.Dhana ya Imani katika Uislamu.
Maana ya Tawhiid.
- Ni fani inayohusiana na imani ya kuwepo Allah (s.w) na siku ya mwisho pamoja na vipengele vyote vya nguzo za imani.
- Ni kumpwekesha Allah (s.w) katika kila kitu kwa Upweke na Umoja wake na uweza wake juu ya kila kitu.
Matapo (makundi) ya Tawhiid.
- Tawhiid imegawanyika makundi makuu matatu:
1)Tawhiid – Rubbuubiyya: Ni Kumpwekesha Allah (s.w) katika Utawala wake.
2)Tawhiid – Asmaa Wassifaat: Kumpwekesha Allah katika Majina na Sifa zake.
3)Tawhiid – Ibaadah: Kumpwekesha Allah (s.w) katika Uungu na Kuabudiwa.

Maana ya imani kwa mujibu wa Qur’an (Uislamu).
- Ni kuwa na yakini moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana kwa macho bali kwa dalili zinazothibitisha kuwepo kwake.

Imani kwa mtazamo wa Uislamu na ule wa dini zingine:
- Katika Uislamu imani ni ile inayodhihirishwa katika vitendo vya mtu tofauti na dini zingine.
- Katika Uislamu imani juu ya kitu au jambo fulani lisiloonekana hutokana na dalili au ushahidi wa kuonesha uwepo wake tofauti na dini zingine.

Nguzo za Imani.
Nguzo za imani ya Kiislamu ni Sita:
1.Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w).
2.Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
3.Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).
4.Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).
5.Kuamini Siku ya Mwisho.
6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa kheri na shari vyote vinatokana kwake.
Rejea Qur’an (2:285), (4:136), (57:22) na (11:6).

Nguzo ya Ihsani.
- Nayo ni ‘kumuabudu Allah (s.w) kana kwamba unamuona na kama humuoni basi yeye anakuona’.
Nani muumini wa kweli? (Sifa za muumini wa kweli).
- Ni yule ambaye imani yake inathibitishwa katika matendo ya kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Rejea Qur’an (2:8-9).

- Ni yule anayejipamba na sifa za waumini zilizoainishwa katika Qur’an na Sunnah katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Rejea Qur’an (23:1-11), (25:63-77), (33:35-36), n.k.
- Ni yule anayeendea kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu wa vipengele vyote vya nguzo za imani ya Kiislamu.
oHawi muumini wa kweli kwa imani isiyoendana na matendo wala kwa kuamini baadhi ya nguzo za imani.