Hutuba ya ndoa wakati wa kuoa

Hutuba ya ndoa wakati wa kuoa

Khutuba ya Ndoa



Kabla ya kuozesha (kufungisha ndoa), ni Sunnah kwanza kuleta khutuba ya ndoa (mawaidha ya ndoa) kwa ufupi iii kuwakumbusha wanaooana na Waislamu wengine wachunge ahadi waliyoichukua mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa watakaa kwa wema katika maisha ya ndoa na ikibidi kuachana, wataachana kwa wema vile vile.


Ni vyema katika mawaidha haya kuwafahamisha hawa wenye kuoana na kuwakumbusha Waislamu wote waliohudhuria kuwa maisha ya ndoa yatakuwa ya furaha na upendo endapo kila mmoja, mume na mke, atajua wajibu wake kwa mwenziwe na akawajibika kwake ipasavyo. Ndoa iliyofanikishwa kulingana na ahadi ya ndoa ni msingi wa furaha, ushirikiano, utulivu na amani katika familia na jamii kwa ujumla. Ndoa pia imekusudiwa iwaokoe wenye kuoana na adui Shetani na iwasalimishe kwa Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa ujumla, katika khutuba hii, ni vyema umuhimu wa ndoa uelezwe kwa muhtasari.



Msisitizo wa Khutuba unaonekana katika hadithi zifuatazo:



Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema; Ndoa yoyote ambayo ndani yake hamna Tashahhud (Maamkizi ya Mwenyezi Mungu (s.w) ni kama kata isiyo na mkono. (Tirmidh).



Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Jambo lolote muhimu lililofanyika bila ya kumtukuza (Kumhimidi) Mwenyezi Mungu (s.w) kwa utukufu wake, limekosa baraka. (Ibn Majah).



Kutckana na hadithi ilisimuliwa naAbdullah bin Mas'ud (r.a), Mtume (s.a.w) amelΓΌndisha tashahud mbili, ya kwanza ni ile ya swala (Tahiyyatu) na ya li ni ile inayopalikana katika khutuba ya kukidhiwa haja, kama vile khutuba ya ndoa, ambayo inaanza na kuendelea kama iluatavyo:


Sfa zote anastahiki Mwenyezi Mungu (s.w). tunamtukuza kwa Utukufu wake, Tunataka msaada wake, na msamaha Wake, na tunajikinga kwake na shari ya nafsi zenu na shari ya vitendo vyetu viovu. Ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, hakuna awezaye kumpoteza, na ambaye amempoteza hatakuwa na wa kumwongoa. Na ninashuhudia kuwa hapana mola ila Mwenyezi Mungu (s.w), na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtumwa wake na Mjumbe Wake.


Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha wala msfe ispokuwa mmekwisha kuwa Waislamu kamili. (3:102).


Enyi Watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka wawili hao. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana.Na (muwatazame) jamaa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mlinzi juu yenu. (4:1).


Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya Haki Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na Atakusameheni madhambi yenu; Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila shaka amefuzu kufuzu kukubwa. (33:70-71).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 2498

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

DARSA ZA TAWHID

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
swala za tahiyatu al masjid, qabliya na baadiya

Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid.

Soma Zaidi...
SHIRK

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH

Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila.

Soma Zaidi...