 Tawhiid.
oKimaana: Ni Umoja au Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w).
oKimatumizi: Ni fikra, mtazamo wa kimapinduzi katika kumkomboa mwanaadamu na aina zote za utumwa wa kibinaadamu na kuwa mtumishi huru wa Muumba wake.

Aina za Tawhiid.
Kuna aina kuu tatu za Tawhiid kama zilivyoainishwa katika aya za Qur’an.
(i) Tawhid Al-Uluuhiyyah – Upweke wa Allah (s.w) katika Uungu wake. Nayo ni Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika Uungu wake kwa kutokuwa na mungu mwingine yeyote wa kumuelekea kwa ibada au maombi isipokuwa yeye peke yake. Rejea Qur’an (2:163), (3:62) na (112:1-4).

(ii) Tawhiid Al-Asmaa Wassifaat – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Majina na Sifa. Nayo ni kutomsifu Mwenyezi Mungu (s.w) kwa sifa za viumbe au majina ya viumbe na pia kutomsifu kiumbe yeyote kwa sifa za Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an (57:1-6) na (59:22-24).

(iii) Tawhiid Rabbuubiyya – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Ubwana,Utawala na Mamlaka Yake. Kumpwekesha Allah (s.w) katika Ubwana na Utawala wake ni kutofuata na sheria na taratibu za maisha kinyume na zile alizoziweka yeye kwa kumfanya ndiye Mlezi, Mlinzi, Mwendeshaji wa kila kitu. Rejea Qur’an (4:59), (31:14-15), (25:52), (3:149), (3:100) na (5:57). bofya hapa