Navigation Menu



image

TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO

TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO

Sayansi na Teknolojia

Teknolojia ya mawasiliano

TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO


YALIYOMO

1. NJIA ZA KUTAMBUWA VIRUSI KATIKA KIFAA CHAKO
2. SIMU KUSUMBUWA MTANDAO NINI SABABU
---i8ouj 3. NINI MAANA YA LEGACY CONTACT KATIKA FACEBOOK
4. JE NITUMIE SIMU YANGU WAKATI INACHAJI
5. KIPI KINGINE UTAFANYA UKIWA FACEBOOK
6. KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
7. EPUKA VIRUSI NA MALWARE UKIWA MTANDAONI
8. UTUNZAJI WA BETRY YA KIFAA CHAKO:
9. KAMA SIMU YAKO AU KOMPYUTA INASTAK (UNRESONDING)
10MWISHO



NJIA ZA KUTAMBUWA VIRUSI KATIKA KIFAA CHAKO
1.Kifaa chako kutokuwa na kasi katika ufanyaji kazi (slow); Hapa inaweza ikatokea unabonyeza batani lakini inachelewa kufanya kazi. Wakati mwengine unaweza ukabonyeza batani ya kuangalia meseji lakini ikachelewa kufunguka mpaka unasubiria kwa muda kidogo.


Ijapokuwa tatizo la kifaa chako kuwa slow linaweza kusababishwa na mabo mengine kama vile RAM, kuwepo kwa Spyware, na kujaa kwa hard disk, lakini kuwepo kwa virusi huwa ni chanzo kikubwa kama RAM na Hard disk ikawa safi yaani ikawa na uwezo wa kutoshelezea mahitaji yako.


kuweza kutatuwa tatizo hili tulisha eleza katika baadhi ya post zetu, ila kwa ufupi hakikisha kifaa chako kina nafasi ya kutosha katika memory yake au hard disk. Hkikisha mstari mwekundu wa kuonesha kuwa memory au Hard disk imejaa haupo, Hakikisha kompyuta yako ina RAM ya kutosha kwa mahitaji ya kifaa chako. Skann virusi kwa kutumia ant virus iliyo madhubuti\ na iliyo up to date.


2. Kuchelewa kufunguwa internet, Hapa huwa kifaa chako unapofunguwa intanet kinachelewa kuload. inatokeaa unabonyeza batani ya kusearch lakini unasubiria muda mrefu. Unapokuwa unadownload kifaa chako kinachelewa sana kudawnload. Kwa ufupi intanet kuwa slow husababishwa na kuwepo kwa virusi kwenye kifaa chako.


Ijapokuwa zipo sababu zingine zinazosababisha kifaa chako kuwa slow kwenye intanet kama vile netwprk kuwa kidogo. HIvyo kabla haujajiridhisha kuwa kifaa chako kina virusi kwanza hakikisha kuwa unamtandao wa kutosha kwenye kifaa chako. Pia hakikisha umeruhusu 3G au 4G katika kifaa chako. Kama itakuwa bado slow anza taratibu za kuondowa virusi katika kifaa chko.


3. Program kujifunguwa zenyewe; Hapa inatokeya baadhi ya program katika kifaa chako ziajifunguwa zenyewe bila ya kuruhusiwa. Hiki ni kiashiria kimojawapo cha kuwepo kwa virusi katika kifaa chako. Jambo la kufanya hapa ondowa proram hizo zinzojifunguwa zenyewe kisha skan viruri katika kifaa chako.


Tatizo la kuwa na virusi katika vifaa vya kielectronoc ni lakawaida, na ni vigumu kuliepuka kabisa. Jambo la kufanya ki kuwa na utaratibi wa kutazama kifaa chako kila wakati kama kuna athari yoyote. kuwa na utaratibu wa kuskani kifaa chako. Au ruhusu auto scan. yaani kifaa chako kiwe kinajiskani chenyewe kulingana na muda utakaotaka. Jambo la kuzingatia zaidi hapa ni kuhakiisha ant virusi uliyo nayo ipo vizuri kwa kufanya kazi hii.









