Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil

Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil

Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s.

Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil

Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil.


Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s.w)katika ardhi takatifu. Lakini ubaya wa bahati, Bani Israil walikhini amana hii na kuwa wezi wa fadhila. Hebu turejee Qur'an tuone baadhi ya neema za Allah juu ya Bani Israil na jinsi walivyofanya ukaidi.



"Enyi kizazi cha Israili! Kumbukeni neema zangu nilizokuneemesheni na nikakutukuzeni kuliko viumbe wengine (wakati huo)" (2:47).




Na (kumbukeni) tulipokuokoeni kwa watu wa Firauni waliokupeni adhabu mbaya; wakiwachinja watoto wenu wanaume na kuwawacha hai wanawake; na katika hayo (kuokolewa huko) ilipatikana neema kubwa iliyotoka kwa Mola wenu. Na (kumbukeni) tulipoitenga bahari kwa ajili yenu na tukakuokoeni, na tukawazamisha watu wa Firauni na hali mkitazama" (2:49-50).



Na (kumbukeni habari hii pia): Mliposema: "Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi". Yakakunyakueni mauti ghafla na hali mnaona. Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru. Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu (mlipokuwa mnakata jangwa kutoka Misri kwenda Palestina) na tukakuteremshieni Manna na Salwa: (Tukakwambieni) "Kuleni katika vitu vizuri hivi tulivyokuruzukuni." Nao hawakutudhulumu sisi (walipokhalifu amri yetu) lakini walikuwa wamejidhulumu nafsi zao." (2:55-57).




Na (kumbukeni khabari hii nayo): Musa aliomba maji kwa ajili ya watu wake, tukasema: "Lipige jiwe kwa fimbo yako" mara zikabubujika humo chem.-chem kumi na mbili; kila kabila likajua mahali pake pa kunywea. (Tutawaambia) kuleni na kunyweni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika ardhi mkafanya uharibifu. Na (kumbukeni) mliposema: "Ewe Musa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi, kama mboga zake na matango yake na ngano yake na adesi zake na vitunguu vyake". Akasema (Mwenyezi Mungu): "Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora? Nendeni kwenye mji, huko mtapata mlivyoviomba"; Na ikapigwa juu yao (chapa ya) dhila (unyonge) na umaskini; nawakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu na wakiwaua manabii pasipo haki. Basi haya ni kwa sababu ya kuasi kwao na kupindukia mipaka (ya Mwenyezi Mungu) (2:60-61).



Hizo ni baadhi tu ya aya miongoni mwa aya zibainishazo neema za Allah juu ya Bani Israil na ukaidi wao.



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 1404

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 web hosting     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Mambo anayofanyiwa maiti baada ya kufa

Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtazamo wa makafiri juu ya dini

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake

Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu.

Soma Zaidi...
Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri

Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera.

Soma Zaidi...
Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab

Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa

Soma Zaidi...