JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.
FAIDA ZA TANGAIZI
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China. Mmea huu hutambulika kwa faida zake za kitiba toka zamani sana. Na karibia dunia nzima hutumia tangaizi kama tiba na kama kinywaji. Ndani ya tangaizi kuna chembechembe ziitwazo gingerol, hizi ndizo huipa tangaizi uwezo wake wa kitiba.
Unaweza kutumia tangaizi kwa kutafuna vipande vidogovidogo au kwa kutia kwenye mboga. Pia unaweza kuweka kwenye chai ikiwa vipande vidogo au ikiwa imekauchwa na kusagwa kama ungaunga. Zipo njia nyingi za kutumia tangaizi. Zifuatazo ni katika baadhi ya faida za tangaizi iafya:-
- Tangaizi ni mujarabu sana katika kutibu kichefuchefu. Hususani kichefuchefu cha mimba. Kwa ujumla kichefuchefu huwapata sana wajawazito, na watu walofanyiwa upasuaji wa ndani. Lakini kinaweza kumpata mtu yeyote. Unaweza kutumia tangaizi kwenye chai, ama kutafuna vipande vidogo. Hakikisha unakula japo gram moja.
- Hupunguza maumivu ya misuli
- Hupunguza maumivu ya viungo
- Husaidia katika kushusha kiwango cha sukari. Hususan kwa wenye kisukari type 2. kwa kufanya hivi pia hupunguza athari ya kupata maradhi ya moyo
- Husaidia kwa wenye tatizo la kutokupata choo na kukosa hamu ya kula.
- Hupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wanawake.
- Hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani (cancer)
- Huimarisha afya ya ubongo
- Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga za mwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula spinach
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach
Soma Zaidi...Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa
Soma Zaidi...Fahamu virutubisho vya wanga na kazi zake, vyakula vya wanga na athari za upungufu wake
Hapa tutaona kuhusu virutubisho vya wanga, kazi zake na athari za upungufu wake
Soma Zaidi...Matunda yenye vitamini C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matunda yenye vitamin C kwa wingi
Soma Zaidi...