SIMU KUSUMBUWA MTANDAO NINI SABABU
Kuna mambo mengi sana ambayo yanachangia simu yako kutokuwa na mtandao mzuri yaani network kuwa ndogo. Mambo haya ni pamoja na:-
1. Umbali kutoka kwenye mnara
2. Hali ya hewa
3. Uwezo mdogo wa simu, ama simu kuwa mbovu
4. Vitu vinavyo kuzunguka na sehemu ulipo kama mabondeni, kwenye shimo, kwenye msitu mnene n.k
5. Kubadilika kwa mnara.
Kuna mambo mawili hapa nitaongezea. Hutokea wakati mwingine upo sehemu nzuri, na karibu na mnara na simu yako ni nzima, lakini mtandao unasumbuwa. Hapa kuna mambo mawili unatakiwa uyajue kama:-
1. Kubadilika kwa mnara. Unapotoka sehemu moja kwenda nyingine kwenye mnara mwingine, simu yako itabadilisha mnara kutoka ule wa mwanzo na kutumia wa pili. Hivyo basi njia sahihi hapa ni ku restart au reboot simu yako. Ama izime kisha iwashe tena.
2. Pia wakati mwingine huwenda simu yako ina app (program) nyingi ambazo zinatumia network kwa mfano ukiwasha data na ukiwa na application nyingi ambazo zinatumia data kwa kuonyesha matangazo, pic, sms n.k hili huweza kufanya network ya simu yako kuwa ndogo ama dhaifu.
Kwa maelezo zaidi ya makala hizi za sayansi na teknolojia usiwache kutembelea tovuti yetu, bofya hapo chini



NINI MAANA YA LEGACY CONTACT KATIKA FACEBOOK?
Facebook hawana mpango wa kufunga akaunti ambazo hazijatumiwa kwa muda mrefu, haijalishi akaunti ni ya marehemu ama yupo hai. Kama hutaki akaunti yako ya facebook kuna njia moja tu nayo ni kuifuta. Hata hivyo mchakato huu inachukuwa kuanzia siku 114 yaani siku 14 za akaunti kuwa haipo active na aiku 90 za kuthibitisha kufuta akaunti hii.


Kwa waliofariki akaunti zao zitabakia milele ama mpaka facebook wakibadili sera ya kutofunga akaunti zilizotumika. Wakati mwingine akaunti za waliofariki zinatumiwa vibaya, hivyo unaweza kuchagua nini kifanyike utakapo fariki, aidha akaunti yako ifungwe ama ibakie kama ya kumbukumbu.


Kufanya haya yote mawili unatakiwa umchague mtu atakayefanya haya. Na mtu huyu itamchagua ukiwa hai. Mtu huyu anatambulika kama LEGACY CONTACT. Legacy contact ni friend kwenye akaunti yako ya facebook ambaye imemchagua kuwa ndiye utampa madaraka ya kuweza kuomba akaunti yako ya facebook ifungwe pindi utakapo fariki, ama akaunti yako iwe ni akaunti ya kumbukumbu yaani memorization account.


Mtu huyu hataweza kulog in kwenye akaunti yako. Yaani hataweza kuona taarifa zako za siri hata moja. Yeye atakuwa na madaraka kama:
1.Kuomba akaunti yako ifungwe ama iwe ya kumbukumbu
2. Kubadili profile picture ama profile cover picture.
3.Kukubali friends request chache kutoka katika watu wa familia
4.kuzuia ni picha zipi ziweze kuonea na ni nani aweze kuziona
5.kuzuia watu wasidownload picha zako ana kama utamruhusu kupitia legacy ataweza kudownload yeye tu.
6.kuondoa tag kama kuna mtu amekutag


Memorization account
Kama legacy wako ameomba akaunti yako isifungwe bali iwe memorization account basi itakuwa na sifa hizi
1. Haitaonekana kwenye ukurasa mkuu wa facebook
2.hata mtu akisach nina halitakuwa
3.waliokuwa friend ndio watakaoweza kuona akaunti tu.
4.Ni akaunti kwa ajili ya kumbukumbu kwa ndugu na jamaa
5. Facebook wataweza lebo karibu na profile picture kuonyesha kuwa huyu amefariki
6. Hautaweza kutumiwa meseji akaunti hii
Ukitaka kujua namna ya kumchagua mtu huyu atakayekuwa na mamlaka ya kufunga akaunti yako ama kuihamisha iwe ya kumbukumbu, angalia video kwenye link hapo chini
https://youtu.be/NKN41RXYNcg





JE NITUMIE SIMU YANGU WAKATI INACHAJI???
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza swali hili. Pia kutokana na baadhi ya video vilizoeneaga wakati fulani kuwa mtu alilipuliwa na simu yake kwa sababu alitumia ikiwa INACHAJI.


