Rangi za matunda
Fida za matunda huanzia kwenye rangi zake, je unajuwa kama rangi ya matunda inaeleza jambo?
RANGI ZA MATUNDA
Unaweza kujiuliza ni kwa nini matunda yana rangi mbalimbali? Hili swali Mwenyezi mungu aliyeumba kila kitu ndiye anajuwa saidi. Ila kwa ufupi utambuwe kuwa rangi katika matunda ni dalili ya ishara flani. Katika post hii tutaona baadhi ya rangi katika matunda. Mwisho wa post hii utaweza kutambua nini kimo katika tunda utakaloliona kwa kuangalia rang.
1.rangi nyekundu
Rangi nyekundu kwenye matunda hutokana na nyembenchembe ziitwazo lycopene. Hizi ni antoxidant ambazo husaidia katika kulinda mwili dhidi ya sumu za vyakula. Sumu hizi mara nyingi huweza kuharibu seli ndani ya miili yetu. Pia sumu hizi husababisha mtu kuzeeka haraka. Chembechembe hizi pia husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli mwilini. Huimarisha mfumo mzima wa kinga mwilini. Na pia husaidi akatika kulinda au kupunguza adhari za magonjwa ya moyo na saratani.matunda yenye rangi hii ni pamoja na tomato, matikiti, pilipili n.k
2.rangi ya njano.
Rangi ya njano kwenye matunda husababishwa na chembechembe ziitwazo beta-carotene, hizi pia ni antoxidant. Chembechembe hizi husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini. Mwili huweza kubadili beta-carotene, kuwa vitamini A. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimu sana katika afya ya mtu. Kupamabana mna maradhi mablimbali nna kuimarisha afya ya macho. Kupambana na wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo. Huimarisha afya ya ngizi na maeneo mengune yenye utando laini.miongoni mwa matunda yenye rangi hii ni viazi, karoti, maembe n.k
3.rangi ya kijani.
Rangi ya kijani husaidia kutambuwa uwepe wa vitamini Ana C. Kama inavyotambulika mboga za majani zina rangi hii. Vitamini A na C huweza kupatikana kwa wingi kwenye rangi hii. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimi katika kudhibiti mfumo mzima wa kinga mwilini. Upungufu wowote wa vitamini hivi viwili uanaweza kusababisha madhara makubwa mwilini.
4.rangi ya bluu na violet
Rangi hii hutambulisha uwepo wa anthocyanin ambayo ni antioxidat. Itambulike kuwa antioxidant zina uwezo mkubwa wa kupambana na sumu mbalimbali ndani ya mwili. Sumu hizi zinasababishwa ba vyakula tunavyokula kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivi vyenye rangi hii huwa vina vitamini C kwa kiasi kikubwa. Pia vyakula hivi vina kambakamba ambazo ni muhimu sana katika afya ya mtu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 web hosting π2 kitabu cha Simulizi π3 Kitabu cha Afya π4 Madrasa kiganjani π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Faida za kiafya za kula bamia
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula bamia
Soma Zaidi...Faida za kiafya za peaz/ peas
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi
Soma Zaidi...UPUNGUFU WA PROTINI NA FATI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Vyakula bora kwa ajili ya afya ya macho.
βMacho ni moja ya viungo muhimu zaidi vinavyokuunganisha na ulimwengu, lakini mara nyingi tunayasahau hadi pale tunapoanza kupata changamoto za kuona. Kama ilivyo viungo vingine, macho yanahitaji virutubisho maalum ili yasibadilike ubora kadiri umri unavyosonga mbele. Makala haya yanakupa orodha ya vyakula bora unayoweza kuingiza kwenye sahani yako leo ili kuimarisha uwezo wako wa kuona
Soma Zaidi...