NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki.
NIMLAUMU NANI.
1. Basi kwa kuwa frank siku zote alijiona mnyonge na ambaye alikuwa mstaarabu aliamua kufunga tena mlango na kuwaacha Amina na James wakiendelea na shughuli zao ila James aliumia sana kuona anamsaliti rafiki yake akaanza kumlaumu Amina na kumlalamikia kuhusu uhusiano wao kwa sababu Amina ndiye aliyemshawishi James.
2. Basi frank alipoendelea kuwaza kuhusu Amina na James ghafla simu ikalia kutoka kwa yule dada aliyempa lift ,akamuuliza hali halisi na jinsi rafiki yake alivyomshauri lakini frank aliishia kuangua kilio kwenye simu ,yule dada aliumia sana akaamua kuendesha gari mpaka kwenye nyumba ya akina james akamkuta frank amekaa chini ya mti na akina James na Amina wamo ndani wakizozana na kulaumiana, basi yule dada akamsihi frank apande kwenye gari na akakubali wakaenda sehemu iliyotulia wakaongea.
3. Basi frank akamuuliza yule dada jina akamjibu na kusema kwamba anaitwa Amisa , ndipo frank akajaribu kumweleza kila kitu ila kwa uchungu mkali na kilio ila Amisa akamsihii ajitahidi basi frank akafanikiwa kumweleza kila kitu kilivyokuwa basi Amisa akamsihii frank ajitahidi na akahaidi kumsai dia kwa kila kitu atakachohitaji, basi Ili Amisa kumfurahisha Frank aliamua kumpeleka beach Ili afurahie na kupoteza mawazo, basi frank Ms Amisa wakaongozana mapaka beach.
4. Basi wakiwa huko beach Amisa alinunua kila kitu ambacho frank alihitaji na walifurahi na Amisa alifurahi kuona frank anapoteza mawazo, basi na akina James na Amina nao walifika pale beach wakiwa wameshikana mikono wakitembea ufukweni mwa bahari, basi katika pita pita zao Amina akamwona frank na Amisa wanakunywa na kula kwenye meza yao na kila kitu kilikuwepo ambacho kilivutia kwa macho.
5. Basi Amina akamwachia James mkono kwa nguvu na kuanza kumlalamikia na kusema wewe uliaribu penzi letu ona sasa frank ana msichana mwingine wanakula na kunywa na wewe hauna hata miatano ya kununua soda, wakazozana hapo na James akamwambia Amina kwamba ni wewe uliyearibu urafiki wangu na James,hali haikuwa nzuri kila mtu akapitia Njia Yake ila macho ya Amina ni kuangalia Frank atapitia njia ipi.
Itendelea
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 ai web app π2 kitabu cha Simulizi π3 web hosting π4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π5 Madrasa kiganjani π6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya.
Soma Zaidi...NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku
Soma Zaidi...Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara.
Soma Zaidi...Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 4)
Posti hii inaendelea kuelezea hasara za kuwepo kwa wivu na kutokuwa wazi katika, jamii inafikia wakati baba anapifahamu ukweli anawaita wazazi wawili na kuwaombeza kwa kuwa kimya baada ya kuona matatizo yaliyokuwa yanampata mtoto Lisa.
Soma Zaidi...Hadithi katika kijiji cha burugo
Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii .
Soma Zaidi...SAFARI YA MUUJIZA
Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama.
Soma Zaidi...