picha

Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

  1. Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).

 

- Ni viumbe wa kiroho wenye mabawa.

- Ni viumbe wasio na matashi ya kimwili (kula, kunywa, kulala, n.k.)

- Hawana hiari katika kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w).

- Ni vimbe wasio na jinsia.

- Ni viumbe walioumbwa kutokana na Nuru.


 

            Zifuatazo ni baadhi tu ya kazi za baadhi ya Malaika.

  1. Kuleta Wahyi (ujumbe) kwa wanaadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Malaika Jibril ndiye mhusika mkuu wa kupeleka wahyi kwa mitume na manabii.

Rejea Qur’an (81:19-20), (16:2) na (11:69-73).

 

  1. Kumchunga na Kumlinda kila mtu na kuandika amali zake nzuri na mbaya.

Kila mtu anakundi la malaika nyuma na mbele yake kumlinda na mambo yaliyo nje na uwezo wake. Pia kuna malaika wa kulia anayeandika mema na wa kushoto anayeandika maovu ya mtu.

Rejea Qur’an (82:1-12), (50:17-18) na (13:11).

 

  1. Kuwaombea Waumini maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Hawa ni malaika ambao huzunguka katika makundi ya waumini anapotajwa ndani yake Mwenyezi Mungu (s.w) au kusomwa Qur’an Tukufu.

Rejea Qur’an (40:7), (42:5) na (17:78).

 

  1. Kuwasaidia waumini katika vita vya kupambana na maadui wa Allah (s.w).

Pindi waumini wanapopigana katika kusimamisha haki, Mwenyezi Mungu (s.w) huteremsha malaika kuwasaidia.

Rejea Qur’an (3:123-126) na (8:12).

 

  1. Kuwaangamiza watu waovu waliopindukia mipaka.

Watu waovu waliopindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) wakaonywa muda mrefu na wasionyeke huangamizwa na malaika maalum.

Rejea Qur’an (11:81-83).

 

  1. Kutoa roho za viumbe.

Malakul-Maut ndiye mhusika mkuu na wengineo katika kutoa roho za viumbe.

Rejea Qur’an (32:11).

 

  1. Kuzihoji, kuzistarehesha au kuziadhibu roho za wafu kaburini.

Malaika wanaohusika na kazi hii ni Munkar na Nakir.

 

  1. Kupuliza Parapanda siku ya Qiyama.

Mipulizo ya Parapanda katika kufisha na kufufua viumbe siku ya Qiyama itafanywa na malaika Israfil.

Rejea Qur’an (39:68).

 

  1. Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema peponi.

Hili kundi jingine la malaika watakaofanya kazi hiyo siku ya Qiyama.

Rejea Qur’an (41:30-32) na (39:73).

 

  1. Kuwasimanga na kuwaadhibu watu waovu motoni.

Kuna kundi la malaika watakaokuwa wanaadhibu watu waovu motoni. Mlinzi mkuu wa milango ya moto ni Malaika Maalik.

Rejea Qur’an (25:22), (74:26-30) na (43:77).

 

  1. Kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu (s.w).

Kuna kundi la malaika maalum kwa kazi hii tu.

Rejea Qur’an (40:7).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 2149

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

Haki za kielimu za mwanamke katika uislamu

Haki ya ElimuKatika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ?

Soma Zaidi...
Nguzo za imani katika uislamu na mafunzo yake

Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu nuzo 6 za imani ya uislamu na pia utajifunz akuhusu mafunzo yanayoweza kupatikana kwenye Nguzo hizi.

Soma Zaidi...
Elimu yenye manufaa

Elimu yenye manufaa Ni ipi? (EDK form 1:elimu yenye manufaa)

Soma Zaidi...
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo

Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na nini? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo)

Soma Zaidi...
Mgawanyo wa Elimu Usiokubalika katika uislamu.

Kipengele hichi kinahusu mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu.sababu za mgawanyiko wa elimu udio sahihi katika uislamu.

Soma Zaidi...
Aina kuu za dini

Katika kipengele hichi tutajifunza aina kuu mbili za dini.

Soma Zaidi...
Kwa nini Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?

Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu)

Soma Zaidi...
Maana ya uislamu.

Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti.

Soma Zaidi...
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu

Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu Ni upi? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu)

Soma Zaidi...