NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tatu)


image


Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina.


NIMLAUMU NANI .

1. Basi pale beach baada ya kumwona Frank akiwa na Amisa rafiki yake mpya wakila na kunywa Amina aliona wivu na kuanza kumwita Frank ila Frank akimwangalia kama vile hajawahi kumwona na ukizingatia James alikuwa hana kitu hata senti moja kwa kuwa Amina anapenda sana kula aliumia sana akifikiria kwamba Frank amepata mchumba mpya na mwenye hela zake, na walipokuwa wamemaliza kula na kunywa wakaamua kupanda gari kuelekea hotelini kwa maongozi zaidi kwa sababu pale Amina alikuwa anawaletea  hewa ambayo si nzuri, kwa hiyo Frank na Amisa walipanda gari na Amina akawasindikiza kwa macho huku akimlaumu sana James na pia James akambembeleza na kumshika mkono lakini hakujali akauachia  mkono kwa nguvu na akaamua kupanda bodaboda na kwenda sehemu ya hotel ambapo frank na Amisa wakielekea, hapo njiani akiwa amepanda bodaboda alipata ajali yeye na mwendesha bodaboda.

 

 

2. Basi pale walipopatia ajali ilikuwa sehemu moja ambayo ipo karibu na ile hoteli waliokuwepo akina Frank na Amisa kwa  hiyo na akina Frank walikuja na Frank alipomwona mpenzi wake wa zamani moyo uliuma sana na akaanza kumbeba Amina akampangusa vizuri na kusaidiana na Amisa wakampeleka hospitalini na baada ya hapo ilibidi Frank kumpigia James simu kumwambia habari za Amina James aliumia sana na kudai kuwaa wa walikuwa wote kwa nini ajali imetokea na hatimaye yeye ndiye aliyeiona,basi Frank baada ya kusikia lawama zote aliamua kuachana naye na kwenda kwa wazazi wa Amina na kutoa taarifa ya ajali iliyotokea.

 

3. Basi baba na Mama wa Amina walikuwa wameshaona kwamba kuna uhusiano kati ya Amina na Frank, walimuuliza Frank maswali mengi kuhusu ajali ilikuwaje ila Frank hakujibu chochote kwa sababu hakujua Amina alikuwa anaelekea wapi ila alieleza jinsi alivyokuta watu wamemzunguka na kwa kuwa alimfahamu alimpeleka hospitali na kuja hapo kutoa taarifa baada ya mahojiano kati ya Frank na wazazi wa Amina mara moja aliingia James akiwa analia machozi mengi akilaani kwamba Frank amemsaliti rafiki yake na kufanya mpango ili agongwe na kupata ajali baada ya wazazi wa Amina kusikia hivyo waliumia sana na baba Amina akachukua bunduki ili kumshuti Frank, kwa hiyo Frank aliumia sana akapaswa kukimbia na kumpigia Amisa aliyekuwa amebaki hospitalini kwa ajili ya kumhudumia Amisa na wakaondoka zao.

 

4. Basi Frank alilia sana na kuamua kutaja sentensi hizi mara kwa mara alisema NIMLAUMU NANI? Ila Amisa alimbembeleza kadri alivyoweza ili aweze kutulia na kuona ni kawaida akimwambia kwamba hao ndio binadamu, kwa hiyo baba yake na Amina alikuwa mtu mkubwa akaanza kumfuatilia sana Frank ili aweze kumpeleka polisi,kwa bahati nzuri siku moja Amisa akiwa kazini aliweza kuona mabango mbalimbali katika miji yalibandikwa na picha ya Frank ipo ikisema huyu mwalifu anatafutwa kwa sababu Amisa alijua kila kitu na ukweli wake aliamua kueleza kila kitu kwa watu ili kuonyesha ukweli ila mwenye hela hata kama ni uongo siku zote anapenda kushinda .

 

 

5. Basi hali ya Amina iliendelea vizuri na kwa kuwa alimpenda Frank baada ya kusikia tuhuma alizozifanya James alifurahi sana na akamwambia frank kwamba naomba uachane na huyo dada na ukiachana naye na kunipenda mimi nitamwambia baba na kesi yako itaisha au la utaishia jera,hapo Frank akachanganyikiwa kwa sababu alikuwa anampenda sana Amisa kwa sababu ya uchumi wake ulikuwa mzuri na alikuwa anampa Frank kila kitu ingawa hawakuwa wote kimapenzi ila ulikuwa ni msaada ambao Amisa aliutoa kwa Frank baada ya maumivu aliyoyapata, Frank alijaribu kumwomba msamaha Amina na kumweleza ukweli kwamba Amisa sio mpenzi wake ila Amina hakuamini, kwa sababu kipindi hicho Frank alikuwa anaishi kwa Amisa na Amisa alisikia kila kitu kwamba yeye si mpenzi wa Frank aliumia sana kwa sababu lengo la Amisa ni kutaka Frank awe mme wake kwa sababu alikuwa ni kijana mzuri wa sura na tabia kwa hiyo aliamua kuongea na Frank kama tutakavyoona.

 

6. Ilikuwa ni mda wa jioni Amisa alimwita Frank na kuanza kupiga naye story akimuuliza habari za wazazi wake Frank akamwambia kwamba wazazi wake wako kijijni ila yeye alikuja mjini kutafuta maisha na pia ana mpango wa kurudi huko kwa sababu ya vitisho vya Baba Amina, na pia Amisa akamuuliza kuhusu mahusiano na ni mwanammke gani ambaye angependa kumwoa akamwambia angependa kuishi na mwanamke wa kijijini kwa sababu yeye ni maskini, akaendelea kumwambia kwamba je akipata tajiri kama yeye akasema naweza kumshukuru Mungu kwa sababu wanaweza kusaidiana kwenye maisha , basi hapo Amisa akaingia kwenye Friji akatoa kinywaji wakaanza kuangalia move huku Amisa akiendelea kumpatia frank kinywaji ili alewe na Frank akaendelea kunywa na kulewa hatimaye akalala kwenye kochi ila Amisa alikuwa hajalewa akambeba Frank mpaka kitandani mwake akamvua nguo zote akamvalisha nguo za kulalia na yeye akavaa nguo za kulalia akalala kwenye kitanda cha Frank, na kujifunika shuka moja, basi Frank aliposhutuka usingizini na pombe kumwishia akashtuka kuona pembeni mwake kuna mtu akaanza kupiga kelele na kusema Amisa dada yangu nisaidie, Amisa akamwita Frank akasema mimi akamuuliza mbona uko hapa akasema tulia nikwambie mimi ndiye mke wako fanya chochote upendacho, Frank akamsihii akasema wewe ni dada yangu na unanisaidia siwezi fanya lolote.

itaendelea 

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    2 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    3 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Ndani ya pango la makaburi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Malipo ya wema ni wema
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu. Soma Zaidi...

image Hadithi ya Kaka wa kwanza wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Safari ya sita ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

image Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mtihani penzini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Harusi ya aladini na binti sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...