Muda wa Hijja
Ibada ya Hija hufanywa katika muda maalum wa mwaka kama inavyosisitizwa katika Qur-an:
“Hija ni miezi maalum...” (2:197).
Miezi iliyowekwa kwa ajili ya Muislamu kunuia kuizuru Ka’ba kwa ajili ya Hija ni mwezi wa Shawwal, mwezi wa Dhul-Qaadah (mfungo pili) na siku kumi za mwanzo za mwezi wa Dhul-Hijah. Wakati wowote katika miezi hii mtu anaweza kwenda Makka kwa ajili ya Hija, lakini hataweza kufanya matendo ya Hija mpaka uanzie mwezi wa Dhul-Hija. Siku za Hija ni kuanzia tarehe 8 Dhul-Hija mpaka tarehe 13 Dhul-Hija.
Mwenendo wa mwenye kunuia Hija au ‘Umra
Mwenye kunuia kuhiji katika miezi hiyo iliyotajwa, analazimika ajipambe na tabia nzuri.Ajizuilie na maneno na matendo machafu na maovu. Ajitahidi kuishi na watu kwa wema, awatake radhi kwa yale yote mabaya aliyowatendea na azidishe kuwatendea wema.Allah (s.w) anatuagiza:
... Na anayekusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija.
Na kheri yoyote mnayoifanya Mwenyezi Mungu huijua ....” (2:197).
Mwenye kuhiji au kufanya ‘Umra anatakiwa ajipambe na tabia hiyo njema kwa kipindi chote atakapokuwa safarini. Yafuatayo ni mambo muhimu anayotakiwa ayazingatie mtu anapokuwa katika safari ya Hija au Umra.
(i)Ajiepushe na maneno maovu na machafu, pia ajiepushe na vitendo viovu na vichafu.
(ii)Azidishe kusoma Qur’an na Kuswali swala za faradhi kwa jamaa, kuswali swala za sunnah, kuomba msamaha na kutubu kikweli kweli kwa Mola wake.
(iii)Ajitahidi kuwa mwema na mpole kwa wasafiri wenzake, kuongea nao vizuri, kuwapa msaada wanaohitajia, kuwasamehe kwa kosa lolote watakalomfanyia, kujizuia na hasira na kuvumilia maudhi mengi yanayotokana na wasafiri wenzake au wenyeji wa sehemu za Hija.
(iv)Ajitahidi kuchanganyika na wasafiri wenzake kutoka sehemu mbalimbali, ajitahidi kujihusisha kwenye mikutano na mazungumzo ya kheri na kujaribu kubadilishana mawazo na wenzake kutoka sehemu mbalimbali ambao wanaelewana lugha, juu ya usimamishaji Uislamu ulimwenguni.
(v)Ajitahidi kuinamisha macho yake katika makundi yenye mchanganyiko wa wanawake na wanaume na kila itakapowezekana ajiepu she kuwa katika mchanganyiko wa wanaume na wanawake.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 510
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Kitabu cha Afya
Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu, sifazao na lengo la kuletwa kwao
1. Soma Zaidi...
SIKILIZA QURAN KUTOKA KWA WASOMAJI WA TANZANIA
Soma Zaidi...
Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram
Soma Zaidi...
Swala ya Kuomba Toba (tawbah) na namna ya kuiswali
Soma Zaidi...
Namna ya kuswali swala ya kuombea haja
9. Soma Zaidi...
NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA
Soma Zaidi...
Ni nini maana ya ndoa?
Soma Zaidi...
Taratibu za mahari katika uislamu
Soma Zaidi...
nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji
2. Soma Zaidi...
Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke?
Je, Mahari inashusha hadhi ya mwanamke? Soma Zaidi...
Namna ya kutufu, na masharti ya mwenye kutufu
3. Soma Zaidi...
ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli
Ukweli ni uhakika wa jambo. Soma Zaidi...