Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija.
Muhammad (s.a.w) KUMUOA BI KHADIJA.
Bi khadija alikuwa ni mwanamke wa miaka 40 baada ya kutengana na mumewake alikaa muda mrefu bila ya kuolewa. Bi khadija alikuwa ni mwanamke mwenye busara, fahamu kubwa na heshima pia. Alikuwa ana mali, na alikuwa akiajiri wanaume kwa kazi zake. Watu wengi walikuwa waienda kutoa posa lakini alikuwa akiwakatalia.
Katika shughuli zake za kibiashara bibi Khadija (Radhiya Llahuu anha) alikuwa akiwaajiri wanaume wawili kila mwaka. Mmoja kwa ajili ya kwenda Sham wakati wa Kusi na mwengine kwa ajili ya kwenda Yemen wakati wa Kaskazi. Na hivi ndivyo yalivyokuwa maisha ya kibiashara Bara ya Arabu yote.
Wakati huo huo Muhammad bin Abdillah (Swalla Laahu alayhi wa sallam) (kabla ya kupewa utume) alikuwa akiishi pamoja na ami yake Abu Talib baada ya kufariki kwa babu yake Abdul Muttalib, na alikuwa akimsaidia ami yake katika shughuli za kibiashara na katika kuchunga kondoo na mbuzi mpaka alipofikia umri wa miaka ishirini na mitano, na kutokana na uaminifu wake na ukweli wake, watu wa Makka walikuwa wakimuheshimu sana.
Hii ukijumuisha pia kuwa Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam) hakupata hata siku moja kuyasujudia masanamu waliyokuwa wakiyaabudu na kuyaogopa wala hakupata kunywa pombe, na hakuwa akijishughulisha na anasa wala starehe ya aina yoyote ile katika starehe walizokuwa wakijishughulisha nazo vijana wa wakati ule.
Alikuwa mwema, msema kweli, muaminifu, mwenye tabia na mwenendo mwema uliompendeza kila mtu, na alikuwa na haiba kubwa sana pale Makka hata akawa maarufu miongoni mwao kwa jina la ‘Al Swaadiqul Amin’, bimaana Mkweli Mwaminifu.au ‘Muhammad Al Amin’, na maana yake ni Muhammad muaminifu.
Sifa zote hizo zilikuwa zikimfikia bibi Khadija aliyekuwa mfanya biashara maarufu pale Makka pamoja na sifa nyingine mbali mbali, na pia zilikuwa zikimfikia habari za kusafiri kwake pamoja na ami yake Abu Talib katika shughuli za kibiashara kwenda nchi ya Sham, na kwamba ami yake alikuwa akipata faida kubwa sana tokea alipoanza kushirikiana naye katika shughuli hizo.
Habari hizo zikawa zinamshughulisha sana bibi Khadija na usiku mmoja katika siku za joto alipokuwa amekaa juu ya dari la nyumba yake pamoja na mwanamke mmoja aitwae Nafisa binti Munabih, bibi Khadija alikuwa akitazama chini sana huku akitafakari, jambo lililomfanya Nafisa amuulize:
“Unatafakari juu ya nini ewe Khadija?”
Bi Khadija:
“Natafakari juu ya jambo la ajabu sana”
. Bi Nafisa:
“Unanificha mimi?”
Bi Khadija: “Mimi siwezi kukuficha kitu ewe Nafisa, jambo lenyewe linahusiana na Muhammad bin Abdillah!”.
Bi Nafisa:
“Ah! Muhammad Muaminifu. Unataka nini kwake?”
Bi Khadija:
“Muhammad Muaminifu husafiri baadhi ya wakati kwa ajili ya shughuli za kibiashara pamoja na ami yake Abu Talib, ningefurahi kama angekubali pia kushughulikia biashara zangu maana yeye ni mtu wa pekee ninayeweza kumuaminisha katika mali yangu. Lakini sijuwi vipi nitaweza kumjulisha?”
Nafisa:
“Mimi, mimi ndiye nitakayemjulisha ewe Khadija, lakini nitazungumza na ami yake Abu Talib maana naona haya kumkabili Muhammad juu ya jambo hili.” Abu Talib akalikubali ombi hilo na akamnasihi Muhammad akubali pia, na Mtume (Swalla Llaahu alayhi wa sallam) akamwambia ami yake: “Ikiwa wewe unaona sawa, basi na mimi nimekubali”.
Bibi Khadija alifurahi sana alipojulishwa kuwa Muhammad (Swalla Llaahu alayhi wa sallam) amelikubali ombi lake, akatayarisha msafara wa biashara na kumtaka mtumishi wake Maysara afuatane na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam) kwa ajili ya kumhudumia na kumshughulikia katika safari ndefu hiyo.
Muhammad (Swalla Llaahu alayhi wa sallam) akafanikiwa kuuza bidhaa zote za bibi Khadija katika masoko ya Sham na akarudi akiwa amempatia faida kubwa sana kuliko alivyowahi kupata miaka yote iliyopita.
RUDINAE MAKA HARAKA SANA
Tokea waliporudi kutoka safari ya Sham yule kijana Maisara aliyevutiwa sana na tabia na mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alouona walipokuwa safarini, akawa anamuhadithia bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) juu ya yale aliyokuwa akiyaona safarini walipokuwa wakienda na walipokuwa wakirudi na baadhi ya miujiza iliyokuwa ikitokea.
