image

Swala ya kupatwa kwa jua na mwezi na namna ya kuiswali

11.

Swala ya kupatwa kwa jua na mwezi na namna ya kuiswali

11. Swala ya Kupatwa kwa Jua na Mwezi



Swala ya kupatwa kwa mwezi au jua ni sunnah iliyokokotezwa ambayo huswaliwa katika jamaa. Jua au mwezi unapopatwa Waislamu wanatakiwa waitane na kuswali swala ya Suunah ya kupatwa jua au mwezi kama alivyokuwa akifanya Mtume wa Allah:



Aisha (r.a) ameeleza kuwa jua lilitokea kupatwa wakati wa Mtume (s.a.w). Alisimama kuswali na alirefusha kisimamo (kiasi cha kumaliza kusoma Suratul-Baqara). Kisha alirukuu na kurefusha sana rukuu yake. Kisha aliinuka kutoka kwenye rukuu na akarefusha kisimamo lakini kilipungua kidogo kuliko kile cha kwanza. Kisha alirukuu tena na kurefusha rukuu lakini kupungua kidogo kuliko ile rukuu ya kw anza. Kisha alisujudu na kisha akasimama tena lakini kwa kitambo kilichopungua kidogo kuliko kisimamo kilichotangulia. Kisha alirukuu tena kw a kitam bo kilichopungua kidogo kuliko kile cha rukuu iliyotangulia. Kisha aliinuka kutoka kw enye rukuu na kurefusha kisimamo lakini kupungua kidogo kisimamo kilichotangulia. Kisha alirukuu tena na kurefusha rukuu yake lakini kupungua kidogo kuliko ile iliyotangulia. Kisha alis ujudu. Kisha ligeuka (aligeukia watu) na wakati huo jua lilikwisha kuwa jeupe na akawahutubia watu. Alimshukuru (alimhimidi) Allah na akasema: Jua na mwezi ni alama mbili za Allah (s.w). Havipatwi kutokana na kifo cha mtu yeyote, wala kutokana na kuzaliwa kwa mtu yeyote. Enyi Ummah wa Muhammad, hapana yeyote mwenye kupata ghadhabu kuliko Allah anavyomghadhibikia mja wake pindi anapozini. Enyi watu wa Muhammad, naapa kwa Allah kuwa kama mngelikuwa mnajua, mngelicheka kidogo na kulia sana ”. (Muslim)



Kutokana na Hadithi hii tunaona kuwa swala ya kupatwa jua na mwezi ina visimamo (au visomo) vinne, rukuu nne na sijda nne. Visimamo na rukuu hutofautiana urefu kama ilivyo oneshwa katika Hadithi.Imamu Shafii na Maimamu wengine wanashikilia kuwa swala ya kupatwa jua na mwezi haina budi kuswaliwa katika muundo huu ulioelezwa katika hadithi hii. Lakini Imamu Abu Daud, anashikilia kuwa swala ya kupatwa kwa jua na mwezi iswaliwe kama swala ya kawaida kwani kutokana na hadithi hiyo Mtume (s.a.w) aliwahi pia kuswali swala hiyo kwa kufuatia muundo wa swala za kawaida.


Kwa ujumla wanachuoni wengi wanasisisitiza kuwa pamoja na kwamba swala ya kupatwa kwa jua na mwezi inaweza kuswaliwa kwa kufuata muundo wa kawaida wa swala, ni vizuri zaidi kama swala hiyo itaswaliwa kwa kufuata muundo ulioelezwa katika Hadithi hii wa kuwa na visimamo (visomo) vinne, rukuu nne na sijda nne.



Lengo la swala hii ni kumkumbuka Allah(s.w) kwa kuzingatia alama zake. Hivyo ni vyema Imamu baada ya swala awawaidhi Waislamu kuwakumbusha wajibu wao kwa Allah(s.w) na kuwakumbusha marejeo yao ya akhera. Hivyo swala ya kupatwa jua (Swalatul-Kusuf) au swala ya kupatwa mwezi (swalatul-Khusuf) hufuatiwa na khutuba mbili kama ilivyo katika khutuba ya Idd. Katika swala hizi Imamu atasoma kwa sauti.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 650


Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI
Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...

Hutuba ya ndoa wakati wa kuoa
Soma Zaidi...

Muda wa kuhiji na mwenendo wa mwenye kuhiji
Soma Zaidi...

TAFSIRI (TARJIMA) YA QURAN KWA LUGHA YA KISWAHILI
Tafsiri ya Quran kwa iswahili iliyotafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-BArwani Soma Zaidi...

kusai yaani kukimbia kati ya mlima swafa na marwa mara saba
4. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...

Uthibitisho Kuwa Qur’an ni Neno la Mwenyezi Mungu (s.w)
Soma Zaidi...

NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA
Soma Zaidi...

Taratibu za kumuona mchumba
Soma Zaidi...

Kuamini qadar na qudra katika uislamu
Kuamini Qadar ya Allah (s. Soma Zaidi...

mgawanyiko katika quran
MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani. Soma Zaidi...

Zijuwe suna (sunnah) za Udhu ama Kutawadha
Soma Zaidi...