image

Zijuwe nguzo tano za uislamu na maana zake katika sheria ya uislamu

Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.

NGUZO ZA UISLAMU

Nini maana ya uislamu?

Uislamu umetokana na neno silm yaani kujisalimisha ama salam kwa maana amani. Hivyo uislamu ni kujisalimisha na kunyeyekea kwa mwenyezimungu kwa kufuata maamrisho yake na kuwacha makatazo yake.

 

Dr. Zakir Naik ametafsirikwa kusema uislamu ni amani inayopatikana kwa kujisalimisha kwa mwenyezi Mungu. Hivyo kila ambaye anajisalimisha kwa mwenyezi Mungu ni muislamu.

 

Katika uislamu tunaamini kuwa Mitume wote walikuwa ni waislamu. Na Mtume  Muhammad (s.a.w) yeye ni Mtume wa Mwisho katika Mitume. Waislamu tunaamini kuwa Mtume muhammad sio Muanzilishi wa uislamu. Tunaamini kuwa uislamu ulikuwepo toka adamu hajaumwa, na amekuja duniani akiwa ni muislamu.

 

Wasomi wa mambo ya mazingira (dunia) wanaamini kuwa uislamu ulianzishwa na Mutume Muhammad mwaka 610 AD katika mji wa Maka. hii sio sahihi kwa mujibu wa mafundisho ya uislamu.

 

Uislamu una nguzo kuu tano. Ni lazima kila muisalamu azikubali nguzo hizo na azitekeleze endapo anaweza kufanya hivyo. Muislamu yeyote mwenye kukataa moja kati ya nguzo tano hizo atakuwa ametoka mwenye uislamu.

 

 

Kutoka kwa Abuu Abdir-Rahmaan Abdillaah Ibn 'Umar Ibn  Al-Khattwaab  (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema:  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akisema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake,  kusimamisha Swalaah, kutoa Zaka na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 


 

Muislamu akiwa si mwenye kuzitekeleza nguzo hizo bado ni muislamu ila atakuwa yupo kwenye makosa. Nguzo hizo ni:-

  1. Kutoa shahada
  2. Kusimmisha swala tano
  3. Kufunga mwezi wa ramadhani
  4. Kutoa zaka
  5. Kuhiji

 

Kutoa shahada:

Kutoa shahada ni kukubali kwa katika moyo wako na kutamka kwa ulumu kuwa hakuna Mungu anayepasa kuabudiwa kwa haki ila ni yeye Mwenyezi Mungu yaani Alla, na Muhammadi (S.A.W) ni mtume wake.

 

Hii ni nguzo muhimu kwa kila muislamu. Kwa ambaye sio muislamuna anataka kuwa muislamu atatakiwa kutamka maneno hayo na hapo hap atakuwa muislamu. Na kwa ambaye amezaliwa katika uisalamu yaani wazazi wake ni waislamu yeye anakuwa muislamu moja kwa moja hata bila ya kutamka.

 

Ni kwa sababu katika uislamu kila akiumbe kinazaliwa katika uislamu. Ina maani kila mtu anapozaliwa anazaliwa akiwa muislamu. Unaweza kutamka kwa kiarabu ama kwa kiswahili.

 

Kusimamisha swala

Kusimamisha swala maana yake ni kuziswali swala tano kila siku ndani ya muda wake. Muislamu asiposwali swala tano bado atabakia kuwa ni muislamu. Hata hivyo Mtume amesema “tofauti iliyopo kati ya uisalmu na dini nyingine ni swala” na katika hadithi nyingine Mtume amesema “swala ni nguzo (kuu) ya dini mwenye kuisimamisha basi amesimamisha dini na mwenye kuivunja basi amevunja dini”.

 

Wapo baadhi ya maulamaa waliofikia kusema kuwa mwenye ,uacha swala ni kafiri. Hata hivyo kauli hii haimaanishi kuwa ametoka katika uislamu. Ila mwenye kuikataa kabisha nguzo ya swala huyu ametoka kwenye uislamu. Kiukataa na kutokuswali ni vitu viwili tofauti.

 

Katika mapokezi mengine Mtume amesema kuwa jambo la kwanza kuhesabiwa mwanadamu siku ya kiama ni swala. Kama swala itakuwa sawa basi matendo mengine yatachukuliwa kuwa yapo sawa. Ila swala ikiwa ina shida hapo matendo mengine yataangaliwa.