Bibi Khadija naye aliyekuwa wakati wake wote anawaza juu ya Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam) alikuwa akipenda kila mara kuhadithiwa juu ya sifa zake hizo, na siku moja alipokuwa amekaa pamoja na mtumishi wake huyo, akamwambia: “Enhe! Hebu nihadithie vizuri juu ya safari yako na Muhammad”. Maisarah akasema:
“Sikupata kuona mtu bora wa kusafiri naye kuliko yeye. Alikuwa mtulivu, hana kiburi, mkarimu na mpole sana. Nilikuwa ninapoumwa ananishughulikia na ninapochoka ananisaidia, na alikuwa akigawana na mimi sawa sawa chakula chake na maji yake. Kwa hakika alikuwa akinitendea kama kwamba ni ndugu yake.
Lakini jambo lililonistaajabisha zaidi ewe bi Khadija,” akaendelea kusema: “kulikuwa na kiwingu kilichokuwa kikimfuata wakati wote tokea tulipoondoka mpaka tuliporudi. Kilikuwa kikimfuata na kumkinga na juwa kali wala hakuwa akihisi joto hata kidogo wakati wote wa safari. Isitoshe, Muhammad hapendi kusema sana, na kila tunaposimama kwa ajili ya kupumzika alikuwa akijitenga peke yake na alikuwa akipenda kutizama mbinguni kwa khushuu na mdomo wake ulikuwa daima ukitikisika huku akisema maneno yasiyosikika”.
Bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) aliyekuwa na shauku ya kutaka kujuwa zaidi habari za Muhammad akasema: “Enhe! Kisha? Endelea, nini kilichotokea baadaye?” Maisarah akasema:
“Tulipokuwa tukirudi Makka, tulisimama mahali muda mdogo kwa ajili ya kujipumzisha, na mimi nikaondoka kwenda kutafuta chakula cha ngamia, na mahali hapo palikuwa na mti mkubwa sana na Muhammad alikaa chini ya mti huo huku akitizama mbinguni kama kawaida yake kama kwamba anatafuta kitu, na karibu na mahali hapo palikuwa na hekalu la mcha Mungu mmoja aitwae Nastwur aliyenijia mimi na kuniuliza:
“Nani huyu kijana aliyekaa chini ya mti ule?”
Nikamwambia;
“Huyu ni kijana anayetokana na mabwana wa kabila la Kikureshi”.
Akaniambia:
“Umeona lolote lisilo la kawaida kutoka kwake?”
Nikamwambia:
“Nimeona kiwingu kikimfuata kikimkinga kutokana na jua kali tokea tulipoondoka na wala hakikumuacha abadan”.
Akauliza tena:
“Macho yake yakoje?”
Nikamjibu:
“Meusi na makubwa na katika weupe wake umo wekundu khafifu ndani yake”.
Akasema:
“Kijana huyu atakuwa na shani kubwa, rudi naye Makka haraka sana, kwani hakupata kukaa chini ya mti huu isipokuwa Nabii”. Maneno haya yalimtia kizunguzungu bibi Khadija na tokea alipoondoka hapo akawa usiku na mchana hana analowaza isipokuwa juu ya Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam).
SIFA ZA ALIYE TAKASWA
Bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akaanza kufikiri huku akikumbuka na kuunganisha maneno ya Maisarah na maneno aliyoambiwa na bin ami yake Waraqah bin Noufel, akawa anajisemesha: “Kwa nini isinipitikie wakati wote huu? Huyu ndiye kijana anayetokana na mabwana wa kabila la Kikureshi anayejulikana kwa ukweli na uaminifu na upole na ukarimu, na Makureshi wote wanamuheshimu na kumtukuza kutokana na kujitenga kwake mbali na tabia zote mbaya walizokuwa nazo vijana wa kabila la Kikureshi na wengineo. Na huyu ndiye kijana aliyesafiri na mali yangu na kunipatia faida kubwa sana, na huyu ndiye kijana ambaye kiwingu kilikuwa kikimkinga kutokana na juwa kali tokea alipoianza safari yake mpaka aliporudi. Na huyu ndiye kijana ambaye mcha Mungu Nastwur amesema juu yake kuwa atakuwa na shani kubwa akamtaka Maisarah arudi naye Makka haraka sana”.
Bibi Khadija akawa anawaza na kukumbuka yote hayo mpaka akawa na uhakika ndani ya moyo wake kuwa sifa kama hizi haziwezi kumuandama mtu wa kawaida. Sifa njema kama hizi ambazo si kila mtu anaweza kuwa nazo hazipatikani isipokuwa kwa watu waliochaguliwa na kutakaswa. Kutokana na yote haya, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akazidi kujishughulisha na kuwaza juu ya Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1685
Sponsored links
๐1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
๐2 kitabu cha Simulizi
๐3 Kitau cha Fiqh
๐4 Madrasa kiganjani
๐5 Kitabu cha Afya
๐6 Simulizi za Hadithi Audio
Imam Bukhari na Sahihul Bukhari
Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII SHUโAYB(A.S)
Nabii Shuโayb(a. Soma Zaidi...
Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kiafrika hapo zamani
3. Soma Zaidi...
Nini maana ya tabii tabiina
Soma Zaidi...
Khalifa โUmar bin Abdul Aziz
Soma Zaidi...
Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Je waislamu walishindwa vita vya Uhudi?
Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri? Soma Zaidi...
NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA) BINTI KHUWALD
MTUME Muhammad (s. Soma Zaidi...
Kuandaliwa Mtume(s.a.w) maandalizi ya kimafunzo na maandalizi ya ki ilham
Mitume huzaliwa Mitume. Soma Zaidi...
Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri. Soma Zaidi...
KAZI ALIZOFANYA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KABLA YA UTUME
KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S. Soma Zaidi...
HISTORIA NA MAISHA YA NABII ISMAIL(A.S)
Ismail(a. Soma Zaidi...