Navigation Menu



image

Makundi ya dini zilizotajwa kwenye quran na athari zake katika jamii

2.

Makumndi ya dini zilizotajwa kwenye quran na athari zake katika jamii

2. MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA DINI

2.1. Makundi makuu ya Dini yaliyotajwa katika Qur’an

Makundi makuu ya dini

a) Dini ya Allah (s.w), ambayo ni Uislamu.

b) Dini zilizoundwa na wanaadamu, ambazo zimegawanyika makundi yafuatayo;

i. Dini yak Ukafiri

ii. Dini yak Ushirikina iii. Dini yak Utawa




2.2. Tofauti kati yak Uislamu na Dini zingine

- Tofauti yak dini hizi ziko katika sehemu kuu mbili; a) Itikadi na madhara yak dini za wanaadamu b) Ubora na Matunda yak Dini yak Uislamu


a) Itikadi na madhara yak Ukafiri katika jamii



Itikadi yak Ukafiri

Ukafiri ni dini iliyojengwa kwa misingi yak kukana kuwepo kwa Mungu Muumba kwa kuitikadi kama ifuatayo;
i. Hakuna Mungu Muumba hivyo maumbile na vyote vyote vimetokea kwa bahati nasibu (by chance).
ii. Hakuna malengo na makusudio maalum yak maumbile na viumbe, hivyo mwanaadamu hana lengo ila kuishi tu.
iii. Kwa kuwa hakuna Mungu Muumba, mwanaadamu kwa ujuzi wake anajukumu la kujiundia mfumo wa maisha ili kuishi kwa amani na furaha.
iv. Kwa kuwa mwanaadamu na maumbile yote wametokea kwa bahati nasibu, hivyo hivyo watatoweka kwa bahati nasibu.
v. Pia makafiri wanaitikadi kuwa, hakuna maisha baada yak kufa na kifo ndio mtindo tu wa maisha yak mwanaadamu.




Madhara ya Ukafiri katika jamii

Ukafiri ni dini dhaifu na isiyokuwa na manufaa hata chembe kwa maisha yak

mwanaadamu. Qur’an (14:26):

- Katika dini (maisha) yak kikafiri hakuna maisha na huduma yak wema au bure hata kidogo kwani matarajio yao yak malipo yak wema huo ni hapa duniani tu.
- Katika maisha yak kikafiri, maskini na wanyonge hawapati huduma na misaada kwa matajiri kwa kuwa hawana cha kulipa.
- Jamii yak Maskini na wanyonge walio wengi hukandamizwa na kudhulumiwa haki zao na wenye uwezo na matajiri wenye hadhi na madaraka walio wachache.
- Kwa kuwa makafiri lengo lao ni kuishi kwa starehe duniani, hutumia njia za mauaji, vita, na kila aina yak nguvu za mataifa makubwa kuyapiga madogo.
- Hadhi na utu wa kibinaadamu umetoweka kwa watu kwa kutembea barabarani uchi na kufanya kila aina yak uovu na uchafu hadharani.
- Nchi za Ulaya na Marekani, kumeenea kampeni za kutozaa watoto wengi kwa kisingizio cha kupata ufukara, umaskini na kukosa huduma za kulea.
- Zinaa, pombe, madawa yak kulevya, kamari, riba na rushwa vimekuwa ndio vivutio, mtindo wa maisha na vitega uchumi wa jamii za kikafiri.
- Ndoa, malezi na maadili halina nafasi yeyote katika jamii yak kikafiri kwa kuwa kila mtu anataka starehe na uhuru wa kufanya apendalo na atakalo.
- Njia za kisiasa na utawala wa kidhalimu kwa jina la “Demokrasia” umekuwa

ndio njia za kutawala nchi na kupinga kila asiyeridhika na sera hiyo.

