Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa
Elimu yenye Manufaa
Elimu yenye manufaa ni ile ambayo: Kwanza, humuwezesha mja kufikia lengo la kuumbwa kwake. Tumeona kuwa elimu imekuwa faradhi ya kwanza kwa waumini kwa kuwa elimu ndio nyenzo kuu ya kuwawezesha binaadamu kufikia lengo la kuumbwa kwao ambalo ni kumuabudu Allah (s.w), ipasavyo
katika kila kipengele cha maisha yao. (Qur-an 51:56). Pia elimu ndio nyenzo kuu ya kuwawezesha waumini kuwa viongozi wa jamii (makhalifa wa Allah) katika ardhi. (Qur-an 2:30 - 31).
Elimu itakayotafutwa kinyume na kumuwezesha mtu kumuabudu Mola wake ipasavyo na kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika ardhi itakuwa si elimu yenye manufaa bali elimu yenye kuhasirisha kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w)
amesema: “Anayetafuta elimu isiyokuwa kwa ajili ya
kutafuta radhi za Allah (s.w), hasomi kwa lengo lolote
lile ila la kupata maslahi ya hapa duniani tu. Huyo
siku ya kiyama hatapata hata harufu ya Pepo.”
(Ahmad, Abu Daud, Ibn Majah).
Pia Mtume (s.a.w) ametuasa kuwa mwenye kutafuta elimu ili awazidi wasomi wengine au ili kuitumia katika biashara za kijahili au ili kujionesha kwa watu kuwa naye ni msomi, Mwenyezi Mungu atamuingiza motoni. (Tirmidh).
Pili, elimu yenye manufaa kwa binaadamu hapa ulimwenguni na huko akhera ni ile ambayo pamoja na mtu binafsi kuitumia katika kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo katika maisha yake ya kila siku, huifundisha au huifikisha kwa wengine pia kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w).
Ni vibaya mno mbele ya Allah (s.w) mtu kukataa au kuacha kufikisha kwa wengine kila anachokijua kama tunavyojifunza katika hadithi ifu atayo:
“Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Atakayeulizwa juu ya jambo alilojifunza kisha akaficha (akakataa kutoa elimu ile) atavalishwa mshipi wa moto katika siku ya Kiyama”. (Ahmad, Ibn Majah, Tirmidh na Abu Daud).
Katika hadith nyingine iliyosimuliwa na Abu Hurairah Mtume (s.a.w) amesema:
“Mfano wa elimu isiyonufaisha ni sawa na mfano wa mali iliyokusanywa bila ya kutumiwa katika njia ya Allah ”. (Ahmad, Darini).
Kutokana na hadith hizi tunajifunza kuwa elimu yenye kunufaisha ni ile iliyofundishwa kwa wengine kinadharia na kiutendaji. Kwa kufundisha watu unachokijua bila ya wewe mwenyewe kutenda ni mfano mbaya mno kwa wale wanaofundisha na chukizo kubwa mno mbele ya Allah (s.a.w):
“Enyi mlioamini mbona mnasema msiyoyatenda?) Ni chukizo kubwa mbele ya Allah (s.w) kusema msiyoyatenda.” (61:2-3)
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na nini? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo)
Soma Zaidi...Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu Ni upi? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu)
Soma Zaidi...Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an.
Soma Zaidi...Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.
Soma Zaidi...Allah anatutaka kuchunguza umbile na mbingu na ardhi ili kupata mazingatio.
Soma Zaidi...Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...