Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito, ni ugonjwa unaowapata sana akina mama wajawazito na uisha tu pale Mama anapojifungua kwa hiyo tunapaswa kujua wazi sababu za ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito.
Ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito.
1. Kwanza kabisa ugumu wa choo ni hali inayotokea kwa wajawazito ambapo choo ushindwa kutoka nje au kwa wakati mwingine utoka nje kwa kutumia nguvu kubwa hii ni kwa sababu kuna mabadiliko kwenye mfumo wa umengenywaji ambapo usababisha maji kuisha kwenye kinyesi na kusababisha ugumu wa kinyesi na pengine hali huu usababishwa na kubadilika kwa homoni za mimba hasa hasa progesterone homoni.
2. Kwa hiyo kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo hili la choo kuwa kigumu, Mama wajawazito wanapaswa kunywa maji mengi ili kurainisha chuo na pia wanapaswa kutumia aina mbalimbali za matunda kama vile mapapai, maparachichi, maembe na matunda mengine mbalimbali ambayo ufanya kinyesi kuwa kiraini, pia wanapaswa kutumia mboga mboga za majani kwa wingi, na chakula chenye mlo kamili ili kuweza kupunguza hali huu ya kinyesi kuwa kigumu.
3. Kuna njia nyingine ambayo ni kunywa maji asubuhi kabla haujala chochote na hali hii pia upunguza ugumu wa choo, na pia akina Mama wajawazito wanapopata tatizo kama hili wanapaswa kuachana na vyakula ambavyo kwa asili yake ufanya kinyesi kuwa kigumu kama vile vyakula vya mtama na vyakula vingine ambavyo vinaweza kuongeza tatizo zaidi.
4. Na pia wanawake wajawazito wanapaswa kufanya mazoezi mengi hasa hasa kutembea walau kwa dakika thelathini kila siku ili kuweza kulifanya tumbo kubwa laini na kinyesi kupunguza ugumu wake, na baada ya kufanya mazoezi akina Mama wanapaswa kunywa maji ya kutosha. Na pia wauguzi na wataalam wa afya wanapaswa kuwaeleza wazi wajawazito kubwa huu ni ugonjwa ambao upo na uisha tu baada ya kujifungua.
5. Kwa kawaida kuna jamii nyingine ambazo uwa na imani potovu na kufanya vitendo ambavyo ki afya hairuhusiwi kwa Maana mama mjamzito akipatwa na tatizo la ugumu wa kinyesi wanachukua mti wanamkalisha mama na kuanza kuchokonoa kinyesi ili kitoke taratibu hii ni hatari kwa sababu wanaweza kuharibu na sehemu mbalimbali kwa sababu ya kuchokonoa na mti kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii nzima ili kuepuka udhalilishaji wa kijinsia na kusababisha uharibifu kwa akina Mama.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi Ute ambao umo kwenye uke, Ute huu utofautiana kulingana na hali ya mama aliyonayo, kama mama ana mimba uke utakuwa tofauti na yule ambaye hana mimba au kama Ute una una magonjwa na hivyo utakuwa tofauti.
Soma Zaidi...Post hii inazungumzia mama wajawazito Mara tu mama anapohisi kuwa yeye ni mjamzito anashauriwa kuanza clinic.na clinic hizi zinasaidia kuwapatia wakina mama elimu,namna ya kumkinga Mtoto asipatwe na maradhi Kama UKIMWI. Pia mama anapoanza clinic
Soma Zaidi...Maumivu yavtumbo huwenda yakachanganya sana, Keane yanahusianana sababu nyingi sana. Kina baadhi ya watu hupata na maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa ama punde tu baada ya kumaliza.
Soma Zaidi...Hivi unadhani kuharisha ni katika dalili za mimba, vipi kuhusu kutopata choo pia inaweza kuwa ni ujauzito?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuongezeka uzito kwa wajawazito, Mara nyingi Mama akibeba mimba uongezeka uzito kutoka wiki ya Kwanza mpaka wiki ya mwisho ya kujifungua.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama anaenyonyesha
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mwanamke hapaswi kufumbia macho.
Soma Zaidi...