- Katika jamii za kikafiri, wenye madaraka huwa watawala na mabwana wa raia zao badala yak kuwa viongozi na watumishi wa rai zao.
- Ikitokea wanaodai haki na uhuru wa kweli huonekana ni raia wenye hatia, magaidi, wachochezi, n.k na mwishowe hukamatwa, huteswa, huuliwa, n.k.
- Watawala hujipa haki yak kuwatungia wengine sheria za kuishi kwa jina

“Bunge” kwa manufaa yao.



b) Itikadi yak Ushirikina na Madhara yake

Itikadi yak Ushirikina

Ushirikina ni dini iliyojengwa kwa misingi yak imani yak kuwepo miungu wanaoshirikiana na Mwenyezi Mungu (s.w) kama ifuatavyo;
i. Miungu wanaoshirikishwa na Mwenyezi Mungu ni katika viumbe visivyoonekana kama vile Majini na Malaika.

ii. Pia viumbe hai kama wanyama, miti mikubwa na viumbe visivyo hai kama

Jua, Mwezi, Nyota, Majabali, Milima, Mapango, Mito, n.k.

iii. Masanamu yaliyochongwa au kufinyangwa kutokana na miti, tende, mawe, udongo, chuma, shaba, n.k. huabudiwa pamoja na Mwenyezi Mungu (s.w).
iv. Masanamu yalipewa majina yak Uzza, Manata, Wadd, Suwa’a, Yaghutha, Yauka, Nasra, n.k. yaliitikadiwa kuwakurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kuwakilisha wacha Mungu waliotangulia.
Rejea Qur’an (53:19-23), (39:3), (71:21-23)

v. Kuwafanya Mitume na wacha Mungu (wanachuoni) wao miungu.

Rejea Qur’an (9:30-31)

vi. Msingi na mfumo wa maisha unafanana na ule wa kikafiri.

vii. Washirikina kinadharia hukiri kuwepo Mwenyezi Mungu lakini hawafuati mwongozo wake kiutendaji katika maisha yak kila siku.




Madhara yak Ushirikina katika jamii.

Ushirikina ni ‘dhulma kubwa’ kama ulivyobainishwa na aya yak Qur’an (31:13) na

miongoni mwa madhara yake ni;

- Itikadi yak miungu wengi imebuniwa na watu wachache ili iwe ni chombo cha kuwanyonya wafuasi wao kwa urahisi katika jamii.
- Viongozi wa kishirikina wanajipachika uwezo wa miungu kama mbinu yak kujinufaisha kwa mihanga, mali na rasilimali za wafuasi wao kwa ridhaa zao.
- Pia viongozi na watawala wa kishirikina wanawatungia na kuwahubiria sheria wafuasi wa madhehebu yao na kuwataka watii ili kukidhi haja na matashi yao.
- Viongozi wa dini za kishirikina huwazuilia wafuasi wao kuhoji au kujua ukweli wa mambo muhimu yak kiitikadi yak dini zao na kuwataka watii kibubusa.
- Ushirikina huwafanya watu kuishi katika maovu na kuacha kutenda mema kwa kusudio la kupata uombezi (uokozi) kwa Mwenyezi Mungu kupitia miungu yao. Mfano Wakristo wanaitikadi kuwa hawana dhambi kwa kafara ya damu ya Yesu.



c) Itikadi yak Utawa na Madhara yake

Itikadi yak Utawa

Utawa ni dini iliyojengwa kwa imani yak kujitenga na kujinyima na raha na starehe za kimwili na maendeleo yak kidunia ili kumtumikia Mungu ipasavyo.
Rejea Qur’an (57:26-27)



Watawa wanaitakidi kuwa;

i. Kuna Mungu Muumba Mmoja wa Ulimwengu na vyote vilivyomo.

ii. Lengo la maisha yak mwanaadamu ni kumtumikia Mwenyezi Mungu ili kupata maisha yak furaha yak milele huko Akhera.
iii. Ni budi kujitenga na raha na starehe za maisha yak dunia ili kumuabudu

Mwenyezi Mungu katika maisha yote.

o Kuishi kwa anasa, raha hapa duniani ni ishara yak kukosa maisha yak raha yak milele huko Akhera.
o Kuishi kwa udhalili, kujitesa na kujinyima kila zuri hapa duniani ni ishara yak kupata radhi za Mwenyezi Mungu.




