Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Kitabu cha Qur’an |
Vitabu Vingine vya Mwenyezi Mungu |
1. Neno la Asili. Qur’an imebakia katika lugha yake ya asili ya kiarabu fasaha pamoja nakutafsiriwa katika lugha tofauti. |
Vitabu vingine lugha zao za asili zilizoshushiwa zimepotea na kutojulikana. |
2. Lugha zilizoshushiwa Vitabu. Lugha ya Qur’an ni hai kwani mpaka leo inatumika na kufahamika na walimwengu wengi. |
Lugha za vitabu vilivyotangulia ni mfu, zimefutika zamani na hazijulikani na watu. Rejea Qur’an (14:4). |
3. Kuhifadhiwa na Kulindwa Vitabu. Qur’an imebaki katika asili yake kama ilivyoteremsha bila kubadilishwa chochote na wanaadamu ndani yake. Rejea Qur’an (15:9) na (41:42) |
Vitabu vingine vimepotea katika asili yake kwa kupunguzwa, kuongezwa na kupotoshwa asili ya ujumbe wake na mikono ya wanaadamu.. |
4. Hitoria ya Kushushwa Vitabu. Historia ya kushushwa Qur’an inajulikana vyema mfano; namna, sehemu, muda/kipindi na sababu ya kuteremshwa kila aya. |
Vitabu vingine historia ya kushushwa kwao haijulikani, mfano; muda, nama, sababu au sehemu. |
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu
Soma Zaidi...Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe).
Soma Zaidi...