 

Muislamu anatakiwa kuswali swala za sunnah baada ya swala za faradhi kwa swala izi za sunnah zitasaidia kuziba madhaifu yanayojitokeza kwenye kusimamisha swala tano.

 

Kutoa zaka

Kutoa zaka ni kutoa kiasi na kiwango maalumu cha mali  kuwapa watu maalumu. Sio kila mali inatolewa zaka. Pia zaka inatolewa kwa kiasi maalumu kidogo tu kwenye mali nzima. Watu wanaopasa kupewa zaka ni:-

  1. Mafukara
  2. Masikini
  3. Wenye kuikusanya
  4. Wenye kuzoeshwa nyoyo zao kwenye dini mfano waliosilimu hivi karibuni
  5. Watumwa
  6. Wenye madeni
  7. Kwenye njia ya Allah mfano jihadi
  8. Wasafiri

Mali ambazo zinatolewa zaka

Kama nilivyotangfulia kusema hapo awali kuwa sio kila mali inatolewa zaka. Malia ambazo zinatolewa zaka ni pamoja na:-

  1. Wanyama wanaofugwa wenye miguu minne
  2. Madini kama dhahabu na fedha
  3. Mavuno ya shambani
  4. Matunda
  5. Mali ya biashara

 

Kufunga ramadhani

Kufunga ramadhani ni nguzo muhmu kwa waislamu kiroho na kwa ajili ya afya zao. Imepokelewa hadithi kuwa Mtume amesema “fungeni mtapata afya” . Ni dhahiri hata wataalamu wa afya wanathibitisha kuwa funga ina faida kiafya. Hata hivyo sio waisamu wote wana ulazima kufunga.

 

Kufunga maana yake ni kujizuia, kisheria kufunga ni kujizuia kytokana na kula na kunywa pamoja na matendo maovu kutokea alfajiri mpaka jua linapozama. Hata hivyo watoto wadogo, wagonjwa, wajawazito, wanaonyonyesha pamoja na wazee vikongwe sio lazima kufunga.

 

Pia itambulike kuwa kuwa  wengine sio lazima kufunga ila watatakiwa kulipa mfano wanaonyonyesha. Pia wapo ambao hawatatakiwa kulipa ila watatoa fidia mfano wazee vigkongwe. Tutajifunza zidi kwenye darsa zetu za fiqh.

 

Kuhiji:

Kihiji ji kukusudia kuiendea nyumba ya Allah kule Makkah kwa ajili ya ibada. Hija ina mkusanyiko wa ibada mbalimbalia mabazo zina mahusiano na historia za mitume mbelimbali. Ibada kuu katika ibada za hija ji kusimama ‘arafah.

Nguzo hii ya hija ni lazima kwa mwenye kuweza. Na ni lazima mara moja tu katika umri. Yaani ukienda mara moja huna ulazima wa kwenda tena. 

 

Mwisho:

Katika somo hili nimekufundisha kwa ufupi kuhusu hizi nguzo za uislamu. Tutajifunza kwa undani zaidi kuu ya nguzo hizi tutakapokuwa tunasoma mambo maalumu yanayohusiana na nguzo hizo. Sdomo linalofuata tutajifunza hukumu za uislamu.

 

JIPIME:

  1. Nini maana ya uislamu?
  2. Ni mali zip hutolewa zaka?
  3. Taja aina 8 za watu wanaopewa zaka
  4. Ni nguzo ipi ya uislamu ni lazima mara moja tu katika umri?
  5. Ni nguzo ipi kuu katika kungo za uislamu?





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1430


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Dhana ya haki na uadilifu katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Aina za Najisi na twahara katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu Soma Zaidi...

ZIJUE HUKUMU NA FADHILA ZA KUTOA ZAKA KATIKA UISLAMU
Zaka ni nini? Soma Zaidi...

kuletewa ujumbe
(c)Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

Namna ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Wenye ruhusa za kutofunga ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

mambo yanayofungua swaumu
post hii ijakwenda kukufundisha mambo yanayoharibu funga Soma Zaidi...

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA
*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko. Soma Zaidi...

Madhara ya riba kwenye jamii
Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba? Soma Zaidi...

Aina za swala..
Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Funga ya ramadhan na nyinginezo
Nguzo za uislamu (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...