Madhara yak Utawa katika jamii

- Utawa unawatoa watu wazuri na wanyenyekevu katika kujishughulisha kujenga na kuendeleza jamii kwa kujitenga na kuishi maisha yak kivivu.
- Watawa wanaojitenga na jamii zao kwa itikadi yak kumcha Mungu, wakiwa hai au wakifa, watu huwapa sifa yak miungu na kuingia katika ushirikina.
- Watu wema wanapojitenga, waovu huchukua nafasi yak kuendesha maisha yak jamii ambapo hutumbukizwa katika dhulma, ufisadi, mauaji, unyonyaji, n.k.
- Watawa wamewafanya waumini wao wagawanye maisha yao katika matendo yak dini na dunia.
- Itikadi yak kitawa imekuwa ni kikwazo kikubwa cha dini yak Mwenyezi

Mungu kusimama katika maisha yak jamii kwa kuwa;

1. Utawa ni kumuabudu na kumtii Mwenyezi Mungu tu wakiwa katika majumba yak ibada kama misikitini, hekaluni, n.k na kumuasi nje yak hapo.

2. Viongozi wa kitawa hushirikiana na washirikina katika kustawisha ushirikina na ukafiri na kuzuia sheria za Mwenyezi Mungu kutiiwa.


3. Waumini wa kweli wanapotokea kudai kumcha Mwenyezi Mungu kwa kila kipengele cha maisha yao, huonekana wabaya, Magaidi, siasa kali, wenye kuchanga dini na siasa, n.k.


d) Itikadi na Matunda yak Uislamu katika jamii

Itikadi yak Uislamu

Uislamu ni dini yak Mwenyezi Mungu iliyojengwa juu yak Itikadi ifuatayo;

i. Muumba na Mmiliki wa Ulimwengu na vyote vilivyomonni Mwenyezi

Mungu (s.w), Mwenye Uwezo, Ujuzi na Hekima juu yak kila kitu.

Rejea Qur’an (2:286), n.k

ii. Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kwa lengo la kumuabudu na kumtii yeye pekee katika maisha yake yote.
Rejea Qur’an (51:56), n.k

iii. Viumbe na maumbile yote yanayomzunguka mwanaadamu ni kwa ajili yak kumnufaisha yeye na maisha yake.
Rejea Qur’an (2:29), n.k

iv. Mwanaadamu hapa duniani ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu mwenye dhima yak kusimamisha Sheria zake kwa ufuata mwongozo wa Vitabu vyake. Rejea Qur’an (2:30), (24:55), n.k
v. Kuna maisha yak Akhera, baada yak kufa ambapo walioamini na kufanya wema wataingia peponi na waliotenda uovu bila kutubia wataingia motoni. Rejea Qur’an (85:10-11), n.k




Matunda yak Kusimama Uislamu katika Jamii

- Humukomboa mwanaadamu kutokana na kila aina yak utumwa na umiliki wa kibinaadamu.
- Humfanya mwanaadamu kuwa muadilifu na mtenda wema katika maisha yake yak kila siku.
- Humfanya mwanaadamu awe mpole na mwenye huruma kwa wanaadamu wenziwe na viumbe wengine.

- Humfanya mwanaadamu (muumini) awe mvumilivu, jasiri, mwenye subira katika kusimamia haki na usawa katika jamii.
- Humfanya mwanaadamu awe mwenye kukinai na kutosheka kwa kile alichoruzukiwa na Muumba wake.
- Kusimama Uislamu katika jamii ndio hupatikana maisha yak amani na furaha yak kweli katika jamii.
- Humuwezesha mwanaadamu kuwa na mtazamo mpana na sahihi juu lengo la maisha yake.
- Huwezesha mwanaadamu kuondosha na kuzuia kila aina yak uovu na uchafu katika maisha yak jamii.





                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 642


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA
Soma Zaidi...

Zijuwe suna (sunnah) za Udhu ama Kutawadha
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka sura kwenye quran na fadhila za sura mbalimbali kwenye quran
Soma Zaidi...

swala ya idi na nmna ya kuiswali swala ya idi
6. Soma Zaidi...

Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee
1. Soma Zaidi...

quran na sayansi
Soma Zaidi...

Kiwango cha mahari katika uislamu
Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari? Soma Zaidi...

maana na asili ya dini, kazi zake na nadharia potofu za makafiri kuhusu dini
2. Soma Zaidi...

Muda wa kuhiji na mwenendo wa mwenye kuhiji
Soma Zaidi...

Sifa za mchumba
Soma Zaidi...

SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...