Posti hii inakwenda kukufundisha kuhush swala za sunnah.
Kusimamisha Swala za Sunnah
Baada ya Swala tano za faradhi, kuna swala nyingine za nyongeza alizozisimamisha Mtume (s.a.w) na akatuagiza nasi tumuigize. Swala hizi za ziada tunaziita Swala za Sunnah (Nawafil).
Lengo la Swala za sunnah ni lile lile la swala za faradhi la kututakasa na mambo maovu na machafu. Ni muhimu kwa kila Muislamu kudumisha hizi swala za Sunnah kwa sababu zifuatazo:
1.Kusimamisha Swala za Sunnah ni katika kumtii na kumuigiza Mtume (s.a.w), jambo ambalo ametuamrisha Allah (s.w) katika Qur-an:
2.Kusimamisha swala za sunnah kutatupelekea kufikia ucha Mungu kwa wepesi.
3.Swala za Sunnah pia zina kazi ya kujaziliza swala za faradhi ambazo kwa sababu ya udhaifu wa kibinaadamu hazikuswaliwa kwa ukamilifu unaostahiki.Kama tunavyojifunza katika Hadithi zifu atazo.
Imesimuliwa na Abu Hurairah (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: Amali ya kwanza atakayoulizwa mtu siku ya Kiyama (siku ya Hukumu) ni Swala. Swala zake zikiwa zimekamilika atafuzu. Swala zake zikiwa pungufu atafeli na kuhasirika. Kama swala zake za faradhi zitakuwa zimepungua, Allah (s.w) atasema angalia kwa mja wangu kama anaswala za ziada (Sw ala za Sunnah) ili zichukuliwe kujazia sehemu iliyopungua katika sw ala za faradhi. Kisha ndio vitendo vyake vingine vitaangaliw a kwa namna hiyo hiyo”. (Tirmidh, Abu Daud, An-Nasai, Ibn Majah na Ahm ad).
Swala za Sunnah ni nyingi. Muislamu anatakiwa, kila atakapohisi kuhitajia msaada wa Allah (s.w) atatawadha na kuswali kwani Allah (s.w) anatuagiza:
“Jisaidieni (katika mambo yenu) kwa kusubiri na kuswali, na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu. Ambao wana yakini ya kwamba watakutana na Mola wao na watarejea kwake”. (2:45-46)
Hata hivyo katika kitabu hiki tutajihusisha na Swala maalum za Sunnah zifuatazo:
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowHaya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kuhusu funga za kafara, zinavyotokea na na jinsi ya kuzifunga.
Soma Zaidi...Mtume amemfundisha kuwa watoto wafundishwe kuswali wakiwa na miaka saba na waadhibiwe wakiacha wakiwa na miaka 10
Soma Zaidi...Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa.
Soma Zaidi...