Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu
a) Wakati wa Ukhalifa wa Uthman bin Affan (r.a)
- Dola ya Kiislamu ilianza kuporomoka nusu ya pili ya uongozi wa Khalifah, Uthman bin Affan (r.a).
- Wanafiki wakiongozwa na Abdullah bin Sabaa, walizua fitna na kumtuhumu kiongozi wa Dola na kuanzisha imani na itikadi potofu.
- Wapinzani wa Dola ya Kiislamu walijiimarisha na kutuma wajumbe watatu kutoka Misri, Basra na Kufa kwa Khalifa kuwasilisha malalamiko yao.
- Wajumbe hao walirejesha fitina kwao kuwa ujumbe wao umepuuzwa na Khalifa, hivyo wakaandaa jeshi la askari 1000 ili kuangusha utawala wa Uthman (r.a).
- Wakazi wa Madina walipambana na waasi hao lakini walizidiwa nguvu na
hatimaye kuingia hadi Msikitini na kumuua Khalifa akiwa anasoma Qurāan.
b) Wakati wa Khalifa Ali bin Abi Taalib (r.a)
- Baada ya kuuliwa Uthman (r.a), wapinzani walishikilia mji wa Madina kwa siku sita na kuongoza wao na siku ya 6 walimtangaza Ali (r.a) kuwa ndiye Khalifa.
- Uchaguzi huu wa Ali (r.a) haukukubalika kwa Waislamu, na kuwagawa waislamu makundi manne.
i. Vita kati ya Bi Aisha (r.a) na Khalifa Ali (r.a), Vita vya Jamal (Ngamia)
- Bi Aisha (r.a) waliungana na Talha na Zubair (r.a) na kuandaa jeshi la kulipiza kisasi cha kuuliwa Uthman (r.a).
- Ali (r.a) walifanya sulhu na Bi Aisha pamoja na Muaāwiya (r.a) kwa kuafikiana kuwa Khalifa Ali (r.a) atawaadhibu wauaji wa Uthman (r.a) Dola ikiwa na amani.
- Mpinzani mkubwa, Abdullah bin Sabaa na jeshi lake walivuruga sulhu hiyo na vita vikapiganwa mji wa Basra na waislamu 10,000 walikufa.
ii.Vita kati ya Khalifa Ali (r.a) na Muaāwiya; Vita vya Sifin
- Wakati Ali anatawazishwa Ukhalifa, Muaāwiya alikuwa Gavana wa Syria, Khalifa Ali alimvua ugavana Muaāwiya lakini Muaāwiya alikataa.
- Khalifa Ali (r.a) aliandaa jeshi na kupigana na jeshi la Muaāwiya huko
Syria sehemu iitwayo Sifin mnamo mwaka 36 A.H.
- Musa Ashaār (r.a) kwa upande wa Khalifa walifanya sulhu na Amr bin Al- As (r.a) kwa upande wa Muaāwiya (r.a) lakini wauaji wa Uthman hawakutaka sulhu na kuamua kujitenga na kupambana na Khalifa Ali na Muaāwiya (r.a).
- Kundi hili lililojitenga na Khalifa Ali (r.a) liliitwa āKhawaarijā
(waliojitenga).
iii.Kuuliwa Khalifa Ali bin Abi Twalib (r.a)
- Khawaarij walipanga njama za kumuua Muaāwiya, Ali na Amr bin Al-As (r.a) aliyekuwa mshauri wa Muaāwiya (r.a) mwaka 40 A.H.ndani ya swala ya Alfajir.
- Muuaji wa Ali (r.a) alimjeruhi Ali vibaya kwa upanga wa sumu na hatimaye akafa siku ya 3 yake.
- Wauaji wa Muaāwiya na Amr (r.a) hawakufanikiwa kwani Muaāwiya na
Amr (r.a) hawakufika msikitini swala ile.
- Baada ya kuuliwa Ali bin Abi Twalib (r.a), mtoto wake Hassan alichaguliwa kushika nafasi ya Ukhalifa.
- Muaāwiya aliandaa jeshi na akapambana na Hassan (r.a) na mwishowe walikubaliana kuwa, Muaāwiya achukue Ukhalifa na baada ya kufa, uongozi utakuwa chini ya Hussein bin Ali (r.a).
- Kinyume na makubaliano, Muaāwiya kabla hajafa alimteua mtoto wake
Yazid kushika uongozi wa Dola baada yake.
- Dola ya Kiislamu iliyoasisiwa na Mtume (s.a.w) ikaporomoka na ufalme
ulioasisiwa na Muaāwiya ukachukua nafasi.
Mafunzo yatokanayo na kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu
i. Ni muhimu na wajibu kwa waislamu kuwa makini katika kuandaa na kuchaguzi viongozi wa Kiislamu kwa mujibu wa malengo yao.
ii. Maadui wa Uislamu hawatarudi nyuma kamwe katika kuupiga vita Uislamu na waislamu.
iii. Mgawanyiko wa kimakundi ndani ya umma wa Kiislamu ndiye ufa pekee unaopelekea kudhoofika Uislamu na waislamu.
iv. Kuwabaini wanafiki na maadui wa Uislamu na mbinu zao ni jambo la msingi mno katika kuendesha harakati za Kiislamu.
v. Waislamu watakapokuwa tayari kikweli kweli kuupigania Uislamu, Uislamu utachukua hatamu yake yak kuongoza maisha ya jamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno ĀSwalaatĀ lina maana ya Āombi au Ādua.
Soma Zaidi...Mayahud Mwanzoni Mayahud walipoona kuwa Waislamu wanafunga siku ya Ashura pamoja nao na wanaelekea Qibla cha Baitul- Muqaddas pamoja nao hawakuonyesha chuki ya dhahiri dhidi ya Mtume(s.
Soma Zaidi...