa bei ya dirhamu moja, kwa sababu anayerejesha Sadaqat baada ya kuitoa ni kama mbwa anayekula matapishi yake ”. Katika simulizi nyingine Mtume alisema: “Usichukue (usiirejeshe) Sadaqat baada ya kuitoa kwa sababu yule anayeirejesha Sadaqat baada ya kuitoa ni kama yule anayekula matapishi yake”. (Bukhari na Muslim).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1162
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Kitau cha Fiqh
NI ZIPI SWALA ZA SUNNAH: (qabliya (kabliya) na baadiya, tahajudi, tarawehe, qiyamu layl, shukr, istikhara)
Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi. Soma Zaidi...
Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Soma Zaidi...
Faida na umuhimu wa ndoa katika jamii
Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi Soma Zaidi...
haki na wajibu katika jamii
Soma Zaidi...
Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa
Soma Zaidi...
Ni ipi hukumu ya kutoa talaka hali ya kuwa umelazimishwa au ukiwa umerukwa na akili
Endapo mtu atamuacha mke pasi na ridhaa yake yaani amelazimishwa ama amemuwacha wakati amerukwa na akili. Je ni ipo hukumu yake. Soma Zaidi...
Nini maana ya ndoa katia uislamu na ni upi umuhimu wake
Hapa utajifunza maana ya ndoa kulingana na uislamu na umuhimu wake katika jamiii Soma Zaidi...
Swala ya jamaa na mnamna ya kuswali swala ya jamaa, nyumbni, msikitini na kwa wanawake
Soma Zaidi...
Nadharia ya uchumi kiislamu
1. Soma Zaidi...
Jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa
Kutawadha ni katika ibada muhimu za mwanzo kutakiwa kuzijuwa na ni lazima. Swala yako haitaweza kutimia bila ya kujuwa udhu. Inakupasa kujuwa nguzo za udhu, yanayoharibu udhu na namna ya kutawadha kifasaha. Hapa utajifunza hatuwa za kutawadha Soma Zaidi...
Zijuwe Suna zinazofungamana na swaumu na funga ya ramadhani
Soma Zaidi...
haya ndiyo mambo yanayaribu swala na yanayobatilisha swala
Soma Zaidi...