image

Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu, sifazao na lengo la kuletwa kwao

1.

Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu, sifazao na lengo la kuletwa kwao

Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu, sifazao na lengo la kuletwa kwao

1.1. Kuamini Mitume wa Allah (s.w)

Uwepo wa Mitume wa Allah (s.w)

- Mitume ni wanaadamu wanaume walioteuliwa na Allah (s.w) kwa ajili ya kuufikisha ujumbe wake kwa wanaadamu wote.


- Mitume waliotajwa ndani ya Qur’an ni 25 ambapo ni wajibu kwa kila muumini wa Kiislamu kuamini uwepo wao na mafundisho yao kutoka kwa Allah (s.w). Rejea Qur’an (2:136), (2:285) na (4:150-152).


- Kila Mtume alifundisha mwongozo sahihi wa Allah (s.w) na kuwaongoza watu wake mfumo na njia sahihi ya maisha.




Umuhimu wa Kuamini Mitume wa Allah (s.w)

(i) Kuamini Mitume wa Allah (s.w) ni amri ya Allah (s.w)

Rejea Qur’an (4:150-152)



(ii) Kuamini Mitume wa Allah (s.w) ni nguzo ya nne ya imani ya Kiislamu.



(iii) Kuamini Mitume wa Allah (s.w) ni miongoni mwa sababu za kunusurika muumini na adhabu ya Allah hapa duniani na Akhera pia.


(iv) Kutoamini Mitume wa Allah (s.w) au Kuamini baadhi na kukufuru baadhi yao ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.
Rejea Qur’an (4:150-152).



Sifa na Lengo la Kuletwa Mitume.

Sifa za Mitume wa Allah (s.w).

i. Ni watu waliozaliwa, walioa, walikula, waliugua, walikufa, n.k. kama binaadamu wa kawaida isipokuwa Nabii Adamu (a.s).
ii. Walikuwa na kila tabia njema, wakweli, waaminifu na wenye huruma.

iii. Walikuwa na upeo wa Elimu wa hali ya juu kuliko watu wote enzi zao kwa sababu kuletewa kwao wahayi.
iv. Walikuwa Wacha-Mungu wa hali ya juu kuliko watu wote.



Lengo la kuletwa Mitume wa Allah (s.w).

i. Kusimamisha Uislamu (haki na uadilifu) katika maisha ya jamii zao.

Rejea Qur’an (57:25), (9:33), (61:9), (48:28), n.k.

ii. Kufundisha na kutekeleza mafundisho ya ujumbe (wahyi) waliokuja nao kutoka kwa Allah (s.w).
iii. Kuwa mifano bora ya kuigwa katika kuiongoza jamii katika mfumo sahihi wa maisha.
Rejea Qur’an (33:21).

iv. Kuitoa jamii katika giza la ujahili, upotofu na kila aina ya dhuluma na kuipeleka katika nuru, haki, uadilifu na usawa.
Rejea Qur’an (2:256)



Haja au sababu ya kuja Mtume mwingine baada ya Mtume aliyetangulia kuondoka
i. Iwapo mafundisho ya Mtume aliyetangulia yamepotoshwa na kupoteza ukweli na asili yake.
ii. Iwapo mafundisho ya Mtume aliyetangulia hayakukamilika katika kutosheleza mahitaji ya kibinaadamu ya kibinafsi na kijamii kulingana na wakati huo.
iii. Iwapo Mtume aliyetangulia alipelekwa kwa watu (taifa) fulani tu, hivyo inabidi



Mtume mwingine apelekwe taifa jingine.

Hapana haja ya kuja Mtume mwingine baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)

kwa sababu zifuatazo;

i. Mafundisho ya Qur’an (Uislamu) yameepukana (yamehifadhiwa) na upotofu na

uharibifu wowote tangu wakati wa Mtume (s.a.w) hadi siku ya Qiyama.

Rejea Qur’an (15:9), (41:42)



ii. Pia mafundisho ya Mtume (s.a.w) na mwenendo wake yamehifadhiwa katika

Hadith sahihi.



iii. Mtume Muhammad (s.a.w) ameletwa kwa walimwengu wote kwa zama zilizobaki mpaka kufika siku ya Qiyama.


iv. Ujumbe wa Qur’an (Uislamu) umekamilika na kukidhi mahitaji yote ya

wanaadamu kibinafsi na kijamii.

Rejea Qur’an (5:3)





Ujumbe wa Uislamu umekamilika na haupitwi na wakati kwa sababu zifuatazo;

- Mafunzo ya Uislamu ni ya milele kutoka kwa Allah (s.w) aliye Mjuzi wa yote yaliyopita, yaliyopo na yajayo.
- Mafundisho ya Uislamu yanaendana sambamba na umbile la mwanaadamu kwa zama zote zilizobaki.
- Qur’an na Sunnah zimeweka sheria na kanuni za kudumu zinazoweza

kutekelezeka zama zote za maisha ya mwanaadamu.



Mitume wa uongo

o Aswad Aus

- Alikuwa wakati wa Mtume (s.a.w) na aliuliwa kwa amri ya Mtume (s.a.w).



Msailama – Al-Kadh-dhaab

- Alijitangaza wakati wa Ukhalifa wa Abubakar (r.a) na aliuliwa katika mapigano ya vita vya Yamamah.


Bahsullah

- Alijitokeza huko Iran karne ya 19 A.D na aliuliwa na waislamu.



Mirza Gulam Ahmed

- Alijitokeza India, mji wa Kadian karne ya 20 A.D na alilindwa na serikali ya

Uingereza na kuanzisha dini mpya.



Maana ya Kuamini Mitume wa Allah (s.w) katika maisha ya kila siku

i. Ni kuwati kwa kufuata maamrisho na kuacha makatazo yao katika kuendea kila kipengele cha maisha ya kibinafsi, kifamilia na kijamii.
Rejea Qur’an (3:31-32), (59:7), (4:59), n.k



ii. Ni kuwaiga mienendo na tabia zao katika maisha ya kibinafsi, kifamilia na kijamii.
Rejea Qur’an (33:21)



iii. Ni kuwapenda Mitume kuliko hata nafsi zetu.

Rejea Qur’an (9:24)



iv. Ni kuwafanya Mitume kuwa Mahakimu wetu juu ya jambo lolote tunapohitilifiana.
Rejea Qur’an (4:65), (33:36)



v. Ni kuyakinisha kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) ndiye Mtume wa mwisho.

Rejea Qur’an (33:40)



vi. Ni kumswalia Mtume Muhammad (s.a.w) mara kwa mara na kila anapotajwa.

Rejea Qur’an (33:56)



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 904


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-