Katika Uislamu imani inanguzo kuu 6.Pia muumini anatakiwa ajipambe na sifa za waumini. Posti hii itakufundisha kuhusu imani katika Uislamu.
Maana ya imani
Imani: ni neno la Kiarabu lenye maana ya kuwa na yakini au kuwa na uhakika moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana machoni lakini kuna dalili za kuthibisha kuwepo kwake
. Hivyo ili mtu awe na imani juu ya jambo lolote lile asiloweza kuliona, hanabudi kuwa na ujuzi wa kina utakaompa hoja au dalili za kutosha zitakazomkinaisha moyoni juu ya kuwepo jambo hilo.
Nani Muumini?
Imani ni kitu cha moyoni kisichoonekana lakini dalili za Muumini huonekana kwenye matendo. Katika Uislamu mtu hatakuwa Muumini kwa kudai tu bali uumini wake utaonekana katika matendo yake.
Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa:
“Na katika watu wako wasemao, ‘tumemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.”(2:8).
Si wenye kuamini kwa sababu hawajaingiza imani yao katika matendo bali wamebakia kwenye kudai tu kuwa wao ni waumini pengine kwa kujiita majina au kuchagua kufanya vitendo fulani fulani tu.
Muumini wa kweli ni yule atakayethibitisha imani yake katika mwenendo na matendo yake ya kila siku.
“Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.(8:2).
Ambao husimamisha swala na wanatoa katika yale tu liy ow apa. (8:3).
Hao ndio wanaoamini kweli kweli, wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora kabisa”. (8:4).
“Wenye kuamini kweli kweli ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kisha wakawa si wenye shaka na wanaopigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kw eli kweli” (49:15)
Sifa za waumini
Umeionaje Makala hii.. ?
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي ذَرٍّ جُنْدَبِ بْنِ جُنَادَةَ، وَأَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ رَسُولِ اللَ...
Soma Zaidi...Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu?
Soma Zaidi...Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Soma Zaidi...