Navigation Menu



Vituo vya kunuia ibada ya hija

Vituo vya kunuia ibada ya hija

Vituo vya kunuia Hija



Miongoni mwa mambo muhimu kwa wenye kuhiji au kufanya ‘Umra ni kufahamu vituo ambapo watanuia kuanza kuhiji rasmi na kuvalia vazi la Ihram. Vituo hivi huitwa Miiqaat. Miiqaat ni vituo maalum vilivyowekwa katika njia za sehemu mbali mbali za kuingilia sehemu takatifu (Haram) ya Makka ambapo mahujaji wakifika humo huvua nguo zao za kawaida na kuvalia vazi rasmi la Ihram na kunuia rasmi kuanza ibada ya Hija au ‘Umra. Vituo vya kunuia Hijja alivyoviweka Mtume (s.a.w) kwa watu wa kutoka kila upande ni hivi vifuatavyo:



(i)Zul-Hulaifa: - ni kituo cha watu wanaotoka sehemu za Madina. Kituo hiki kiko umbali wa kilometa 450 kutoka Makka. Hivi sasa kituo hiki kinajulikana kwa jina la Bir-’Ali.



(ii)Juhfah: Kituo hiki kiko umbali wa Kilometa 187 Kaskazini-Magharibi ya Makka. Ni kituo cha watu wanaotoka sehemu za Misr, Sham (Syria), n.k. Hivi sasa kituo hiki kinajulikana kwa jina la Rabigh.



(iv) Qurnul Manazil: - Kituo hiki kiko umbali wa Kilometa 94 mashariki ya Makka na ni kituo cha watu kutoka mji wa Najd. Kituo hiki hivi sasa kinajulikana kwa jina la Sail. Yalamlam: Kituo hiki kiko umbali wa kilometa 54 kusini magharibi ya Makka: Ni kituo cha watu kutoka Yemen na sehemu nyingine za kusini kama vile Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kusini, n.k.



(v) Makka: Wakazi wa Makka watavalia Ihram na kunuia Hija au ‘Umra humo humo majumbani mwao. Vile vile wakazi wa vituo vingine, vilivyotajwa hapo juu, watanuia Hija au ‘Umra na kuvalia Ihram humo humo majumbani mwao. Vituo hivi vitano vimebainishwa katika Hadith ifu atayo:


Ames imulia Ibn Abbas (r.a) kuwa Mtume wa Allah ameweka Dhul-Hulaifa kama Miiqaat ya watu wa Madina; Al-Juhfa kwa watu wa Sham (Syria); Qarn ul-Manaazil kwa watu wa Najd; na Yalamlam kwa watu wa Yemen. Kwa hiyo hivi ni vituo (Mawaaqiit) kwa wale wote wanaoishi katika vituo hivi na wale wanaopitia katika vituo hivi kw a nia ya Kuhiji au kufanya ‘Umra na yeyote anayeishi katika sehemu hizi atavalia Ihram nyumbani kwake, hali kadhalika wakazi wa Makka wanaweza kuvalia Ihram humo humo Makka. (Bukhari).



(vi)Dhaaru-Irq: Kituo hiki kipo umbali wa kilomita 94 kaskazini-mashariki ya Makka. Ni kituo cha watu wa Iraq, Iran, n.k. Kituo hiki hakikuwekwa na Mtume (s.a.w) bali kiliwekwa na ‘Umar bin Khattaab (r.a) alipokuwa Khalifa kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo:
Amesimulia Ibn Umar (r.a): Wakati miji hii miwili (Basra na Kufa) ilipotekwa, watu walikwenda kwa ‘Umar (r.a) na kusema: Ee Amir wa Waumini, Mtume (s.a.w) ameweka Qarn kama Miiqaat ya watu wa Najd, lakini iko kinyume kabisa na njia yetu na ni vigumu sana kwetu kupitia hapo. Akasema, (Umar), fanyeni kituo (miiqaat) chenu katika sehemu iliyo kinyume na Qarn ambayo iko katika njia yenu ya kawaida. kwa hiyo aliiw eka Dhaaru-irq kam a Miiqaat. (B u kh a ri)


(vii) Jiddah: Miiqaat ya Wasafiri wa ndege. Kama ilivyosisitizwa katika Hadith watu kutoka sehemu mbali mbali wanalazimika kuvalia Ihram na kunuia Hija au ‘Umra katika vituo vilivyowekwa endapo watapitia humo. Ilivyo ni kwamba vituo vyote hivi vilivyotajwa katika Hadith hizi vinapitiwa na wasafiri wa gari au wanyama. Wasafiri wengi wanaotoka nchi za mbali husafiri kwa ndege mpaka Jiddah na hapo ndipo wanapovalia Ihram na kunuia Hija au ‘Umra. Jiddah iko kilomita 72 kutoka Makka.




                   


Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 635


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula Mbegu za maboga
Soma Zaidi...

Athari na faida za kumuamini Allah katika maisha ya mwanadamu duniani na akhera
Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s. Soma Zaidi...

NAFASI YA SUNNAH KATIKA UISLAMU
Nafasi ya Sunnah katika UislamuMtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

Taratibu za mahari katika uislamu
Soma Zaidi...

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
1. Soma Zaidi...

Hizi ndizo aina tatu za Hija
Soma Zaidi...

Taratibu za kufunga ndoa na kumuinglia mke
Soma Zaidi...

swala ya kuomba mvua na namna ya kuiswali
12. Soma Zaidi...

maana na asili ya dini, kazi zake na nadharia potofu za makafiri kuhusu dini
2. Soma Zaidi...

MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...