Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah

Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah


Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu iumizayo kwa sababu ya kule kusema kwao uwongo. (2:8-10)


Na wanapoambiwa: "Msifanye uharibifu ulimwenguni." Husema "Sisi ni watengenezaji. "Hakika wao ndio waharibuji, laini hawatambui.Na wanapoambiwa: "Aminini kama walivyoamini watu" Husema"Oh! Tuamini kama walivyoamini wale wapumbavu?" Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui. (2:11-1 3)



Na wanapokutana na walioamini husema: "Tumeamini"; na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema: "Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunawacheza shere tu." Mwenyezi Mungu atawalipa shere yao na kuwawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo. Hao ndio waliokhiari upotofu kuliko uongofu; lakini biashara yao haikupata faida wala hawakuwa wenye kuongoka. (2:14-1 6)


Mfano wao (hawa wanafiki) ni kama mfano wa wale (wasafiri waliokumbwa na kiza) wakakoka moto, (na) ulipowaonyesha yaliyo pembezoni mwao, Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao hiyo na kuwawacha katika viza; hawaoni. (2:17)


Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea. (2:18)


Au (mfano wao pia) ni kama mvua kubwa itokayo mawinguni; ndani yake mkawa mna viza na radi na umeme; wakawa


wakitia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya mingurumo, kwa kuogopa kufa; (na kufanya hivyo hawakusaidii kitu). Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema hao makafiri. (2:19)


Unakaribia umeme huo kunyakua macho yao; kila unapowaangazia huenda ndani yake na unapowafanyia giza husimama. Na Mwenyezi Mungu angependa angaliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuweza juu ya kila kitu. (2:20)



Kutokana na aya hizi tunajifunza sifa za wanafiki zifuatazo:
(i)Kuonesha imani ya uongo. Katika vinywa vyao wanadai kuwa ni waumini lakini katika nafsi zao na matendo yao wanaikanusha imani yao.
(ii)Wanauchukia Uislamu nyoyoni mwao, na wanazidi kuuchukia kila Uislamu unavyosonga mbele.
(iii)Hufanya uharibifu katika nchi huku wakidai kuwa wanatengeneza.
(iv)Huwabeza waumini wa kweli wanaofuata Uislamu vilivyo.
(v)Hawana msimamo. Wanataka wapate maslahi ya Uislamu na wakati huo huo wawe pamoja na makafiri.
(vi)Wanawacheza shere Waislamu.
(vii)Kwa mujibu wa mfano uliopigwa katika aya ya 17 (2:17) wamekhiyari kupotea baada ya kujiwa na mwongozo (nuru).
(viii)Kwa sababu wamedhamiria upotevu badala ya uongofu kwa ajili ya maslahi ya dunia, hata ukiwaita kwenye uongofu hawawezi kuja. Wamefananishwa na watu wenye vilema vitatu kwa pamoja vya uziwi, ububu na upofu. Hivyo hawawezi kusikia neno la mwenye kuadhini wala la mwenye kukimu.


Kwa mujibu wa mfano uliopigwa katika aya ya 19 na 20 (2:19-20), wanafiki wanatamani matunda yatokanayo na kusimama kwa Uislamu katika jamii lakini hawako tayari kukabiliana na changamoto zinazotokana na mchakato mzima wa kusimamisha Uislamu katika jamii. Wanafurahia matunda yanayotokana na mvua nzuri za masika lakini hawako tayari kukabiliana na radi, ngurumo na umeme vinavyoandamana na mvua hizo.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1106

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Athari za vita vya Uhud

Vita vya uhudi viliweza kuleta athari nyingi. Post hii itakuletea athari baadhi za vita hivyo.

Soma Zaidi...
Maswali kuhusu njia za kumjua mwenyezi Mungu

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu

Soma Zaidi...
Kina Cha uovu wa shirk

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Himizo la kuwasamehe waliotukosea

β€œNa wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).

Soma Zaidi...
Nguzo za imani katika uislamu na mafunzo yake

Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu nuzo 6 za imani ya uislamu na pia utajifunz akuhusu mafunzo yanayoweza kupatikana kwenye Nguzo hizi.

Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu katika uislamu

Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu.

Soma Zaidi...
(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini

Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini.

Soma Zaidi...