Ukweli ni kwamba kutumia simu wakati inachaji hakuwezi kuifanya iripuke hata kidogo, napia hakuwezi kuuwa betri yako. Mainjinia wa vifaa vya umeme wanatueleza kuwa katika simu kuna kifaa ambacho kinaundwa kama simu umesha jaa na kuizuia isichaji tena, hivyo hakuna madhara ya kuchaji simu hata kwa masaa 10.


Jambo la kuzingatia ni joto la betri yako. Wakati unapotumia kifaa chako hakikisha joto la simu yako halipandi kuwa la juu sana. Kwani hili joto ni hatari sana kwa maisha ya betri yako.


Ni vyema kama unatumia simu yako aidha ikiwa chaji au haipo chaji pindi joto la betri yako likipanda uipumzishe. Pia hakuna madhara ya kuilaza simu yako kwenye chaji.




KIPI KINGINE UTAFANYA UKIWA FACEBOOK
Facebook ni mtandao wa kwanza wa kijamii (social media) unaotembelewa na watu wengi. Mitandao mingine ni kama twitter, linkedin, youtube, whatsApp, instagram na mingine mingi. Facebook imeanzishwa huko marekani, na imekuwa ikiongeza nguvu kila kukicha na kuboresha huduma zake zaidi kila siku. Leo facebook imekuwa ni kituo cha kufanya mengi zaidi ya mtumiaji wa kawaida anavyotambua. Katika makala hii nitakueleza matumizi mengine ya facebook ambayo watu wengi hawayajui.


Mtumiaji wa kawaida wa facebook amezoea kulogin na kuchat kwa sms, kushare picha, maoni, video na masimuliz, kupiga simu ya sauti yu ama video. Pia hutumika facebook kwa kuhifadhi taarifa binafsi pamoja na kuupdate wasifu wako. Hebu tuone baadhi ya matumizi mengine unayoweza kuyafanya ukiwa facebook


1.Kutangaza biashara na wasifu wako. Facebook ni njia ya haraka kwa anayetaka kutangaza wasifu wake, biashara yake ama kampuni. Ukiwa marafiki, na watu wengi wanaokufuata unaweza kuitumia nafasi hii kwa ajili ya kutangaza kile unachokitaka watu wakijue.
2.Unaweza kutumia facebook kama kituo cha kukupatia kipato. Wapo watu wengi leo wanajiingizia kipato kwa kutumia facebook, kwa mfano watu wanaomiliki kurasa za video wanaweka matangazo ya watu na kujiingizia kipato. Pia unaweza kutumia fursa hii ya facebook kutangaza biashara yako na kupata wateja. Sambamba na haya unaweza kujiingizia kipato kwa kutumia makala unazoandika kwenye ukurasa wako unaoumiliki.
3.Unaweza kufanya mikutano ya siri, watu maalumu ama ya hadhara, inaweza kuwa kwa kutumia video ama kwa sauti tu. Halikadhalika pia mikutano hii inaweza kuwa ya njia ya maandishi kama mkipenda pia.
4.Pia unaweza kucheza gemu ukiwa facebook. Huna haja ya kudownload gemu, ukiwa na simu ya smartphone
5.Kukusanya taarifa kuhusu mtu, watu, kikundi ama kampuni. Taarifa hizi zinaweza kuwa: namba ya simu, barua pepe (email), familia, sehemu, marafiki, vitu anavyopenda, mawazo yake kuhusu siasa, dini ama jamii, tabia yake na vitu anavyochukia. Pia unaweza kupata taarifa za mtu kuhusu vitabu anavyosoma, watu anaowafuata, video ama miziki anayotazama na kusikiliza, tarehe ya kuzaliwa na anapofanya kazi ama shule alizosoma, sambamba na kiwango cha elimu yake. Miongoni mwa taarifa hizi watu wengi wanadangaya ukweli wa mambo hususani majina na tarehe ya kuzaliwa.





KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Akaunti kuhakiwa inamaana kuna mtu amelogin kwenye akaunti yako bila ya ruhusa yako ama bila ya kumpatia neno la siri. Facebook imeweka njia kadhaa kuhakikisha kuwa akaunti za watu zipo salama muda wowote.


Two-factor authentication ni katika njia mujarabu ambazo facebook wameweka ili kulinda akaunti za watumiaji wake. Kwa kutumia njia hii hata kama mtu anaijuwa password yako (neno la siri) hataweza kuingia kwenye akaunti yako ya facebook mpaka awe na laini yako ambayo namba yeke umeisajili facebook.


Njia hii inaongeza tabaka lingine la usalama wa akaunti yako ya facebook. Baada ya kuingiza neno la siri kwenye akaunti yako ya facebook, facebook watakutumia code (namba sita) kwenye laini yako ulioisajili facebook. Namba hizo utaziingiza kwenye kibox na ndipo utaruhusiwa kuingia kwenye akaunti.


Kuanza kutumia njia hii ingia kwenye setting, kisha security and login kisha Two-Factor Authentication. Utatakiwa kuingiza namba ya simu na maelekezo machache yatafuata. Utalogout kisha utalogin tena ili kuthibitisha huduma kama ipo tayari.


Njia hii itasaidia sana kwa wale ambao tayari password zao kuna watu wanazifahamu. Hata kama mtu anaijua password TROJAN) yako katu hataweza kuingia kwenye akaunti yako mpaka awe na laini yako. Karibia mitandao mingi inatumia njia hii ikiwemo google, linkedin, github na mingine mingi.


EPUKA VIRUSI NA MALWARE UKIWA MTANDAONI
Malware ni neno pana na watu wengi si wenye kulitumia. Malware hukusanya maana za virusi, trojan, spyware na worm. Watu wengi wamezoea kutumia neno virusi. Utasikia mtu anasema kuwa simu yake ina virusi. Kwahiyo virusi ni sehemu ndogo sana ya malware.


Mara nyingi virusi hawawezi kuharibu mafaili kwenye kifaa chako ila huathiri utendaji wa kazi wa kifaa chako. Virusi huweza kujizalisha wenyewe kwa wenyewe ndani ya kifaa chako. Worm wanaweza kutembea kutoka faili moja mpaka jingine. Kuna tofauti kubwa kati ya virusi, worm na trojan.


Malware ni program ama software ama code zinazoingizwa kwenye kifaa chako kama simu ama kompyuta, na kuunganisha kifaashako na mitandao ya watu au kuharibu taarifa (data) za kwenye kifaa chako. Malwarei huweza kuingia kwenye kifaa chako kwa kupitia:
1.Waya wa USB
2.Flash
3.Ukiwa mtandaoni kwa kudownload mafaili, kufungua email (barua pepe)
4.Bluetooth
5.Kushea mafaili kwa njia nyinginezo.


Malware huondolewa kwenye kifaa chako kwa kutumia program za kuondoa malware zijulikanazo kama antivirus. Kuna program (software) nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi hui ya kuondoa malware ikiwemo virusi. Program hizo ni pamoja na avast, kerspersky, avag, window defender na nyinginezo nyingi. Pia kwa watumiaji wa simu google playstore inafanya kazi hiyo bure kwa kuscan App zote ulizoziinstall.


Njia za kujilinda na malware
1.Weka antivirus kwenye kifaa chako.
2.Hakikisha unascan kifaa chako mara kwa mara
3.Scan waya wa USB
4.Kuwa makini unapotuckuwa mafaili kwa kutumia bluetooth ama njia nyingine. Vi vyema ukascan mafaili hayo
5.Kuwa makini na kudownload kitu usichokijua, ama kufungua mafaili ama email usisozijua.
6.Kuwa makini na matangazo yanayotaka uclick eitha upate zawadi ama bonasi
7.Scan mafaili yote ulioyadownload.


