Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.
Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku.
Muumini wa kweli huishi katika kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu wa taratibu na kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w), na hii kama ifuatavyo;
(i)Kupata ukombozi kutokana na utumwa wa aina zote;
Huu hupatikana baada ya mtu kuwa huru na kuishi kwa kufuata taratibu na kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.
Rejea Qur’an (12:39).
(ii) Mwanaadamu huwa mwadilifu katika utendaji wa maisha yake ya kila siku;
Muumini wa kweli hufanya mema na kuepuka maovu bila hata ya kusimamiwa au kuonekana na watu, kwa kujua kuwa mjuzi pekee ni Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (50:16).
(iii) Humfanya mwanaadamu kuwa mpole, mvumilivu na mwenye huruma;
Mwanaadamu huwa mpole hasa kwa wenye shida na matatizo na pia kuwa na subra anapofikwa na mitihani na kujiepusha na kibri, majivuno na kujiona.
Rejea Qur’an (6:165).
(iv) Humfanya mja kuwa jasiri katika kusimamia haki, uadilifu na usawa katika jamii;
Muumini wa kweli huwa shujaa katika kupambana na dhulma na ukandamizaji wa aina yeyote na kupigania haki bila kumchelea mtu yeyote.
Rejea Qur’an (4:74), (5:45) na (9:111).
(v) Humfanya mja kuwa na mtazamo mpana na sahihi juu ya maisha;
Muumini wa kweli kamwe hawi na fikra na mtazamo finyu katika kuyaendea maisha yake ya kila siku kwa kujua lengo, thamani na nafasi yake juu ya maisha ya Akhera.
Rejea Qur’an (15:9).
(vi) Humuwezesha mja kuwa mwenye kukinai na kutosheka;
Muumini wa kweli hutosheka na kuridhika na kile alichokadiriwa na Mwenyezi Mungu (s.w) iwe kwa kupungukiwa au kuzidishiwa, yote kwake anashukuru.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.
Soma Zaidi...