Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi

Nitakujiza dawa ya chango na maumivu ya tumbo lahedhi, dalili zake na njia za kukabiliana na maumivu ya tumbo la chango.

Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi

Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi.
Ni hali ya kawaida kwa mwanmke kupatwa na maumivu akikaribia hedhi ama anapokuwa kwenye hedhi. Hali hii haihitaji hata uangalizi wa daktari. Maumivu haya yanaweza kutofautiana kulingana na umri na maumbile. Kwa wanaoanza sasa wanaweza kupatwa na maumivu makali hata kuliko ambao ni wakubwa. Ambao wana matatizo ya homoni mau,ivu yanaweza kuw ani makali pia. Ukali hii ni wenye kuvumilika, lakini inatokea baadhi ya nyakati kwa baadhi ya wanawake maumivu hayawezi kuvumilika ni makali sana, mpaka anapelekwa hospitali.



Basi makala hii ni kwa ajili yako, tutaona sababu za maumivu haya makali yasiyoweza kuvumilika na pia tatuaona dawa za chango na maumivi ya tumbo la hedhi. Usichoke endelea nayo makala hii mpaka mwisho. Ukipenda tuwachie maoni yako hapo chini.



Ni zipio sababu za maumivu makali ya chango na tumbo la hedhi?
1.Kuota kwa vinyama maeneo mengine ndani ya mwili lakini nje ya tumbo la mimba. Hali hii inaweza kuwa na dalili kama kupata hedhi yenye damu nyingi sana na za mabonge, hedhi kuwa zaidi ya siku 7, maumivu makali ya tumb, maumivu makali wajati wa kushiriki tendo la ndoa.



2.Kama mfumo wa homoni haupo sawa yaani hormone imbalance. Tatizo la homoni ni sugu sana kwa wanawake wengi. Inakadiriwa kuwa katika kila wanawake 10 basi mmoja wao atakuwa na tatizo hili. Shida ya homoni inaweza kuwa na dalili kama:- maumivu makali ya chango, kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, kutokwa na chunusi nyingi usoni, mwanamke kuwa mzito sana, nywele zake zinakuwa dhaifa na kunyonyoka kwa haraka, na ngozi kuwa na madod madoa.



3.Kuwa na uvimbe kwenye mfumo wa uzazi. Mwnamke anaweza kuwa na dalili kama maummivu ya miguu, maumivu ya mgongo kwa chhini, kukosa choo kikubwa, kupata hedhio yenye damu nyingi, maumivu mkakli ya chango, kukojoa mara kwa mara na kushindwa kumaliza mkojo wote anapokojoa.



4.Kuwa na maambukizi au mashambulizi ya bakteria, fangasi na virusi kwenye mfumo wa uzazi. Mwanamke anaweza kupatwa na dalili kama kutokwa na damu kablya ya kuinia hedhi na baada, kutokwa na majimaji yanayotoa harufu ukeni, maumivu makali wakati wa kukojoa, kupata homa.



Sababu nyingine ni:
1.Kukaza kwa tisu za kwenye tumbo la kizazi
2.Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango
3.Maumbile ya mwanamke.



Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi.
A.Ibuprofen (Advil, Motrin IB)
B.Naproxen sodium (Aleve na Anaprox)
C.Ketoprofen (Actron na Orudis KT)
D.Mefenamic acid



Namna ya kukabiliana na tumbo la chango na maumivu ya tumbo la hedhi
1.Fanya mazoezi ya mrakwa mara
2.Hakikisha huna misongo ya mawazo
3.Punguza kula vyakula vyenye chumvi sana pia punguza kula vitu vya sukari sana
4.Punguza unywaji wa chai ya majani ya chai (caffein)
5.Punguza vyakula vyenye mafuta ya wanyama kwa wingi kama nyama.





                   



Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 4709

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Njia za uzazi wa mpango zinazomhusisha mwanaume

Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango unavyofanya na mwanaume kushiriki, ni njia ambayo umfanye mwanaume awe mhusika hasa wakati wa kujamiiana.

Soma Zaidi...
NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME

Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.

Soma Zaidi...
Faida za uzazi wa mpango kwa jamii

Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa jamii, tunapaswa kujua kuwa uzazi wa mpango ukitumiwa vizuri na jamii nayo inapata faida kwa hiyo zifuatazo ni faida za uzazi wa mpango kwa jamii.

Soma Zaidi...
Dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14

Soma Zaidi...
Je mwanamke anaweza pata mimba ikiwa wakati watendo la ndoa hakukojoa Wala kusikia raha yoyote ya sex wakati watendo landoa

Je wewe ni mwanmake unayepata shida kufika kileleni? (Kukojoa wakati wa tendo lwa ndoa). Post hii itakujibu baadhi ya maswali yako.

Soma Zaidi...
Dalili za tezi dume.

Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo anaweza kuzipata mwenye Ugonjwa wa tezi dume, sio Dalili zote mtu anaweza kuzipata kwa sababu dalili kama hizi zinaweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine.

Soma Zaidi...
Kazi na mdalasini katika kutibu matatizo ya homoni.

Posti hii inahusu zaidi kazi ya mdalasini katika matibabu ya homoni kwa wanawake.

Soma Zaidi...
Mabadiliko ya via vya uzazi kwa Mama mjamzito.

Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye via vya uzazi kwa wajawazito, tunajua kuwa Mama akibeba mimba tu kuna mabadiliko utokea katika sehemu mbalimbali za mwili.

Soma Zaidi...
Dalili za kuvimba kwa ovari.

  Posti hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa ovari kunakosababishwa na maambukizo ya bakteria na kawaida huweza kusababishwa na magonjwa sugu katika Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke.

Soma Zaidi...
Mabadiliko ya mzunguko wa damu kwa wajawazito.

Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya mzunguko wa damu kwa wajawazito, tunajua wazi kuwa wajawazito pindi ujauzito ukiingia tu, kila kitu kwenye mwili ubadilika vile vile na mzunguko wa damu ubadilika.

Soma Zaidi...