UTUNZAJI WA BETRY YA KIFAA CHAKO:
Kabla ya kuona njia za kutunza betry ya kifaa chako kwanza tuone adui mkubwa ambaye anachangia kuharibu betry yako kwa kiwango kikubwa.
Jambo hatari sana linalosababisha kuharibika kwa bety hako ni kupata joto. Eric Limer alizungumza hivi "What's far more dangerous to a battery's well-being is heat. Lithium-ion batteries despise heat. A li-ion battery that's been exposed to temperatures of around 100 degrees Fahrenheit for a year will lose about 40 percent of its overall charge capacity. At 75 degrees, it'll lose only about 20 percent."


hivyo joto ni katika adui mkubwa wa betry yako ya simu au kompyuta. Betry ikiwa inapata joto jin gi wakati wa kutumika inaweza kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi kwa haraka zaidi na kwa kiwango kikubwa kama alivyosema katika nukuu za hapo juu kuwa betry iliyowekwa katika joto la 100 Fahrennheit kwa mwaka inapoteza asilimia 40% za uwezo wake wa kijumla wa kuchaji, na likiwa joto hilo ni 75% inapoteza 20% ya uwezo wake wa kuchaji. hivyo kama utaizuia betry yako kupata joto jingi kwa muda mrefu unapofanya kazi utaweza kudhibiti uwezo wa betry yako wa kufanya kazi. Sasa kwakuwa tumeshaona adui mkubwa wa betry zetu hebu tuone sasa namna ya kutunza betry zetu.


Njia za kutunza betry
1. Towa betry yako katika kifaa chako ili ipowe kama imepata moto kwa muda mrefu bila ya kupozwa. simu au laptop zingine huwa zikipata joto huchelewa kupowa hivyo kitendo hiki kitafanya betry yako iendelee kuathirika. hivyo kamma utakuwa umemaliza shughuli zako unaweza kuitowa nje betry yako ili iweze kupowa.


2.weka kifaa chako katika mazingira yasiyo na joto la hali ya juu. kwa mfano usiweke simu yako juu ya PS ambapo pana joto au juu ya laptop au kompyuta iliyo na joto. pia jiepushe kuiweka simu yako juu ya deki iliyo na joto. Halikadhalika kwa betry ya laptop yako epusha kuiweka katika mazingira nambayo yataifanya ipate joto la juu kwa mfano kuiweka juu ya godoro au kitu ambacho itasababisha joto la kompyuta yako lisipungue kwani godoro linaweza kuziba matundu ambayo yamewekwa kwa ajili ya kupunguza joto la ziada.


3.Hifadhi betry yako ikiwa ina chaji kiasi walau kidogo.Inatokea unazaidi ya betri oja na unataka kuipunzisha betry ya zamani hivyo inashauriwa kuihifadhi ikiwa ina kiasi cha chaji. pia nivizuri kuiwacha betry katika kifaa chako ikiwa ina kiasi cha chaji walau kidogo.


Mengineyo katika kutunza bety:
Tokeo la picha la wifi1.funga wi-fi kama hautumii. wireless ni katika vyanzo ambavyo pindi ikiwa ON na ipo connected inaweza kutumia chaji nyingi sana kwa wakati mfupi ambapo kitendo hiki pia kianaweza kuhatarisha uhai wa betry yako.


2. funga bluetooth na funguza mwanga wa screen yako na punguza muda wa kudisplay screen yako


3.funga shughuli zote zinazofanyika kwa kufificha yaan background activities.
4. mwisho kama betry yako inaendelea kusumbuwa ni vizuri kwendakuibadilisha ni vizuri kununuwa mpya tofauti na kunu uwa kwa mtu. nenda dukani ukapate betry yako mpya uendelee kuvinvjari ukiwa na kifaa chako.







KAMA SIMU YAKO AU KOMPYUTA INASTAK (UNRESONDING)
Simu za smart phone ni simu ambazo hutumia fumo wa kikompyuta hivyo kuifanya iwe na uwezo wa kufanya baadhi ya kazi sawa na KOMPYUTA zingine. Kitendo hiki kinafanya ishirikiane na kompyuta zingine katika matatizo kwa mfano hili tatizo la "application is not responding" yaani kustak Tatizo hili hutokewa wakati simu yako inaposhindwa kufanya ulichoiagiza kama unapofunguwa baadhi ya application nzito kama GAMES.


