Mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu
Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)
Mgawanyo wa Elimu usiokubalika katika Uislamu (usio sahihi).
- Katika Uislamu, HAKUNA mgawanyo wa ‘Elimu Dunia’ na ‘Elimu Akhera’.
- Mgawanyo huu ni potofu wenye dhana ya kikafiri kuwa kuna maisha ya Dini yanayoongozwa na Mwenyezi Mungu na maisha ya Dunia yanayoongozwa na binaadamu.
Mgawanyo huu sio sahihi kwa sababu zifuatazo:
1. Nabii Adam (a.s) aliandaliwa yeye na kizazi chake kuwa Makhalifa (viongozi) na alifundishwa majina (fani zote) ya vitu vyote.
Rejea Qur’an (2:31) na (2:38-39).
2.Amri ya kusoma aliyopewa Mtume (s.a.w) na umma wake haibagui elimu ya dini na dunia.
3.Muasisi wa (chanzo cha) elimu na fani zote ni Mwenyezi Mungu (s.w). Hakuna mwanaadamu aliyeasisi elimu au fani yeyote ila ni mwendelezaji tu.
Rejea Qur’an (96:3-5).
4. Pia Qur’an inatufahamisha kuwa wanaomcha Allah (s.w) ipasavyo ni waumini wataalamu waliozama katika fani mbali mbali za kumjua Allah (s.w), sio tu fani za kidini za Fiqh, Tawhiid, n.k.
Rejea Qur’an (35:27-28)
6. Katika Qur’an Allah (s.w) anatufahamisha kuwa waumini wenye elimu ya fani mbali mbali ndio wenye daraja kubwa zaidi mbele yake.
Rejea Qur’an (58:11), (49:13).
7. Hakuna mgawanyo wa elimu unaooneshwa katika Hadith za Mtume (s.a.w) zinazoelezea fani za elimu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 web hosting 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
KUAMINI VITABU VYA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya vitabu vya Allah (s.
Soma Zaidi...Sifa za waumini wa ukweli katika uislamu
Je unamjuwq ni nani muumini, na ni zipi sifa za muumini?
Soma Zaidi...Mgawanyiko wa Elimu katika mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira.
Soma Zaidi...