Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir

Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu.

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat HashirHuwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu. Na kama mkipigwa vita lazima tutakusaidieni." Na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa wao ni waongo. Kama wakifukuzwa hawatatoka pamoja nao, na kama wakipigwa hawatawasaidia; na kama wakiwasaidia kwa yakini watageuza migongo (wende mbio); kisha hawatanusuriwa. (59:11-1 2)


Hakika nyinyi (Waislamu) mnaogopwa zaidi katika nyoyo zao kuliko wanavyomuogopa Mwenyezi Mungu; maana wao ni watu wasiofahamu (lolote). (59:13)Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vyao vilivyohifadhiwa, au nyuma ya kuta. Vita vyao baina yao vikubwa. Utawadhani kuwa wako pamoja; kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasio na akili. Hali yao (hawa Mayahudi wa Kibanu Nadir) ni kama ya wale (Mayahudi wa Bani Qaynuqai) waliowatangulia (kufikwa na baa) hivi karibuni; walionja ubaya wa mambo yao; na watapata adhabu (nyingine) iumizayo (vile vile). Ni kama Shetani anapomwambia mtu: "Kufuru;" na anapokufuru akamwambia: "Mimi si pamoja nawe, hakika namuogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu. "(59:14-16)


Basi mwisho wa wote wawili hao ukawa waingie Motoni kukaa humo daima; na hiyo ndiyo jaza ya madhalimu. (59:17)Sifa za wanafiki zilizoainishwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo:
(i)Hushirikiana na kusaidiana na makafiri katika kuuhujumu Uislamu na Waislamu.
(ii)Wanawaogopa watu kuliko wanavyo muogopa Allah (s.w)
(iii)Wanaonekana kuwa wamoja lakini kiutendaji kila mmoja yuko na lake. Umoja wao ni kama ule wa inzi, likitupwa jiwe kila mmoja hutawanyika kikwake tofauti na mshikamano ule wa kundi la nyuki ambao wakichozwa hushambulia kwa pamoja mpaka kumkibiza adai
                   
Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 145


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Sheria Katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

Maana ya Hija na Umuhimu wa kuhiji
Soma Zaidi...

Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

swala ya kuomba mvua na namna ya kuiswali
12. Soma Zaidi...

DUA 51 - 60
51. Soma Zaidi...

Kufunguliwa Yusufu(a.s) Kutoka Gerezani
Yusufu(a. Soma Zaidi...

Masomo ya Dua na Faida zake Dua
Soma Dua mbalimbali hapa, Soma Zaidi...

Kiwango cha mahari katika uislamu
Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari? Soma Zaidi...

MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam). Soma Zaidi...

swala ya witri na namna ya kuiswali
3. Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa mayatima
Soma Zaidi...

Aina 12 za swala za sunnah na idadi ya rakaa zake wakati wa usiku na mchana
Aina za Swala za Sunnah. Soma Zaidi...