image

SHIRK

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

SHIRK

1.2.Shirk.
Maana : Shirk ni kinyume cha Upweke au Umoja (Tawhiid)
Maana ya Kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w):
Ni kujaalia kinadharia au kiutendaji kuwa kuna miungu wengine wanaoshirikiana na Mwenyezi Mungu (s.w) katika kuongoza na kuendesha Ulimwengu.

Aina za Shirk.
Kuna aina kuu nne za shirk,
1.Shirk katika Dhati ya Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Dhaat).
2.Shirk katika Sifa za Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Sifaat).
3.Shirk katika Mamlaka ya Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Ikhtiyaar).
4.Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Ah-kaam).

1. Shirk katika Dhati ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kujaalia au kuvinasibisha viumbe na uungu kwa kuvipa majina rasmi kama washirika wa Mwenyezi Mungu (s.w) na kuviendea kwa unyenyekevu na ibada maalum kama, kuvisujudia, kuchinja na kuviomba msaada.
Rejea Qur’an (25:2-3), (22:73) na (29:41).

2. Shirk katika Sifa za Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kuwasifu au kuwatukuza viumbe kiwango anachostahiki kusifiwa au kutukuzwa Allah (s.w) peke yake. Kama kuomba dua, baraka na msaada kupitia kwa Wacha-Mungu, mfano kwa baraka za Mtume, Abdul-Qadir, Sharifu au Sheikh fulani n.k.
Rejea Qur’an (53:32), (10:62-64), (2:180), (17:110) na (40:60).

3. Shirk katika Mamlaka ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kuwakabidhi viumbe mamlaka kamili ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kuwatii kwayo kama vile kuongoza, kulisha, kulea, kulinda n.k katika maisha ya kila siku kinyume na nafasi au uwezo wao.
Rejea Qur’an (9:31) na (2:208).

4. Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kutunga sheria au hukumu kinyume na sheria au hukumu za Mwenyezi Mungu (s.w) alizoziainisha katika vitabu vyake vitukufu na kuzitumia kuhukumu kwazo katika uendeshaji wa maisha ya kila siku.
Rejea Qur’an (5:38), (24:2), (33:36), (5:44-45, 47) na (5:50).

Kina cha Uovu wa Shirk.
oNi dhulma kubwa kuliko zote na ndio chanzo cha matatizo yote ulimwenguni.
Rejea Qur’an (31:13) na (10:35-36). oNi dhambi kubwa kuliko zote isiyosameheka ila apende Mwenyezi Mungu (s.w) na kutubia kikweli kweli kabla ya kufa.
oNi dhambi inayofuta mema yote ya mtu aliyoyafanya kabla ya kushirikisha.
Rejea Qur’an (4:48), (4:116) na (39:65).

Maana ya Kumuamini Mwenyezi (s.w) katika maisha ya kila siku.
Ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kufuata barabara mwongozo wake katika utendaji wa wetu wa kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku kwa kufanya moja kati ya mambo yafuatayo;
oKusimamisha Tawhiid (Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu) na
oKujiepusha na Shirk za aina zote.


                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 502


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-