UWANJA WA TEKNOLOJIA

Sehemu ya kwanza

.

NINI CHANZO CHA TATIZO LA KOMPYUTA AU SIMU YAKO?
Ni muda wingi tumekuwa tukisumbuliwa na kompyuta zetu kwa kuwa na matatizo mbalimbali ambayo maranyingi huwa yanatugharimu pesa ndefu kuyatatuwa.leo tatizo dogo tu la kompyuta litakugharimu pesa ndefu wakati ungeweza kulitatuwa mwenyewe ukiwa nyumbani.

Katika makala hii tutaangalia vyano vya haya matatizo katika kompyuta zetu hili litasaidia kuweza kujiepusha na matatizo haya. pia tutakuwa tukiangfalia namna ya kuweza kukabiliana na matatizo haya. kwa kawaida kompyuta zinakumbwa na matatizo mengi tuu lakini katika makala hii tutaona tuu yale matatizo yaliyozoeleka. kwa fano wa matatizo hayo ni kama haya;-
1. KOMPYUTA AU SIMU KUWA SLOW
2. KOMPYUTA AU SIMU KUSTAK
3.KOTOWEZA KUFUNGUWA BAADHI YA MAFAILI
4.KUTOWEZA KUCHEZA BAADHI YA GEMU
5.KOTOKUTOWA RANGI NZURI
6.KUSHINDWA KUUNGANISHA WIRELESS NETWORK {WI-FI}
7.KUTOWEZA KUSOMA USB
8.KUTOWEZA KUKONECT NA BLUETOOTH
9.DATA KUPOTEA AU KULIWA
10.KUZIMZAZIMA YENYEWE.

Yapo mengine meengi ambayo pia tutayaona tunapokuwa tunaangalia tatizo moja baada ya jingine.mengi katika mmatatizo haya huwa yanashirikiana sababu za kutokea kwake japokuwa zinatofautiana kwa kiwangogani tatizo limefikia . sasa hebu tuone tatizo moja badala ya lingine na tuine vipi tutaweza kulitatuwa mwenyewe ukiwa nyumbani bila ya kukupotezea pesa za kwenda kwa fundi;-

1.KOMPYUTA AU SIMU KUWA SLOW
tatizo hili linaonekana pale kompyuta yako ina[pokuwa slow yaani inafanya kazi kwa utaratiibu sana yaani haina kasi. Tatizo hili hutokea kwa mfano pale unapoiwasha inatumia muda mwingi sana kuwaka, au unapoizima inatumia muda mwingi katika kuzima. Ila mbaya zaidi ni pale unapoikomand kufanya kitu kisha inakuwa ipo slow. unaweza ukafunguwa program lakini unasubiri uda mwingi kuingoja kompyuta imalize kuload. mfano mzuli ni pale unapofunguwa microsoft office kisha inaload kwa muda wa dakika ndo ifunguwe faili. Tatizo hili linapoteza muda mwingi kwa mtumiaji wa kompyuta hasa pale anapotaka kufanya kazi zake kwa uharaka zaidi.Ssa hebu tuone chanzo cha tatizo hili

CHANZO CHA TATIZO HILI
tatizo hili limenukuliwa na wataalamu mbalimbali na wakaonesha baadhi ya vyanzo vya tatizo hili. Kwa mfano Natasha Stokes mnamo June 03, 2016 katika tovuti yao http://www.techlicious.com/tip/reasons-why-your-computer-is-slow/ wametowa sababu 13 za tatizo hili kama nitakavyo vitaja hapo chini;-

1. VIRUSI
Hapa tunajumuisha virusi, malware, spyware na trojan hizi zote ni software ambazo zimetengenezwa zikiwa na madhara kwa kompyuta yako. Kwakuwa zinalazimisha kukupatia advertizeent, au zinajaribu kuhack compyuta yako au kuathiri mafaili ndani ya kompyuta yako. Haya yote yanasababisha kompyuta kuwa bize hivyo kushindwa kufanya kazi zake kwa uzuli. VIRUS, TROJAN, MALWARE na SPYWARE vyote hivi tummezoea kuviita VIRUSI ila ni kuwa japo kazi zao ni moja kuathiri kompyuta yako lakini vipo tofauti. katika makala zijazo tutakuj kuona utofauti wao MUNGU akitaka.

jinsi ya kulitatuwa njia pekee na ya uhakika ni kuwa na antvirusi iliyoactive na iliyo update. kama huna zipo za free kwa mfano avast au microsoft esential security au window defenda. Tokeo la picha la window defender

vitu vya kuzingatia;-
1. hakikisha unaskan kompyuta yote full scanning
2. hakikisha antvirus yako ipo update
3. ristat kompyuta yako baaya ya kuskan
ITAENDELEA.........         › WhatsApp ‹ Whatsapp