Umuhimu wa kunyonyesha kwa Mama

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha kwa akina Mama, kunyonyesha ni kitendo ambacho Mama utumia maziwa yake na kumlisha mtoto pindi tu anapozaliwa mpaka wakati anapoachishwa titi, kunyonyesha huwa na faida kubwa kwa wote yaani Mama na mtoto, zif

Umuhimu wa kunyonyesha kwa Mama.

1. Kunyonyesha kwa akina Mama usaidia kuzuia Kansa ya kizazi na Kansa ya matiti, kwa sababu kwenye matiti Kuna chemical nyingi ambazo usaidia kutengeneza maziwa kwa hiyo zikibaki bila kutumiwa na mtoto usababisha Kansa ya matiti kwa hiyo akina Mama ambao Hawanyonyeshi na hawana tatizo lolote wanapaswa kufanya hivyo pindi wanapojifungua  Ili kuweza kuepukana na Kansa ya matiti ambayo inawakumba wazazi wengi kwa asilimia kubwa ni kwa sababu ya kushindwa kunyonyesha.

 

2. Pindi Mama anaponyonyesha mtoto wake anaweza kukaa kwa miezi sita ya mwanzoni bila kubeba mimba, kwa kawaida wale akina Mama wanaotumia mda mwingi kiwanyonyesha watoto wao Wana asilimia kubwa ya kutopata hedhi kwenye miezi yao ya mwanzoni na pia kutotumia aina yoyote ya uzazi wa mpango na hawabebi mimba kwa hiyo akina Mama wanapaswa kunyonyesha watoto wao sio chini ya mara nane kwa masaa Kumi na mawili.

 

3. Kunyonyesha usaidia kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya Mama na mtoto, kwa sababu wakati wa kunyonyesha ndipo Mtoto anaweza kumtambua Mama yake na kuwa na uhusiano mzuri, pia Mama anaweza kujua tabia ndogo ndogo za mtoto wake pindi anaponyonyesha. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kujitahidi kiwanyonyesha watoto wao kwa mda unapaswa.

 

4. Kunyonyesha tu baada ya kujifungua usaidia kuwepo kwa homoni ya oxytocin ambayo usaidia kuzuia kuvuja kwa damu, kwa hiyo Mama anapaswa kunyonyesha mtoto tu baada ya kujifungua na isizidi saa Moja kabla Mama hajapewa mtoto wake ili kunyonyesha mara tu anapozaliwa.

 

4. Pia kunyonyesha usaidia kuwepo kwa homoni ya oxytocin kutoka kwenye ubongo ambayo usaidia uterus ku contract tu baada ya Mama kujifungua.

 

5.Vile vile kunyonyesha usaidia maziwa ya Mama kuzalisha homoni ya lactation ambayo usaidia kuzalisha kwa maziwa.

 

6.kwa hiyo baada ya kujua faida za kunyonyesha akina Mama wanapaswa kukaa na watoto wao kwa mda wa kutosha pindi wanapojifungua Ili kuweza kuzingatia uhusiano mzuri kati ya Mama na mtoto, pia kupunguza kuwepo kwa kufuata kwa watoto bila mpangilio hali ambayo usababisha watoto kutokua vizuri kwa sababu ya kukosa lishe.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/21/Thursday - 10:36:51 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1489


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-