image

Ni nini maana ya ndoa?

Ni nini maana ya ndoa?

Maana ya NdoaNdoa, kwa ujumla, ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii. Kwa mfano, hapa Tanzania mume na mke watatambulika kuwa wameoana kisheria, pale watakapokuwa wamefunga mkataba wa kuishi pamoja mbele ya Mkuu wa wilaya au mbele ya walii na mashahidi wawili (ndoa ya kiislamu)au mbele ya Padri (Kanisani).Ndoa ya Kiislamu ni mkataba wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa kuzingatia masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislamu. Ndoa yoyote iliyofungwa kinyume na masharti na taratibu za Kiislamu, haikubaliki kwa Waislamu.Umuhimu wa Ndoa kwa Mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:Katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa ndoa ni katika sunnah yake na akaongeza kusema: "Yeyote anayekataa sunna yangu sipamoja nami ".Anas (r.a) amesema kuwa Mtume wa Allah amesema, 'Mtu anapooa huwa amekamilisha nusu ya dini, kisha amche Allah ili akamilishe nusu iliyobakia." (Bukhari).Ndoa inasisitizwa kutokana na umuhimu wake katika kuijenga na kuiendeleza jamii kwa:
(i)Kuihifadhi jamii na zinaa.
(ii)Kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri.
(iii)Kujenga mapenzi na huruma katika familia.
(iv)Kukuza uhusiano na Udugu katika jamii.
(v)Kukilea kizazi katika maadili mema.
(vi)Kuwafanya watu wawajibike ipasavyo.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 701


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-