hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini
Vitamini B ni katika water soluble vitamin ambavyo vina kazi ya kuhakikisha kuwa michakato yote ya kikemikali mwilini inakwenda vizuri. Na hapa tunazungumzia kitaalamu metabolism. vitamini B vipo katika makundi mengi kma aB1, B2, B3, B5, B6, B7 na B12. katika makala hii nitakwenda kukueleza maana ya vitamini hivi, nini kazi zake hasa mwilini, wapi nitapata vitamini B na je ni zipi dalili za upungufu wa vitamini hivi.
Yaliyomo:
Vitamini B ni nini?
Vitamini B ni katika kundi la vitamini vinavyofahamika kama water soluble vitamin. vitamini B ni kundi la vitamini ambavyo vinafanana sifa lakini vina utofauti kidogo. Vitamini B ndani ya miili yetu vinafanya kazi ya kuhakikisha kuwa michakato ya kikemikali inafanyika, michakato hiyo kitaalamu inafahamika kama metabolism.
Metabolism hii ni michakato ya kikemikali inayofanyika ndani ya seli kwa ajili ya mambo makuu matatu nayo ni:-
Hivyobasi michakato hii yote ili ifanyike kwa ufasaha na ufanisi vitamini B vinahitajika katika miili yetu. Endelea kusoma makala hii ukaone kazi za vitamini B.
Makundi ya vitamini B
Makundi hayo ya vitamini B ni:
Kazi za vitamini B mwilini Na upungufu wa vitamini B mwilini
Kama tulivyoona kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-
B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.
B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.
B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo
B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.
B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.
B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.
Vyakula vya vitamini B
Tunaweza kupata vitamini B kwenye vyakula vifuatavyo:-
Dalili za upungufu wa vitamini B
Athari za kuwa na vitamini b kupitiliza
Makala nyingine kwa ajili yako:
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Vitamini C ni moja kati ya vitamini muhimu sana katika kuboresha ufanyaji kazi wa mfumowa kinga mwilini yaani immune system. Katika post hii utakwenda kujifunza kazi za vitamini C mwilini
Soma Zaidi...Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha madhara ya kuwa na mafuta mengi mwilimi
Soma Zaidi...Hapa tutaona kuhusu virutubisho vya wanga, kazi zake na athari za upungufu wake
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula biringanya eggplant)
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula uyoga
Soma Zaidi...