Kuna sababu kadhaa zinadaiwa kuwa ndio chanzo cha tatizo hili ila nitataja moja katika zile alizozitaja Mr. Mehul Rajput ambayoni INCORRECT MEMORY & CPU USAGE.Kwa ujumla hapa kinachozungumziwa ni matatizo katika storage au memory ya simu yako pamoja na matatizo katika utendaji wa CPU ya simu yako. Hivy pindi simu yako ikianza tatizo hili huenda miongoni mwa sababu hizi zikawa ni moja wapo.


Jinsi ya kutatuwa tatizo hili:
zipo njia kadhaa abazo kitaalamu zinashauriwa kutuia kwa ajili ya kukabiliana na ratizo hili kama vile:-


1.Hakikisha memory yako katika simu ina nafasi ya kutosha. Ikumbukwe kuwa hapa tunazungumzia zaidi memory ya ndani ya simu INTERNAL MEMORY.unaweza ukafuta baadhi ya data au kuclean simu yako


2.Futa data katika application yako. Kama umefunguwa application kisha simu ikakuandikia epllication is not responding nenda kwenye setting za simu yako kisha storage kisha application kisha chaguwa applicatuin hiyo kisha itach kwa muda kisha katika menyu itayokuja chaguwa "CLEAN DATA" kisha maliza na ok.


3.Uninstall application zote ambazo hauzitumii hususan zile ambazo zinachukuwa nafasi kubwa katika memori yako. kwa maelezo namna ya ku uninstall


4.UPDATE application zako unaweza ukatumia playstore na kuapdate application zako.hili litasaidia kupunguza tatizo kani pindi application utakapoziapdate zitakuwa kama zimeingizwa upya.


5. Restart simu yako. Kurestart simu yako kutakufanya uendelee kuitumia simu yako kwa uzuri, kwani itakuwa imejirifresh.


6.RESTORE au fanya FACTORY RESET: kitendo hiki kinaweza kuifanya simu yako isirudie kukuletea tatizo hili kwa muda mrefu kidogo. Lakini kama tatizo ni sirias sana huenda isichukuwe muda kurejea.


7.Nenda ukaiflash simu yako kwenye kopyuter.Kama tatizo limeendelea jambo la mwisho la kukusaidia ni kuiflash simu yako kwa kutumia kompyuta. Sikuhisi wapo wanaodai wanaflash lakini wanatumia batan za simu yenyewe kwa kuirestore, japo kitendo hiki kinapunguza tatizo lakini sio sawa na kuiflash.





MWISHO
WASILIANA NASI KWA
TOVUTI: www.bongoclass.com
Email: admin@bongoclass.com
Simu: :+255675255927





Download kitabu hiki hapa






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Teknolojia Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 899


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Matumizi ya OCR katika simu yako
Somo Hili linakuleteq mafunzo ya OCR katika simu yako Soma Zaidi...

UTUNZAJI WA BETRY YA KIFAA CHAKO
Namna ya kutunza betri yako iweze kudumu kwa muda mrefu Soma Zaidi...

Jinsi ya kutoa pesa ClipClaps kwa Tanzania
Njia za kutoa pesa ClipClaps Soma Zaidi...

SIRI
Hii ni game ya maandishi bila ya kutumia vioneshi (graphics). Soma Zaidi...

yanayoathiri betri ya kifaa chako
makala hii itakuelezea mambo makuu ambayo ni hatari kwa usalama wa betri ya kifaa chako Soma Zaidi...

Kurudisha data zilizo potea
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Njia rahisi ya kudownload video YouTube
Posti hii inakwenda kukuelekeza kuhusu njia rahisi ya kudownload video YouTube Soma Zaidi...

Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

MUDA WA KUCHAJI SIMU YAKO AMA MUDA WA KUCHAJI BETRI YAKO
Wwatu wengi wamekuwa wakijiuliza ni muda gani hasa inapasa kuchaji simu, je nisubiri mpaka chaji iishe kabisa, ama nichaji ikiwa na asilimia ngap? Soma Zaidi...

Kujaa kwa memory au hard disc
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vitu vya kufanya endapo memory au hard disk itajaa Soma Zaidi...

Nini Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

EPUKA MALWARE (VIRUSI, WORM NA TROJAN UKIWA MTANDAONI)
Malware ni neno pana na watu wengi si wenye kulitumia. Soma Zaidi...