image

Kumuandaa maiti kabla ya kufa na baada ya kufa, mambo muhimu anayopasa kufanyiwa maiti wa kiislamu

3.

Kumuandaa maiti kabla ya kufa na baada ya kufa, mambo muhimu anayopasa kufanyiwa maiti wa kiislamu

3.0 MAMBO YA FARADH KWA MAITI YA MUISLAMU.

3.0 MAMBO YA FARADH KWA MAITI YA MUISLAMU.
3.1 Kuna aina Kuu mbili za Faradh.
Fardh A’in.
Ni faradh inayomlazimu kila mtu binafsi kuitekeleza, haina uwakilishi.
Mfano; kusimamisha swala, kufunga saumu, kuhiji, kutoa zaka, n.k.Faradh Kifaya.
Ni faradh ya kuwakilishana, wachache wakitekeleza hutosheleza hitajio.
Mfano; kuswalia maiti, n.k. lakini akikosekana wa kuwakilisha, waislamu wote wanaohusika watawajibika.

3.2 Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa Kiislamu.
- Kila nafsi itaonja mauti (kifo). Qur’an (3:185) na (4:78).
Mambo manne yafuatayo ni lazima kufanyiwa maiti ya kiislamu:
1.Kuoshwa (Kukoshwa).
2.Kuvikwa sanda (kukafiniwa).
3.Kuswaliwa.
4.Kuzikwa.Mambo muhimu anayofanyiwa Muislamu (mtu) anayekaribia kufa.
Mtu akikaribia kufa huwa hajiwezi kwa lolote lile pamoja na elimu, ujuzi alionao, hivyo huhitajia kufanyiwa mambo yafuatayo;
i.Kuogeshwa, kugishwa mswaki na kumpaka mafuta au manukato kama kuna uwezekano.
ii.Kumlaza kwa ubavu wa kulia au chali na kumuelekeza Qibla iwapo kuna uwezekano.
iii.Kumpa maji ya kunywa.
iv.Kutamka (kumsomea) – Shahada “Laa ilaha illallaah”
Abu Said na Abu Hurarirah wamesimulia kuwa, Mtume wa Allah amesema: “Wasomeeni watu wenu wanaokaribia kufa; ‘Laailahaillallaah”Pia Mu’az bin Jabal amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Yule ambaye maneno yake ya mwisho yatakuwa; “Laailahaillallaah” ataingia peponi.
(Abu Daud)
- Si lazima anayekufa aitamke kwa sauti, inaweza ikawa kimoyo moyo.Mambo anayofanyiwa mtu (maiti) mara tu baada ya kufa.
Baada ya mtu kufa inatuwajibikia tuseme: “Innalillah wainnailaihraaji’una”. Qur’an (2:156). Kisha kumfanyia maiti mambo yafuatayo:

i.Kwa taratibu kurudishia mdomo wake usiwe wazi kwa kufunga kwa kitambaa kutoka kidevuni na kuzungushia kichwani.ii.Kufunga macho ya marehemu na huku ukisema;
“Kwa jina la Allah na kwa kufuata mila ya Mjumbe wa Allah, Ewe Mola wetu mrahisishie mambo yake ya sasa na msahilishie mambo yake ya baadaye. Na jaalia anayokutanayo yawe bora kuliko aliyoyaacha.”iii.Lainisha viungo vyake (miguu na mikono) kwa kukunja na kukunjua taratibu.
- Kama kuna ugumu maji ya uvuguvugu au mafuta yanaweza kutumika kulaisha na kunyoosha viungo hivyo.
- Baada ya kulainisha viungo, miguu na mikono inyooshwe na kulazwa uso ukielekezwa Qibla kwenye mkeka au kitanda kisicho na godoro.iv.Maiti avuliwe nguo zote alizokufa nazo na kisha kufunikwa kwa shuka kubwa
- Ni vyema afunwe kitambaa tumboni au kuwekewa kitu kizito ili tumbo lisifutuke.v.Marashi na ubani vitumike kwa wingi ili kuzima harufu ya uvundo wa maiti.


Baada ya kufanyiwa hatua hizo, sasa ni lazima maiti kufanyiwa yafuatayo:
Mambo haya ni faradh Kifaya, wakifanya wachache wanawakilisha wengine.                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 415


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Umuhimu wa funga ya ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nguzo za kufunga ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Muundo wa Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...

Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii. Soma Zaidi...

Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu. Soma Zaidi...

Tofauti kati ya zakat na sadaqat
Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Funga za kafara
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke katika jamii
Unadhani mwanamke kupewa mahari kitendo hiki kinaweza kushusha hadhi yake? Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa mayatima
Soma Zaidi...

Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa
Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii. Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya ndoa ya mke zaidi ya mmoja
Je jamii inachukuliaje swala la kuoa mke zaidi ya mmoja. Soma Zaidi...

Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha. Soma Zaidi...